ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

HAWA KAMA WAMEKUBALI KUSHIRIKI KUUNDA SEREKALI THATS MEANS WAMESHA WAMEHALALISHA UCHAGUZI NA NI KIBALI KIBALI CHA WAZI SASA KWA COVID 19 KUINGIA KAZINI
 
HAWA KAMA WAMEKUBALI KUSHIRIKI KUUNDA SEREKALI THATS MEANS WAMESHA WAMEHALALISHA UCHAGUZI NA NI KIBALI KIBALI CHA WAZI SASA KWA COVID 19 KUINGIA KAZINI

Aidan si anaendelea na ubunge wake, mshahara wake utagombania mpaka kieleweke
 
Vile wanachama wa ACT wakiisikiliza kamati kuu ya chama
9087654654.jpg
 
1. Kujiunga SUK ni kuhalalisha Uchaguzi haramu?

Hapana. ACT Wazalendo kimechukua na kinaendelea kuchukua hatua mbalimbali za ndani na nje ya nchi kuupinga uchaguzi huu na matokeo yake. Chama kitaendelea kufanya hivyo, ikiwemo kupigania Katiba Mpya na Tume Huru ya Uchaguzi ili kuhakikisha uchaguzi nchini unakuwa huru na wa haki.

2. SUK ni hisani ya CCM?

Hapana. SUK ipo kikatiba. Hatupewi na CCM. Tumepewa na Katiba ya Zanzibar. Majimbo tuliyotangazwa kushinda (Pemba) tulishinda kweli. Hata hivyo, Kuporwa kingi hakuhalalishi kususia kidogo kilichopatikana. Ni muhimu ikumbukwe pia kuwa SUK ni zao letu. Mwenyekiti wa ACT Wazalendo Ndugu Maalim Seif Sharif kwa kushirikiana na Rais Mstaafu wa Zanzibar Ndugu Amani Abeid Karume ndio waliokuwa waasisi wa SUK kwa ajili ya kuleta muafaka na maelewano miongoni mwa Wazanzibari.

3. Kujiunga SUK ni kuwasaliti wenzetu waliokamatwa, kuteswa, kuachwa vilema na kuumizwa na wale waliouawa kutokana na uchaguzi?

Hapana. Vitendo vilivyofanywa na Vikosi vya Zanzibar, Vikosi vya JMT (Polisi, Jeshi, Usalama wa Taifa) vya kuuwa, kutesa na kujeruhi watu tena baadhi yao wakiwa mikononi mwa vyombo husika ni vitendo vya kijinai. Jinai haifi. Tutaendelea kutetea haki yao ndani na nje ya nchi hadi haki ipatikane na waliotenda unyama wawajibishwe.

4. Kujiunga SUK kutafifisha kesi yetu ICC?

Hapana. Chama hakitaachana na kesi yake ICC. Kesi itaendelea hadi waliofanya unyama kwenye Uchaguzi Mkuu wawajibishwe.

5. Kujiunga SUK kutafifisha madai yetu kimataifa (Jumuiya ya Madola, AU, Jumuiya ya Ulaya n.k) kuhusu uchaguzi kuhujumiwa?

Hapana. Chama hakitaondoa malalamiko yake kwenye vyombo vya kimataifa kuhusu hujuma kwenye Uchaguzi Mkuu. Tutaendelea kupaza sauti ndani na nje ya nchi kupigania Tume Huru ya Uchaguzi na Katiba Mpya ili Uchaguzi uwe huru, haki na wa kuaminika.

6. Viti vilivyotangazwa ni vichache, hakuna mabadiliko yoyote tutakayoleta SUK?

Ni kweli tumedhulumiwa sana. Uchaguzi ungekuwa huru na wa haki, tungepata wawakilishi wengi zaidi. Lakini hilo halitunyimi kuwaruhusu wachache waliotangazwa kwenda kwenye vyombo vya Uwakilishi. Wakati mwingine, wingi si hoja. Kwenye Bunge lililopita tulikuwa na Mbunge mmoja tu, Zitto Kabwe. Lakini, alikuwa na mchango wa kipekee Bungeni. Chama kitahakikisha kuwa kinawasimamia Wawakilishi wake kwenye vyombo vyote wasimame kidete kutetea maslahi ya umma.

7. Kujiunga SUK ni kukosa msimamo kama wa wenzetu CHADEMA?

Hapana. Kila Chama kinapaswa kufanya maamuzi yake kwa kuzingatia maslahi ya Chama na maslahi ya Taifa. Maamuzi haya yamefanywa na vikao halali vya Chama kwa kuzingatia maslahi ya ACT Wazalendo na Taifa kwa ujumla.

