ACT Wazalendo watangaza nia ya kujitoa SUK
..Nawaunga mkono.

..Ccm haiheshimu mawazo na michango ya wapinzani.
Kikatiba Rais wa Zanzibar hapaswi kufuata ushauri wa mtu yoyote, ila atasikia ushauri, kuufuata na kuutoufuta ni juu yake hashinikizwi kisheria kabla ya kutoka wangepigana kunabadilisha hilo kwamba Rais awe anaufuata ushauri
 
Hii ndio gia mpya waliyoamua kuja nayo baada ya Chaguzi zao kumalizika

Zaidi soma hapa

--
Akizungumza na waandishi wa habari leo tarehe 8 Machi 2024 jijini Dar es Salaam Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo, Ado Shaibu amesema viongozi wa chama hicho watakutana na Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan pamoja na mwenzake wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, Dk. Hussen Mwinyi kwa ajili ya kuwaeleza nia kujitoa kwenye serikali hiyo.

Ado amesema makubaliano yaliyofanywa kati ya Hayati Maalim Seif Sharif Hamad na Rais Zanzibar, Dk. Mwinyi hayajatekelezwa.

Amesema moja ya makubaliano kati Maalim Seif na Dk. Mwinyi ni kurekebisho mifumo ya kiuchaguzi katika nchi ya Zanzibar ili kupatikane uchaguzi wa huru na haki na kuepusha machafuko yanayotokea katika kila uchaguzi visiwani humo.

Amesema Serikali ya SUK ni zao la umwagikaji damu za wananchi wa Zanzibar katika vipindi vyote vya uchaguzi.

“Tuliingia kwenye serikali ya umoja wa Kitaifa kwa sababu mbili ya kwanza hilo ni takwa la kisheria pili kwa sababu ya makubaliano ya Maalim Seif na Dk. Mwinyi,” amesema.

Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar Zanzibar, inaundwa na CCM pamoja na ACT Wazalendo kupitia Mwenyekiti wa chama hicho, Othman Masoud ambaye ni Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar.

Chanzo: Mwanahalisi
Wana huo UBAVU
 
Tukubali afrika hakuna upinzani bali kuna wapigania fulsa ACT wanataka kujitoa kwenye serekali ya umoja wa kitaifa kabla ya mwaka mmoja wa uchaguzi hiki ni kichekesho na kutafuta kick

Kwanini wasijitoe mwaka 2021, 2022 au 2023 wasifanye watu wajinga Tanzania hatuna upinzani na hii imeonyesha usanii wa zitto kabwe
 
Back
Top Bottom