Adam na Hawa walikuwa wawili hapo kale?

Adam na Hawa walikuwa wawili hapo kale?

Samahani Scatter, Tuanzie hapa kwanza " Yai au kifaranga " kipi cha kwanza?
Halafu usisahau kuna kitu chaitwa Baraka (Blessings).....!

mkuu ipo wazi yai? Ama unataka kusemaje
 
mimi hapa "sidhani"

unarudia swali lako lile lile, nilikuambia kuwa usome kitabu cha Mwanzo 1:1-31, wewe umekataa na kukimbilia kujibu hoja bila majibu, tunakuomba utupe reference hautaki, sijui na siye tudhani bila reference!

nishakupa ndugu ! Kitabu cha mwanzo mistari yake yote ndio my reference ukitaka na quruan nitakupa pia
 
Da kaaaaaz kwelikweli kama msingi wako ndio huu manake hata nikichukua hii shule sijui nitamwelezea nani anielewe. Adamu aliishi duniani physically na alikula tunda physically na alitolewa nje ya bustani physically na ardhi ililaaniwa physically; tumepokea kifo na laana toka kwake. Sasa jamaa yangu unaposema waliokula tunda ni watu kibaaaao na walioleta kifo ni watu kibaaaao na waliotolewa ubavu kuumba mwanamke ni watu kibaaaao mbona inakuwa shida sana rafiki yangu? mwanamke ana mbavu 18 na mwanaume mbavu 17 mmoja ukiwa umetolewa kumuumba Hawa sasa unaposema waliumbwa kibao tangu mwanzo ni yupi sasa mmoja wao ubavu ulitolewa na hao kibao mbavu yao mojamoja iliyeyuka saa ngapi na kwenda kufanya nini? maandiko yanasema Adam alikuwa peke yake kwa maelfu ya miaka kabla ya kuumbwa mwanamke wewe unakuja na elimu mpya isiyo hata na mizizi mbona hili ni balaa kubwa!

kabla sijakujibu hoja yako ...mkuu
adam akiwa kama roho alikula tunda gani?
Unajua maana ya tunda enzi za bustan ya edni?
Nadhan tutaelewana tu
 
kuna kitu hapa kinanitatiza.Tunaamini kuwa Mungu hakosei na anajua kabla halijatojea. sasa inawezekanaje Mungu aruhusu kitu halafu baadae akikataze. inamaana tunakiri kakosea? mnaposema zamani ilikuwa ruksa kumlala dada yako halafu then kipindi cha mussa. Mungu huyo akataze? kulitokea nini mpk akataze? so mimi nitarudi tu kwa wanaoamini kuwa duniani kulikuwa na wengi sema adamu alikuwa chaguo lake katii yao km ambavyo alichagua manabii kati yetu. kwasababu Mungu sio bunge la tanzania linalopitisha rushwa"takrima"halafu baadae linakiri lilikosea eti ilikuwa rushwa. MUNGU H AKOSEI.

hii mbona inaeleweka kabisa mkuu...kulikuwa na adam na hawa wawili tu...sasa unadhani dunia ingejaa vipi kama watoto wa kike wa adam wasingezaa na watoto wa kiume wa adam ili waijaze dunia kaama mungu alivyoagiza?
 
mkuu ukisoma vitabu vyote mfano bible mwanzo 2:6 mpaka 2:9 unaelezea philosophy viumbe kuumbwa na ukienda pale mlango wa pili 2:5 unazungumzia mtu wa kwanza kupewa roho ya kumuamini mungu kumbuka tayari keishaumba viumbe ke na me katika nchi
Naona mkuu unataka quotes kutoka kwenye bible kuhusu Adam kua wa kwanza, ndio maana hua nasema ni bora kutoa vifungu sehemu mbalimbali kuliko kujudge kifungu kimoja afu kikakuchanganya, bible inajikamilisha kama utasoma sehemu nyingi na zote zinaendana sio kusoma moja... Sasa hiyo mwanzo unayosema wewe 2:6-9 mkuu haina kitu unachoesma kabisa na haina hiyo philosophy ya viumbe kuumbwa, inaongelea formation of man peke yake,

" Lakini ukungu+ ulikuwa ukipanda kutoka katika dunia na kuunywesha maji uso wote wa nchi.+7 Na Yehova Mungu akamfanya mtu kutoka katika mavumbi+ya nchi+ na kupuliza katika mianzi ya pua yake pumzi ya uhai,+naye mtu akawa nafsi hai.+ 8 Na Yehova Mungu akapanda bustani katika Edeni,+ kuelekea mashariki, na hapo akamweka mtu ambaye alikuwa amemfanya.+ 9 Hivyo Yehova Mungu akachipusha katika nchi kila mti wenye kutamanika kwa macho ya mtu na ulio mwema kwa ajili ya chakula na pia mti wa uzima+ katikati ya bustani na mti wa ujuzi wa mema na mabaya.+"

Naomba usome upya uniambie walipoandika neno watu, pote wameweka mtu, na bado akamuweka katika bustani ya edeni, hajasema akawaweka katika bustani ya edeni watu....

