Mimi nna uhakika kuwa wale watangazaji wasio na maadili ya kazi ni kweli waligombana studio. Nadhani namna bora ingekuwa ni kuomba radhi wasikiliziaji tungewaona wana busara. Kitendo cha kusema lilikuwa zengwe ni kuficha ukweli na kuthibitisha kuwa tumeanza kukolea sumu inayosambazwa na watatawala wetu ya kufichiana maovu. Kwa uelewa wangu mimi kwa tukio kama lile ingefaa wahusika wachukuliwe hatua na uongozi wa chombo hicho na pia shirikisho la wanahabari. Kuwatetea ni Si vema kuwa na chombo cha habari chenye kuashiria upotovu wa maadili. Haya ni tuliyoyasikia. Je kama kuna mengine huwa hatuyasikii?