Adam Kimbisa anaweza na anatosha kuwa Makamu Mwenyekiti CCM bara kumsaidia Mwenyekiti CCM taifa

Adam Kimbisa anaweza na anatosha kuwa Makamu Mwenyekiti CCM bara kumsaidia Mwenyekiti CCM taifa

Tlaatlaah

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2023
Posts
24,665
Reaction score
25,388
Kwa maoni yangu, muungwana anastahili umakamu mwenyekiti wa CCM Taifa kuirithi mikoba ya Kinana, alieng'atuka kwa hiyari yake hivi karibuni. Hata hivyo hilo sio muhimu sana, but Kimbisa anafanya kazi nzuri mno, katika kukiongoza chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma.

Ndugu ADAM KIMBISA,
Aliwahi kua Meya wa jiji la Dar es salaam na mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa.

Lakini pia amewahi kuhudumu kama mbunge wa Bunge la Africa Mashariki, akiwakilisha Tanzania.

Zaidi sana Alhaj ADAM KIMBISA amewahi kua katibu mkuu wa Red Cross Tanzania..

Si hivyo tu ADAM KIMBISA, amehudumu kwa kipindi kirefu, kama afisa muandamizi Wizara ya Mambo ya nje Tanzania.

Kwa kifupi ni mzoefu katika utumishi na uongozi wa chama na serikali Taifa. Ni mtu mzima mweye weledi, hekima na busara katika majukumu yake. Ni muadilifu na mchapakazi hodari mwenye mafanikio makubwa na ufanisi usio na shaka, katika kila kila jukumu au wajibu alopewa kuusimamia, kuutumikia au kuongoza.

Soma Pia: Abdulrahman Kinana, Makamu Mwenyekiti (CCM) Ajiuzulu, Rais Samia Suluhu Aridhia

Kidumu Chama Cha Mapinduzi 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
 
Yaan vyeo vyote hivyo amepitia na bado yupo madarakani, hapana kwa kweli inabidi asitaafishwe kwa lazma

wale wote waliozaliwa 1970-79 wanapaswa wakae pembeni wakati wao umeisha
 
Kwa maoni yangu, muungwana anastahili umakamu mwenyekiti wa CCM Taifa kuirithi mikoba ya Kinana, alieng'atuka kwa hiyari yake hivi karibuni. Hata hivyo Kimbisa anafanya kazi nzuri mno, katika kukiongoza chama cha mapinduzi mkoa wa Dodoma.

Ndugu ADAM KIMBISA,
Aliwahi kua Meya wa jiji la Dar es salaam na mjumbe wa kamati kuu CCM Taifa.

Lakini pia amewahi kuhudumu kama mbunge wa Bunge la Africa Mashariki, akiwakilisha Tanzania.

Zaidi sana Alhaj ADAM KIMBISA amewahi kua katibu mkuu wa Red Cross Tanzania..

Si hivyo tu ADAM KIMBISA, amehudumu kwa kipindi kirefu, kama afisa muandamizi Wizara ya Mambo ya nje Tanzania.

Kwa kifupi ni mzoefu katika utumishi na uongozi wa chama na serikali Taifa. Ni mtu mzima mweye weledi, hekima na busara katika majukumu yake. Ni muadilifu na mchapakazi hodari mwenye mafanikio makubwa na ufanisi usio na shaka, katika kila kila jukumu au wajibu alopewa kuusimamia, kuutumikia au kuongoza.

Kidumu Chama Cha Mapinduzi 🐒

Mungu Ibariki Tanzania
Sidhani kwani hamuna karma kulingana na wasemaji wa karma?
 
Huyu Kimbisa msaliti wa maamuzi ya mwenyekiti wa ccm taifa (Kikwete) mwaka 2015?

Kimbisa aliitisha press huku akiwa amezungukwa na akina Nchimbi, Sophia Simba, John Mgeja, nk na kutoa karipio kali kwa Kikwete baada ya kumkata Lowasa.
 
Back
Top Bottom