Soma na sehemu nyingine sasa
1 Wakorintho 15
45 Hata imeandikwa hivi: “Mtu wa kwanza Adamu akawa nafsi hai.”+ Adamu wa mwisho akawa roho+ inayotoa uhai.+

1 Timotheo 2
14
Pia, Adamu hakudanganywa,+ bali yule mwanamke alidanganywa+ kabisa naye akaingia katika kosa..
Sasa mkuu aliyefanya kosa la kula tunda la mti wa katikati ni Hawa, sasa unataka uniambie walikua hawa kumi na wote wakala huo mti au??

Kwa hiyo, kama ni ubishi wako labda useme sio kibiblia ila kama ni kibiblia basi biblia nzima inasema mwanzo ni Adamu alafu Hawa, hakuna fungu linalopinga hilo swala kwenye biblia nzima...

natumia kimoja kwa sasa:
rejea bible mlango wa kwanza;
2;5 mungu akaijaza nchi viumbe hai kwa jinsi yake, wanyama wa mwituni na watambao
swali kwako
unajua maana viumbe hai??
Hapo hapo mwanzo
mlango wapili ukisoma tena utakutana mungu anasema akampulizia roho adam ili akaitawale dunia na vilivyomo ukisoma zaidi utaambiwa alipeleka kuishi bustani ya eden
swali
unajua maana ya kupuliziwa roho?

Viumbe hai vilikuepo tangu kale ila roho ya kumjua mungu haikuepo hapo kabla ilikuja baada ya kumteua adam aitangaze
so kulikuwa na watu wengi toka kale na ADAM SIO MTU WA KWANZA DUNIANI ILA NI MIONGONI MWA MAUDONGO YALIYOPEWA ROHO YA KUMJUA MUNGU

sijui ulikuwa umuelewi mwalimu wako au mwalimu wako ndio alikuwa haeleweki...nani kakufundisha kuwa viumbe hai ni binadamu peke yake?
 
sijui ulikuwa umuelewi mwalimu wako au mwalimu wako ndio alikuwa haeleweki...nani kakufundisha kuwa viumbe hai ni binadamu peke yake?

usinilishe maneno VIUMBE HAI VYOTE AKIWEMO BINADAMU
 
Bado haujaleta reference yoyote mkuu, ila siyo vibaya ukileta na Quran, ila tukiacha ubishi ni kuwa hapo Mwanzo, "in the beginning" hakukuwa na mtu aliyeumbwa wala kitu chochote Mwanzo 1:1-2 "Hapo mwanzo Mungu aliziumba mbingu na nchi,2"nayo nchi ilikuwa ukiwa,tena tupu,na giza lilikuwa katika vilindi vya maji......",hivyo nathibitisha kupitia Biblia kuwa Mtu "binadamu" aliimbwa baada ya vitu vyote kukamilika, na aliumbwa kwa udongo (Adamu) na kupuliziwa pumzi "Mwanzo 2:4-7"
nishakupa ndugu ! Kitabu cha mwanzo mistari yake yote ndio my reference ukitaka na quruan nitakupa pia
 
Mwanzo 3:20
Adamu akamwita mkewe jina lake Hawa; kwa kuwa yeye ndiye aliye mama yao wote walio hai.

Hao watu wengine unaowasema wewe kwamba walikuwepo, mama yao alikua nani kama tunaambiwa Hawa ndio mama wa wote walio hai?

Angalia vizuri hiyo sentensi, "MAMA YAO WOTE WALIO HAI", obviously alikuwa kulikuwa na walio hai tayari (adam na hawa walikuwa hawajazaa bado).
 
