Adam Mchomvu aomba radhi, asema alikwazika

Adam Mchomvu aomba radhi, asema alikwazika

Hahaha!!! Kama sio fani yako kwakweli utaumbuka/

Utampunguzia nani midhambi isiyo hesabiki ushakaba,Ushaiba na Ushauwa/

Hiyo Mibangee wanayovuta ni stimu za kulanduka
Njisi kijana anavyobadili tabia/
Inavyoonekana amesahau Mila za Mtanzania/

What'sup Sir Nature...
 
Mtangazaji wa Clouds media Adam Mchomvu amemshukuru Rais Magufuli na CCM kwa kumuamini na kumpa jukumu la kuongoza shughuli katika tamasha la wasanii.

Kadhalika Mchomvu amemuomba radhi Rais Magufuli na CCM kwa sintofahamu iliyotokea pale jukwaani kati yake na bwana ndugu msanii mwenzie Emmanuel Mbasha lililosababishwa na hasira.

Source Ayo tv.

Maendeleo hayana vyama!
Kuna mtu alitoa mfano wa mtu kuoga ziwani kichaa akaja akachukua nguo zake...bwana akasema Kama aliyekuwa anaoga akatoka kwenye ziwa akamkimbiza kichaa basi...wote watawaita ni vichaa wanakimbiza...somo: kuvumiliana na kuheshimiana Ni Jambo la msingi Sana..hasa kwenye kadamnasi...na kwa watu wanaojiita au wanaonekana Kama kioo Cha jamii..
 
“Dear #WashkajiZangu, kwanza nimuombe radhi Rais wetu wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Pili kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuniamini na kunipa nafasi ambayo bahati mbaya ilitokea tukapishana kauli jukwaani na Bwana ndugu Msanii mwenzangu, nimepokea simu mbalimbali za Viongozi wa Serikali wakinifahamisha namna nilipaswa kufanya wakati wa shambulio lile la mimi kuitwa 'ADAM Unajua we ni Bangi sana' Kwa pamoja nimewaelewa”

“Nikutake radhi pia Emmanuel Mbasha, mimi sina tatizo lolote binafsi na wewe, kilichotokea ni kukwazika na kauli yako uliyotoa dhidi yangu kwenye tukio kubwa la Kitaifa lililotazamwa na Mamilion ya Watanzania, sisi wote Vijana kuna muda tunakosea na tunawekana sawa japo njia zingine si nzuri. Asante kwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kwa maelekezo yenu. Nitayatii na kwa sasa mimi ni Balozi wenu wa hiari kabisa.
Aache matumizi ya bangi sana.
 
Bangi hata mkulu akiwa mbeya alisema tuchome kisirisiri na tuwe wakali tena akasisitiza ya kyela.Big up Adam kwa kuwa mkali.
 
“Dear #WashkajiZangu, kwanza nimuombe radhi Rais wetu wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli, Pili kwa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kuniamini na kunipa nafasi ambayo bahati mbaya ilitokea tukapishana kauli jukwaani na Bwana ndugu Msanii mwenzangu, nimepokea simu mbalimbali za Viongozi wa Serikali wakinifahamisha namna nilipaswa kufanya wakati wa shambulio lile la mimi kuitwa 'ADAM Unajua we ni Bangi sana' Kwa pamoja nimewaelewa”

“Nikutake radhi pia Emmanuel Mbasha, mimi sina tatizo lolote binafsi na wewe, kilichotokea ni kukwazika na kauli yako uliyotoa dhidi yangu kwenye tukio kubwa la Kitaifa lililotazamwa na Mamilion ya Watanzania, sisi wote Vijana kuna muda tunakosea na tunawekana sawa japo njia zingine si nzuri. Asante kwa Jeshi la Polisi chini ya IGP Simon Sirro kwa maelekezo yenu. Nitayatii na kwa sasa mimi ni Balozi wenu wa hiari kabisa.
Tumekusameee kwakuwa umekiri makosa binadamu tunakosea. Endelea,piga kazi mdogo wetu ; kama mkuu wa kaya anavyosema.
 
Msamaha anao yeye mwenyewe kwa kuacha kutumia Bangee. Watu kama hawa ndio wanasababisha serikali ipige marufuku utumiaji bangee...vipi kama Mbasha nae angekuwa anavuta unadhani nini kingetokea jana pale jukwaani....
Kumbe havuti
 
Ili mradi tushaona mtamaa wao mengine watajuaa wenyeweee[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787]
 
Hata mimi nashangaa kweli. Nimeitizama video katika angle tofauti tofauti ila sijaona kama ule ulikua mtama wa kutisha kama watu wanavyodai.
Kwa mtoto mrembo kama Mbasha ni mtamaa kwelii alafu remind you alikuwa anatembea so lazima angedondoka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Adam anaomba msamaha bhasi tuuu ila bado kammind jamaa sanaa
 
Kwa mtoto mrembo kama Mbasha ni mtamaa kwelii alafu remind you alikuwa anatembea so lazima angedondoka[emoji1787][emoji1787][emoji1787]

Adam anaomba msamaha bhasi tuuu ila bado kammind jamaa sanaa
Huyu Adam hajafunzwa vizuri ndio tunamfunza kimtandao
Ajue Sisi walipe kodi sio kumaindi tu tumepoteza pesa nyingi kuangalia mibangeee yake
Pia, clouds ni kampuni kubwa haistaili kuendelea kuwa na watu wa kaliba ya huyo jamaa
Tutashindwa kuwapelekea kazi tutaogopa mingwala na mamimitama kama yale
Aiseh watu wanapiga mitama hatari mbele ya kamera
 
Back
Top Bottom