DogoWaNjombe
JF-Expert Member
- Feb 7, 2022
- 3,284
- 7,708
ACT Wazalendo imesikitishwa na taarifa na kauli za Serikali zinazotolewa kupitia vyombo vya habari, majukwaa mbalimbali na Bungeni kuhusu mwenendo wa ugharamiaji wa huduma za afya nchini, hususan utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote.
ACT Wazalendo imefanya tathmini na kubaini kuwa, licha ya Serikali kutangaza mafanikio katika utekelezaji wa mfumo huo, bado kuna matatizo makubwa katika kufikia upatikanaji wa huduma za afya bora, nafuu na kwa usawa. Na suala la Bima ya Afya kwa Wote kubaki ni ahadi hewa.
Itakumbukwa kuwa katika kampeni, CCM iliwaahidi Watanzania kuwa ndani ya siku 100 Serikali itazindua Bima ya Afya kwa Wote, kugharamia 100% matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo wenye magonjwa sugu, kuajiri wahudumu wa afya 5,000 na kuacha kuzuia miili ya marehemu hospitalini kwa sababu ya madeni.
ACT Wazalendo imefanya tathmini na kubaini kuwa, licha ya Serikali kutangaza mafanikio katika utekelezaji wa mfumo huo, bado kuna matatizo makubwa katika kufikia upatikanaji wa huduma za afya bora, nafuu na kwa usawa. Na suala la Bima ya Afya kwa Wote kubaki ni ahadi hewa.
Itakumbukwa kuwa katika kampeni, CCM iliwaahidi Watanzania kuwa ndani ya siku 100 Serikali itazindua Bima ya Afya kwa Wote, kugharamia 100% matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo wenye magonjwa sugu, kuajiri wahudumu wa afya 5,000 na kuacha kuzuia miili ya marehemu hospitalini kwa sababu ya madeni.
Kwa tathmini tuliyoifanya, utekelezaji wa ahadi za siku 100 na Bima ya Afya kwa Wote umejikita katika kujaza namba pekee, huku ukiacha mapengo makubwa; watu wengi hawajapatiwa kadi, mamilioni ya maskini hawajafikiwa, dawa na vifaa tiba havitoshelezi, na magonjwa mengi hatari hayajumuishwi kikamilifu kwenye bima ya watu maskini. Uchambuzi wa ACT Wazalendo umebaini yafuatayo;
- Mosi, kasi ndogo ya kuwafikia wananchi maskini. Kwa mujibu wa Utafiti wa Mapato na Matumizi ya Kaya Binafsi (IHBS) 2025, idadi ya watu wanaoishi chini ya mstari wa umasikini Tanzania Bara ni takribani watu milioni 16.5 (16,563,733).
- Hata hivyo, mpaka sasa ni watu 997,015 pekee walioripotiwa kusajiliwa katika Bima ya Afya kwa Wote, huku watu 501,981 kati yao wakiwa bado hawajapatiwa kadi. Kwa kasi hii, Serikali itachukua takribani miaka 20 kuwafikia wananchi maskini ambao ndio walengwa wakuu wa mpango huu.
- Pili, Bima ya Afya kwa Wote inayotangazwa na Serikali bado ina matabaka. Serikali inasema inawaunganisha Watanzania maskini na Bima ya Afya kwa Wote, lakini mfumo huo bado una madaraja manne ya vifurushi (Ngorongoro Afya, Mikumi Afya, Serengeti na Tanzanite Afya), ambapo kifurushi cha gharama ya chini cha takribani Sh 150,000 ndicho kinacholenga wananchi wenye uwezo mdogo zaidi. Kifurushi hiki kina huduma chache zaidi za kibingwa, vipimo na matibabu, huku huduma zikiongezeka kadri uwezo wa mwananchi wa kulipa unavyoongezeka.