kimsingi Adamu wala Hawa si mtu wa kwanza ktk hii dunia,adamu aliishi miaka elfu sita na ushee iliyopita,ilihali dunia ilikuwepo zaidi ya miaka elfu mia moja iliyopita.dhana ya adamu kuwa mtu wa kwanza ni matokeo ya uelewa finyu wa mafundisho ya biblia na quran.biblia inasema adamu alimzaa kaini na habili,na baada ya kaini kumwua nduguye habili mwishowe alikimbilia ktk nchi ya nodi na akaoa huko.kumbe kulikuwa na nchi na kumbe kulikuwa na watu wengine ambao alioa.quran inasema mungu alimwambia malaika mimi nitamweka halifa ktk ardhi.khalifa ni kiongozi,mfalme au mtawala,vipi aje kiongozi bila kuwepo waongozwa.kwa kifupi sana adamu alikuwa nabii wa kwanza kwa mujibu wa kumbukumbu za zama hizi tulizonazo.
Zipo hoja nyingi juu ya jambo hili lakini kwa haraka nimeweka kwanza hizo mbili ili kupisha michango ya wengine.
 
natumia kimoja kwa sasa:
rejea bible mlango wa kwanza;
2;5 mungu akaijaza nchi viumbe hai kwa jinsi yake, wanyama wa mwituni na watambao
swali kwako
unajua maana viumbe hai??
Hapo hapo mwanzo
mlango wapili ukisoma tena utakutana mungu anasema akampulizia roho adam ili akaitawale dunia na vilivyomo ukisoma zaidi utaambiwa alipeleka kuishi bustani ya eden
swali
unajua maana ya kupuliziwa roho?

Viumbe hai vilikuepo tangu kale ila roho ya kumjua mungu haikuepo hapo kabla ilikuja baada ya kumteua adam aitangaze
so kulikuwa na watu wengi toka kale na ADAM SIO MTU WA KWANZA DUNIANI ILA NI MIONGONI MWA MAUDONGO YALIYOPEWA ROHO YA KUMJUA MUNGU

Biblia iko wazi kabisa kwamba Adam alikua mtu wakwanza Mwanzo 2:18 inaelezea: " Bwana Mungu akasema,Si vema huyo mtu awe peke yake, nitamfanyia msaidizi wa kufanana naye.."Hataagano jipya nalo linaelezea ukoo wa Yesu na kurudi kwa Adam kuonyesha kwambaalikuwa binadam wa kwanza. Katika
Luka3:23-38,
wa Mathati, wa Lawi, wa Melki, wa Yana, waYusufu,
wa Matathia, wa Amosi,wa Nahumu, wa Esli, wa Nagai,
wa Maathi, wa Matathia, wa Semei, wa Yusufu, waYuda,
wa Yoana, wa Resa, wa Zerubabeli, wa Shealtieli,wa Neri,
wa Melki, wa Adi, wa Kosamu, wa Elmadamu, wa Eri,
wa Yoshua, wa Eliezeri,wa Yorimu, wa Mathati, wa Lawi,
wa Simeoni, wa Yuda, waYusufu, wa Yonamu, wa Eliakimu,
wa Melea, wa Mena, wa Matatha, wa Nathani, waDaudi,
wa Yese, wa Obedi, wa Boazi, wa Salmoni, waNashoni,
wa Aminadabu, wa Aramu,wa Hesroni, wa Peresi, wa Yuda,
wa Yakobo, wa Isaka, wa Ibrahimu, wa Tera, waNahori,
wa Serugi, wa Ragau, wa Pelegi, wa Eberi, wa Sala,
wa Kenani, wa Arfaksadi,wa Shemu, wa Nuhu, wa Lameki,
wa Methusela, wa Henoko,wa Yaredi, wa Mahalaleli, wa Kenani,
wa Enoshi, wa Sethi, wa Adamu, wa Mungu.

Kwa mujibu wa haya maandiko, neno peke yake na Adam wa Mungu yanaonyesha hapakuwa na watu kabla ya Adam.
Nikirejea hoja yako

"wakuu mie napingana sana na ukweli huu kwani ni UONGO mtupu kwani hawa jamaa ni watu katika watu!
Je UNAMJUA BINADAMU WA KWANZA HAPA DUNIANI! TAFADHALI FUNGUKA!

Mwanzo 2:5-7

"hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."

Uwepo wa viumbe wengine

Mwanzo 1:24-25

"Mungu akasema, Nchi na izae kiumbe hai kwa jinsi zake, mnyama wa kufugwa, nacho kitambaacho, na wanyama wa mwitu kwa jinsi zake; ikawa hivyo. Mungu akafanya mnyama wa mwitu kwa jinsi zake, na mnyama wa kufugwa kwa jinsi zake, na kila kitu kitambaacho juu ya nchi kwa jinsi yake; Mungu akaona ya kuwa ni vyema."

Uumbaji wa Adam unafuatia baada ya kuwepo hivyo vitu kwenye mstari waMwanzo 24-25 kwa hiyo hivyo viumbe hai unavyovisema wewe, havikuwa watu.
 
