ACT Wazelendo yawataka IGP na Waziri wa Mambo ya Ndani kujiuzulu kutokana na vitendo vya Utekaji na mauji ya raia wasio na hatia

Dalton elijah

JF-Expert Member
Joined
Jul 19, 2022
Posts
373
Reaction score
829
"Matukio ya kuuawa, kupotea na kutekwa kwa wananchi, mwaka 2024 umeshuhudia ongezeko la vitendo vya utekwaji, kupotezwa, na hata mauaji ya wananchi wasio na hatia, visa na takwimu ya matukio zaidi ya 150 ya aina hii yamerekodiwa huku wengi wa wahanga (waathirika) wakiwa ni wanaharakati na wananchi waliokuwa wakidai haki zao, vitendo hivyo vya utekaji, kupotea na mauaji ya raia nchini havina majibu hadi leo" -Mchinjita

"Licha ya matukio yote haya ya wazi kabisa, Jeshi la Polisi halijatoa taarifa yoyote ya kina kuhusu matukio haya, licha ya Rais kutoa maelekezo ya kuchunguzwa, kimya hiki kinatupa jibu moja kati haya huenda Jeshi la Polisi linamdharau Rais Samia au Rais ameuhadaa umma" - Mchinjita

"ACT Wazalendo mara kwa mara tumekua tukitoa wito wa uchunguzi wa kina na taarifa ziwekwe hadharani, pia tumetaka Mkuu wa Jeshi la Polisi (IGP) na Waziri wa Mambo ya Ndani ambao ndio wanawajibu wa kulinda usalama wa raia na mali zao wajiuzulu au waondolewe katika nafasi zao lakini serikali 'imetia pamba' masikioni kiasi cha kuacha mashaka kwa umma kuwa wanahusika na kulinda katika matukio haya" - Isihaka Mchinjita, Makamu Mwenyekiti wa ACT Wazalendo.

Pia soma
- Waziri Masauni na IGP Wambura, mnasubiri nini kujiuzulu?
 
Mchinjita, wimbo wa kutaka , kutaka ,kutaka, kutaka serikali, Jeshi la polisi nawengine wajiuzulu wimbo huu umaimbwa for decades......hakuna matokeo bado eti chama cha siasa cha upinzani kinaimba wimbo huo wa kutaka!

Yale yale ya huyu mropokaji mnadhani atafanya nini...eti mropokaji ndiye atatuvusha... atafanya nini? au naye ataimba wimbo na kupata mapambio kama Mrema Lyatonga!
 
Back
Top Bottom