8. Kujiunga SUK ni kuwasaliti Wazanzibar?

Hapana. Chama chetu kimezungumza na wanachama na viongozi wetu kwenye Mikoa yote ya Zanzibar. Wengi wanaunga mkono Chama kujiunga SUK.

9. Kujiunga SUK ni kujali maslahi binafsi (Ruzuku, vyeo n.k?)

Hapana. Chama hiki kimesheheni viongozi wengi ambao wana rekodi zisizoyumba za kutanguliza maslahi ya Taifa badala ya maslahi yao binafsi. Hata uamuzi wa sasa wa kujiunga SUK unazingatia maslahi ya Chama badala ya maslahi binafsi ya mtu.

10. Kujiunga SUK ni kurejesha nyuma madai ya Msingi ya harakati ya mageuzi?

Hapana. Mapambano ya kupigania mageuzi nchini hayatakoma hadi mabadiliko ya msingi yanayopiganiwa kwenye nyanja za kiuchumi, kisiasa na kijamii yapatikane.
 
Huu sasa ndio uamuzi wa busara, sio kususa tuu bila mpango.

Asiyekubali kushindwa sio mshindani, if you can't get what you want, just take what you get!, and if you can't beat them, join them!.

Hatimaye ACT Wazalendo sasa wamekubali matokeo, sio tuu watapokea kidogo walichopata, bali pia wata wa join them kwenye kuunda SUK.

Hongera sana ACT, hizi ndio siasa za kweli.
P
 
Kila la kheri kwa ACT, sote ni wajenzi wa nyumba moja haina haja ya kunyanganyana fito, bado CHADEMA kule wanapambana na wanawake wao

Wakikosea wakabariki huo uhuni wa hao wanawake kushiriki kwenye hilo bunge kibogoyo, wasahau sisi washabiki wao tuliowengi kujitokeza kupiga kura tena. Hatuko tayari kubariki chaguzi za kishenzi.
 
Mkuu kwako wewe vurugu na mauaji ni furaha, unadhani hoja ya ICC ni tishio kwa utawala huu ulio imara kuliko hapo swali?

Vurugu na mauaji zaidi ya yaliyotokea kwenye uchaguzi huu? ACT kwa sasa imejigeuza kuwa chama rasmi cha ulaji.
 
ACT Zanzibar wametepeta.
Makumi ya waliouawa Zanzibar
Wizi wa jutisha wa kura huko Zanzibar
Mashitaka ICC hayana tena nguvu
ACT imewatupa wananchi wa Zanzibar chini ya basi
ACT wamekosa msimamo thabiti wameenda kukaa na madhalimu katika meza ya ulaji.

Hakuna chama tena hapo ni chama maslahi.

Zitto Pole sana, hamna credibility tena ya kuzungumzia uchaguzi huru na haki kwa sababu mko radhi kula matunda ya uchaguzi usiyo wa haki.

Kiufupi ACT haina ajenda kuelekea 2025
Nawaomba Chadema wasigeuke jiwe, wakaze tutawaheshimu zaidi, na Chadema itaimarika zaidi.

Ni kuhadaa umma kudai eti ACT imesikiiza maoni ya wanachama wake, kiufupi ni kuwa akina maalim walikuwa wanataka kusikia wanachotaka kuambiwa maana wangekuwa na msimamo wasingeuliza kama nao wakale kilicho haramu au la!

Leo ACT kwangu mimi imekuwa CCM B

You are absolutely right. Hii tabia ya kuingiza watu kwenye chaguzi kisha kupigwa kuachwa na vilema, vifo na uharamia mwingine wote kama huo, halafu viongozi kuja na maelezo ya kitapeli, kwa sasa ifike mwisho. Ni vyema wananchi kuacha kujitokeza kupiga kura kwa faida ya viongozi wachache wasaka mlo. Kwa sasa ni kuhakikisha wananchi hawajitokezi tena kupiga kura mpaka mfumo mzima wa uchaguzi ubadilike.
 
Kwahali hii Wazanzibari wanapitia wakati mgumu sana
 
Maamuzi ya chama yaheshimiwe na kila mtu kwa kuwa ni ya kikatiba. Hata maamuzi ya Chadema kutokushiriki bunge la JMT ni sahihi pia. Ndugai na wenzake wasishurutishe.
 
Huu sasa ndio uamuzi wa busara, sio kususa tuu bila mpango.
Asiyekubali kushindwa sio mshindani, if you can't get what you want, just take what you get!, and if you can't beat them, join them!.
Hatimaye ACT Wazalendo sasa wamekubali matokeo, sio tuu watapokea kidogo walichopata, bali pia wata wa join them kwenye kuunda SUK.
Hongera sana ACT, hizi ndio siasa za kweli.
P
!!!!!
 
Back
Top Bottom