Angalia vizuri hiyo sentensi, "MAMA YAO WOTE WALIO HAI", obviously alikuwa kulikuwa na walio hai tayari (adam na hawa walikuwa hawajazaa bado).

Mkuu sijakuelewa unachotaka kukielezea, unaweza kuyaweka vizuri maeleo yako tafadhali?
 
kimsingi Adamu wala Hawa si mtu wa kwanza ktk hii dunia,adamu aliishi miaka elfu sita na ushee iliyopita,ilihali dunia ilikuwepo zaidi ya miaka elfu mia moja iliyopita.dhana ya adamu kuwa mtu wa kwanza ni matokeo ya uelewa finyu wa mafundisho ya biblia na quran.biblia inasema adamu alimzaa kaini na habili,na baada ya kaini kumwua nduguye habili mwishowe alikimbilia ktk nchi ya nodi na akaoa huko.kumbe kulikuwa na nchi na kumbe kulikuwa na watu wengine ambao alioa.quran inasema mungu alimwambia malaika mimi nitamweka halifa ktk ardhi.khalifa ni kiongozi,mfalme au mtawala,vipi aje kiongozi bila kuwepo waongozwa.kwa kifupi sana adamu alikuwa nabii wa kwanza kwa mujibu wa kumbukumbu za zama hizi tulizonazo.
Zipo hoja nyingi juu ya jambo hili lakini kwa haraka nimeweka kwanza hizo mbili ili kupisha michango ya wengine.

Mwanzo 2:5-7

"hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."

HAPANA MTU WA KUILIMA ARDHI......kisha "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi......" hao watu wa kwanza (Kabla ya Adam na Hawa) ni akina nani na walikuwa wapi hichi kipindi cha hayo maandiko?
 
inasemekana Mungu alipomuumba Adamu pale anaposema na tumfanye mtu kwa mfano wetu, Mungu akamuumba Adam, Mwanamume na Mwanamke akwaumba, halafu baadaye tunasoma Mungu akimletea usingizi Adam kuumba mwanamke mwinigne, Eva. inasemekana yule mwanamke wa kwanza alitoroka kulingana na watafiti wa Biblia. unajua biblia haikumaliza kujaza gaps nyinig kwenye biblia ambapo unakuta baadhi ya gaps katika kitabu cha mwanzo zinakamilishwa kwenye kitabu cha ufunuo au kingine chochote au zinaachwa blank kabisa kwani hazina impact ya moja kwa moja kwani kutokujulikana kwazo hakupunguzi mpango wa ukombozi ambao Mungu tayari ameuweka .Hiviyo huyo mwanamke wa kwanza akawa anamdhalau Adam, akagoma kulala nae, kulingana na huo utafiti na mwisho wa siku akatoroka kwa kuliita jina la Mungu (ELOHIM) lilokuwa limefichwa kwa wanadamu by that time sijui nani alimwambia, hata YESU alilitaja wakati anakata Roho. alipolitaja tu akapata nguvu ya kutoroka duniani kwenda mbinguni malaika wakaingilia kumzuia na akapelekwa kifungoni ila walau jina lake limetajwa kwenye kitabu cha nabii Isaya anaitwa Lilith nodo Mungu akaona kuondoa hizi dhalau inabidi nimuumbie Adam mwanamke kutoka kwake moja kwa moja.
 
bdo
well done kwa kuweza kutambua kulinga bible mwanzo- kuwa 'mtu' anayezungumziwa hapo kiroho ya kumjua mungu ni nani yes atakua adam lakini kama ni mwelewa utakuta mungu alishaumba viumbe hai siku nyingi lakini hawakuwa wakimjua mungu
soma uelewe kuwa adam sio binaadam wakwanza kuwepo duniani na USIPENDE KUKARIRI
 
Last edited by a moderator:
Mwanzo 2:5-7

"hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.
Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi, akampulizia puani pumzi ya uhai; mtu akawa nafsi hai."

HAPANA MTU WA KUILIMA ARDHI......kisha "Bwana Mungu akamfanya mtu kwa mavumbi ya ardhi......" hao watu wa kwanza (Kabla ya Adam na Hawa) ni akina nani na walikuwa wapi hichi kipindi cha hayo maandiko?

