Adam Mchomvu aomba radhi, asema alikwazika

Jambo la kheri kama amefanya hivyo. Amuombe radhi pia E. Mbasha na Watanzania kwa ujumla.
 
Yule kijana nasikia kuna kampuni zinamtumia kama brand ambassador, hivi wana akili?

Kuna kampuni inajielewa inamtumia yule mvuta bangi kama muwakilishi wao?

Yule amedhihirisha wazi kua bangi sio kitu kizuri, acha iendelee kupigwa marufuku tu.

Kijana muda wote anapandisha suruali kama mtu anaejinyea.

Kama hawa ndio brand ambassadors basi bado tuna safari ndefu.
 
Nakereka sana bangi inapotajwa tajwa hovyo, mnatukosea heshima wavutaji, mnasema bangi mbaya kwani mshawahi kuvuta kenge nyie???

Mchomvu alikuwa anatekeleza maagizo ya Nape Nauye, uzinduzi wa mitama na mabuti
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Jamaa amenikera Sana, haiwezekani Chama kiandae tukio kubwa namna ile halafu yeye aliharibu. Yaani story Sasa kawa yeye badala ya Chama. Mh. Polepole, huyo jamaa inabidi Jana ndio iwe mwisho kushiriki shughuli za chama.
 
Nakereka sana bangi inapotajwa tajwa hovyo, mnatukosea heshima wavutaji, mnasema bangi mbaya kwani mshawahi kuvuta kenge nyie???

Mchomvu alikuwa anatekeleza maagizo ya Nape Nauye, uzinduzi wa mitama na mabuti
Mzee wa goli la mkono!
 
Nimeangalia lile tukio ndio nimethibitisha kweli huyo Mchomvu ni mvuta bangi, ana ujuaji wa kishamba, hakuwa na sababu ya kumpiga Mbasha mtama wakati Mbasha tayari alikuwa anaondoka eneo la tukio, alichokifanya huyo Mchomvu ni utoto wa kutafuta sifa za kijinga.
 
Mchomvu yuko sahihi vijana wa Lumumba kama wale dawa yao mitama tu
Nami nakuunga mkono. Huyo Mbasha, badala ya kupanda jukwaani na kuimba nyimbo za kumtukuza Muumba wetu, yeye akabaki kumtukuza na kumuimba JPM ...... " MAGUFULI HOYEEE! HAKUNA KAMA MAGUFULI! UKAWA MTULIE TUU! "
Mwana kulitafuta kulipata!
 
CCM ina wahuni wa kila aina
 
Yes, kila akipiga hatua moja lazima apandishe suruali, miaka yote hiyo hakui, bado ana usela mavi mwingi sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…