Tatizo ni huyo mama na mtazamo wake juu ya maisha.
Hivi unadhani huyo mama baada ya kuona maisha yake ni magumu na hawezi kumuudumia huyo mtoto, angeamua kujiua na kumuacha huyo mtoto, baada ya watu kujua amejiua na kuacha mtoto nini kingetokea kwa mtoto?
Je na yeye angeuliwa eti kwa sababu mama yake kajiua?
Au angeuliwa eti kwa sababu baba yake kamtelekeza?
Na wangapi wanaishi bila ya wazazi?
Tatizo huyo mama alijiona yeye ndiye uhai wa huyo mtoto, na hajui ya kuwa Mungu ndiye anayetoa riziki na sisi wanaadamu ni asbabu tu.