HAPANA MTU WA KULIMA ARDHI ndugu sio ardhi uijayo wewe ndugu zamani palikuwa na kila kitu ndugu
ardhi inayozungumziwa hapa ni ya kiroho watu wengi walikua hai lakini mungu hakuwapa roho ya kumjua mungu
 
kimsingi Adamu wala Hawa si mtu wa kwanza ktk hii dunia,adamu aliishi miaka elfu sita na ushee iliyopita,ilihali dunia ilikuwepo zaidi ya miaka elfu mia moja iliyopita.dhana ya adamu kuwa mtu wa kwanza ni matokeo ya uelewa finyu wa mafundisho ya biblia na quran.biblia inasema adamu alimzaa kaini na habili,na baada ya kaini kumwua nduguye habili mwishowe alikimbilia ktk nchi ya nodi na akaoa huko.kumbe kulikuwa na nchi na kumbe kulikuwa na watu wengine ambao alioa.quran inasema mungu alimwambia malaika mimi nitamweka halifa ktk ardhi.khalifa ni kiongozi,mfalme au mtawala,vipi aje kiongozi bila kuwepo waongozwa.kwa kifupi sana adamu alikuwa nabii wa kwanza kwa mujibu wa kumbukumbu za zama hizi tulizonazo.
Zipo hoja nyingi juu ya jambo hili lakini kwa haraka nimeweka kwanza hizo mbili ili kupisha michango ya wengine.

As kum je huiamini qurani?km unaiamini Mungu anasema walaqad khalaqna l insaani min sulaa lati min twin maanayake ni kwa hakika nimemuumba binaadamu kwa kutumia udongo uliovunda na unaotoa harufu ,
Na ktk vitabu vyote vinne vya Mungu vimeelezea kuwa binaadamu aliyeumbwa kwa udongo ni Adam je huamini?na sijaona sehemu yyte inayosema kuwa b4 adam kulikuwa kuna watu wengine
Quran inasema zimepita dahri au karne nyingi sana kiumbe binaadamu hakuwepo na maelezo yanasema ndipo MUngu akaumba binaadamu
Hapo mwanzo dunia ilikuwepo na viumbe majini
 
HAPANA MTU WA KULIMA ARDHI ndugu sio ardhi uijayo wewe ndugu zamani palikuwa na kila kitu ndugu
ardhi inayozungumziwa hapa ni ya kiroho watu wengi walikua hai lakini mungu hakuwapa roho ya kumjua mungu
Mwanzo 2:5-7

"hapakuwa na mche wa kondeni bado, wala mboga ya kondeni haijachipuka bado, kwa maana Bwana Mungu hajainyeshea nchi mvua, wala hapana mtu wa kuilima ardhi; ukungu ukapanda katika nchi, ukatia maji juu ya uso wote wa ardhi.

Kwa hiyo, mche, mboga, mvua ardhi na maji vinavyotajwa hapa navyo vilikua vya kiroho?
 
As kum je huiamini qurani?km unaiamini Mungu anasema walaqad khalaqna l insaani min sulaa lati min twin maanayake ni kwa hakika nimemuumba binaadamu kwa kutumia udongo uliovunda na unaotoa harufu ,
Na ktk vitabu vyote vinne vya Mungu vimeelezea kuwa binaadamu aliyeumbwa kwa udongo ni Adam je huamini?na sijaona sehemu yyte inayosema kuwa b4 adam kulikuwa kuna watu wengine
Quran inasema zimepita dahri au karne nyingi sana kiumbe binaadamu hakuwepo na maelezo yanasema ndipo MUngu akaumba binaadamu
Hapo mwanzo dunia ilikuwepo na viumbe majini

mkuu na unijuze viumbe wengine wameumbwa kwanini ...mitambo ama
viumbe vyote pamoja na binadamu wameumbwa kwa udongo tu
 
hichi kitabu sijui hata kwa nn kinaaminiwa kiko full of incosistence na uwongo mwingi.... hawakua wenyewe hata biblia kwa wanaoiamin inaonyesha hawakua wenyewe, soma hapa

genesis 4: 13 na kuendelea:- But Cain answered the Lord, "My punishment is too great to bear!Since You are banishing me today from the soil, and I must hide myself from Your presence and become a restless wanderer on the earth, whoever finds me will kill me."
15Then the Lord replied to him, "In that case, whoever kills Cain will suffer vengeance seven times over, And he placed a mark on Cain so that whoever found him would not kill him. 16Then Cain went out from the Lord's presence and lived in the land of Nod, east of Eden.

sas maswali rahisi tu ni kua kama walikua wenyewe tu cain na wazazi wake cain alikua anaogopa atauliwa na nani alivyofukuzwa na mungu? na huko nod inaonekana ilikua town iko poa tu hadi mshkaj akaend kuanza maisha uko.... na ukisoma bible zaidi mbele mshakaj alipata na jiko kabisa uko mji unaoitwa nod.
 
Back
Top Bottom