Hii ina maana kwamba huduma bora za afya zinaongezeka kadri unavyokuwa na fedha na zinapungua kadri unavyokuwa maskini. Ni matarajio ya wananchi kuwa Bima ya Afya inayomlinda mwananchi maskini lazima ilinde dhidi ya magonjwa yanayoweza kumfilisi au kumuua, badala ya kumlinda dhidi ya sehemu ndogo tu ya gharama za matibabu. Hivyo, hii si bima ya afya kwa wote, ni mfumo wa kibaguzi, ubabaishaji, ulaghai na kuendeleza ukosefu wa usawa katika huduma za afya.
- Ahadi ya matibabu ya magonjwa sugu haijatekelezwa. Moja ya ahadi kubwa iliyotolewa wakati wa kampeni ilikuwa kwamba Serikali ingegharamia kwa asilimia 100 matibabu na vipimo vya kibingwa kwa wananchi wasio na uwezo, hususan wanaougua magonjwa kama figo, saratani, kisukari, moyo na magonjwa mengine makubwa.
Hata hivyo, utekelezaji wa Bima ya Afya kwa Wote unaonesha kifurushi kinachounganishwa kwa watu maskini hakina huduma hizo kama walivyoahidi. Bado huduma na vipimo muhimu vimeondolewa, ikiwemo huduma za kibingwa na vipimo kama uchujaji wa damu (Dialysis), MRI na CT-Scan tofauti na ahadi.
Sasa tunaweza kujiuliza, mgonjwa wa figo atapona bila kupata huduma ya uchujaji wa damu? Mgonjwa wa saratani atapona bila kupata dawa na mionzi inayohitajika? Mgonjwa wa moyo atawezaje kumudu gharama za matibabu ya kibingwa bila mfumo wa bima kumlinda?
Sasa tunaweza kujiuliza, mgonjwa wa figo atapona bila kupata huduma ya uchujaji wa damu? Mgonjwa wa saratani atapona bila kupata dawa na mionzi inayohitajika? Mgonjwa wa moyo atawezaje kumudu gharama za matibabu ya kibingwa bila mfumo wa bima kumlinda?
- Serikali imetangaza kuanza na wazee na watoto wanaoishi katika mazingira magumu. Hata hivyo, Sera ya Afya ya mwaka 2007 tayari inatambua makundi maalum, wakiwemo wazee, watoto chini ya miaka mitano na wanawake wajawazito, kama makundi yanayopaswa kupata huduma za afya bila malipo. Kwa hiyo, kuwasilisha utekelezaji wa huduma kwa makundi haya kama hatua mpya ya Bima ya Afya kwa Wote kunahitaji Serikali kutoa maelezo ya wazi kuhusu tofauti kati ya haki zilizokuwepo kisera na mafao mapya yanayotokana na mfumo wa Bima ya Afya kwa Wote.
- Serikali bado haijaondoa tatizo la kuzuiwa miili ya marehemu Hospitalini. Serikali iliahidi ndani ya siku 100 kuacha kabisa utaratibu wa kuzuia miili ya marehemu katika hospitali za umma kwa sababu ya madeni ya matibabu. Hata hivyo, mpaka sasa bado kuna malalamiko kutoka sehemu mbalimbali nchini kuhusu familia kulazimishwa kulipa madeni kabla ya kukabidhiwa mwili wa mpendwa wao. Hili ni kinyume na utu, heshima na ubinadamu lakini CCM haichukulii hii ni kero kubwa kwa wananchi wake bali ni ahadi za kiuchaguzi tu.
Mbali na uchambuzi juu ya utekelezaji wa ahadi hizo unaonesha ubabaishaji na kukosekana kwa dhamira ya kweli, tumeenda pia kuangazia hali ya huduma ya afya kwa wanufaika wachache waliounganishwa na inayoitwa bima ya afya kwa wote na Watanzania wengine.
