ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

ACT-Wazalendo yaridhia kushiriki kwenye Serikali ya Umoja wa Kitaifa Zanzibar na Vyombo vya Uwakilishi

Hujui kinachoendelea ndani ya Chadema!
Wala sitaki kujua, ila wakosee tu watambue uwepo wa hao wahuni bungeni. Itakapofika wakati wa uchaguzi wawaombe wanaccm wajitokeze kuwaunga mkono, lakini kura zetu wazisahau rasmi. Sasa hivi wenye maamuzi ni sisi wapiga kura, na sio wao. Na uwezo wa kushawishi watu wasipige kura tunao.
 
Kimsingi pamoja na kejeli zitakazoelekezwa na watu juu ya uamuzi huu kwa chama cha ACT Wazalendo mimi naona wametumia busara iliyopitiliza. Kwa mujibu wa Ado walitakiwa wachague jambo moja kati ya mawili, kuamua maamuzi mabaya au kuamua maamuzi mabaya zaidi.

Ninaamini mzee maalim anaijua zanzibar na anajua zanzibar inahitaji nini, ni maamuzi ya kikomavu sana.
 
Asishirikiane na wamwaga damu na wezi wa kura.
Asishirikiane nao kuwasaidia watanzania kurejesha umoja wa kitaifa, kukuza sekta binafsi na uwekezaji kwa ajili ya watanzania aliotaka kuwaongoza? Kwani ana hasira na Watz!?
 
Kufuatia uamuzi was chama Cha Act Wazalendo kukubali kushiriki serikali ya mapinduzi Zanzibar huku wakijua kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki , huku wakijua kuna watu wameuawawa , kupigwa , kuteswa , kufungwa , bambikiwa kesi , chomewa nyumba bila kujali madhira waliyoyapata wafuasi na wanachama wao leo hii Zitto Kabwe.

Maalim Seif Sharifu Hamad na Act Wazalendo bila aibu aiseee wanaenda kushirikiana na watesi wao ili kusaidia waonekane ushindi wao ni halali , ili wapate msaada wa wafadhili , ili kuwaepusha na mashtaka ya ICC licha ya kufanya makosa hayo mchana kweupe . Nashauri kuanzia leo Zitto Kabwe , Maalim Seif Sharifu Hamad na Act Wazalendo wasiaminiwe tena na wananchi .

Wanapigania mageuzi , watu wanapoteza roho zao kwa ajili yao halafu wao wanaenda kuungana na waliopoteza roho za wafuasi na wanachama wao .
 
jamaa anajikutaga mzee wa busara, anapanga mipango kuliko chama chenyewe saaahv kabaki solemba
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]Kuna wakati alikuwa ana mshabikia Membe, sijui alifikiri urais ni sawa na umonitor?
 
Kufuatia uamuzi was chama Cha Act Wazalendo kukubali kushiriki serikali ya mapinduzi Zanzibar huku wakijua kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki , huku wakijua kuna watu wameuawawa , kupigwa , kuteswa, kufungwa...
Zito alisha saliti CHADEMA enzi hizo, kutaka uenyekiti wa Mbowe, si mtu wa kumwamini. Kwa hili mimi sioni ajabu maana Zito ana historia ya usaliti!
 
Wala sitaki kujua, ila wakosee tu watambue uwepo wa hao wahuni bungeni. Itakapofika wakati wa uchaguzi wawaombe wanaccm wajitokeze kuwaunga mkono, lakini kura zetu wasisahau rasmi. Sasa hivi wenye maamuzi ni sisi wapiga kura, na sio wao. Na uwezo wa kushawishi watu wasipige kura tunao.
Ahaaa.. Mkuu acha vituko!

Mbona Mbowe kafanya maamuzi ya kijinga mara nyingi tu na yamekigharimu chama lakini sijawahi kuina reaction yeyote kutoka kwako?
 
ADO SHAIBU: Kamati kuu ilikutana jana jijini Dar es Saalam Tarehe 5 Disemba katika hoteli ya Onomo ambayo iko Posta kwa ajili ya kutafakari hali ya kisiasa inayoendelewa nchini kwetu...
Haya sasa. Tuone na lile povu la covid19 lipi Zito
 
Viongozi wenyewe ACT ni Nondo na Shaibu? nchi hii ina vituko!
 
  • Thanks
Reactions: PNC
Mkuu fikiria mara mbili mbili ,Zitto kwasasa sio mbunge ,kwahiyo karata yake ya mwisho ni Ruzuku za chama,sasa akikataa hapo lazima maisha yawe magumu!! Tatizo NJAA mkuu harakati ngumu kama una njaa.
 
Back
Top Bottom