Tumeendelea kubaini changamoto zifutazo;
Mosi, kadi hazijaambatana na dawa, vifaa tiba na vipimo vya uhakika. Wananchi wenye bima bado hulazimika kununua dawa na kulipia vipimo. Madeni ya Serikali kwa MSD yanayokadiriwa kufikia Sh471.11 bilioni yanaongeza tatizo hili. Kadi bila dawa ni sawa na kigae bila paa.
Tumeendelea kubaini changamoto zifutazo;
Mosi, kadi hazijaambatana na dawa, vifaa tiba na vipimo vya uhakika. Wananchi wenye bima bado hulazimika kununua dawa na kulipia vipimo. Madeni ya Serikali kwa MSD yanayokadiriwa kufikia Sh471.11 bilioni yanaongeza tatizo hili. Kadi bila dawa ni sawa na kigae bila paa.
Pili, uhaba wa wahudumu wa afya nchini. Kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na Serikali, mahitaji ya watumishi wa afya nchini yanafikia takribani 348,923. CCM ilitoa ahadi ya kuajiri watumishi 5000 pekee, hivyo kufanya idadi ya watumishi waliopo baada ya ongezeko hilo imefikia takribani 182,430, sawa na asilimia 52.3 ya mahitaji. Hii inaacha pengo kubwa la watumishi katika mfumo wa afya. Kwa makadirio hayo, ili kufikia mahitaji yaliyopo, Serikali ingehitaji kuajiri kwa wastani watumishi 33,298 kila mwaka ndani ya kipindi cha miaka mitano. Lakini kwa mwenendo huu wa kuajiri watu 5,000 itachukua miaka 33 kufikia mahitaji yaliyopo sasa. Ni dhahiri CCM imefeli na haina uwezo wa kumaliza tatizo la wahudumu nchini.
Changamoto hii ina maana kubwa kwa Bima ya Afya kwa Wote kwa sababu haiwezekani kuwa na bima kwa wote bila kuwa na madaktari, wauguzi, wataalamu wa maabara, wataalamu wa dawa na wahudumu wengine wa afya wa kutosha.
ACT Wazalendo tunalitazama suala la matibabu ya mtanzania kwa uzito mkubwa sana, kwasababu bila ya afya hakuna uhai na bila uhai hakuna taifa. Suala la ugharamiaji wa huduma za afya limekua chanzo kikuu cha mamilioni ya watanzania kudumbukia kwenye lindi la umasikini. Kwa miongo mitatu, Serikali ya CCM imekuwa ikiacha suala la afya kwenye mabega ya wananchi wenyewe au wafadhili kutoka nje. Bajeti ya afya ya Tanzania ni chini ya asilimia 3 ya bajeti kuu ya Serikali, kinyume na makubaliano ya Abuja yanayotaka kutengwa kwa asilimia 15 ya bajeti kuu kwa ajili ya sekta ya afya.
Hivyobasi, ili kubaliana na tatizo hili, ACT Wazalendo inasisitiza kutumia mfumo wa Hifadhi ya Jamii kwa Wote na kufungamanisha na bima ya afya, ambapo sekta rasmi na isiyo rasmi itachangia kulingana na uwezo, Serikali iwalipe 100% maskini, na kila mwanachama apate bima moja yenye usawa, isiyo na matabaka na inayogharamia magonjwa yote muhimu.
Sambamba na hilo, Serikali iondoe utegemezi wa dawa kutoka nje kwa kuwekeza kwa dharura katika uzalishaji wa dawa nchini na kuweka mikataba ya uhakika ya ununuzi wa dawa zinazozalishwa ndani ya nchi.
Bima inayotoa huduma zaidi kwa mwenye fedha na huduma chache kwa maskini si Bima ya Afya kwa Wote. ACT Wazalendo inaamini afya ni haki ya kila mwananchi, si huduma ya anayemudu kulipia.
Imetolewa na;
Dkt. Elizabeth Benedict Sanga
Waziri Kivuli wa Afya na Ustawi wa Jamii 27 Agosti, 2026