Adhabu ya Haji Manara iwe fundisho kwa wote wenye Tabia kama zake

Adhabu ya Haji Manara iwe fundisho kwa wote wenye Tabia kama zake

Error 404

JF-Expert Member
Joined
Jun 21, 2022
Posts
2,151
Reaction score
3,493
Kwenye Maisha kuna kitu kinaitwa kiongozi na Mamlaka ya kiongozi ,kila kiongozi huwa kuna maamuzi ambayo anaweza kuamua kutokana na Mamlaka aliyo nayo.

Kwa upande wa Haji Manara kama inavyonunukuliwa alichokisema kwa kiongozi wa TFF "Wewe unanifatafata sana, hii ni mara ya tatu, sikuogopi kwa lolote,kwa chochote na huwezi kunifanya chochote. Nina uwezo wa kukufanya chochote na huna cha kunifanya.” kina Ukakasi mkubwa kama ifuatavyo:

1. Alikuwa anapima Mamlaka ya kiongozi husika ,na kinachotokea ni kuonyesha uwezo ambao anao kiongozi huyo na TFF kwa ujumla, hiki kitu cha kudharau madaraka ni kikubwa kwenye uongozi kuliko hata mnavyosema vya kumuita mtu mjinga au mpumbavu.

2. Kwa hiyo kauli alikuwa anaonyesha yeye ni mkubwa kuliko TFF na huyo Kiongozi na ana watu wa kumlinda Nyuma yake -Godfather .Na TFF inajaribu kuuonysha Umma kuwa wao sio wakupelekesha tu.

Kwahiyo wanamichezo na msio wanamichezo anachokipata Manara ni sawa kabisa na liwe Fundisho hata Makazini waajiriwa mjifunze kuheshimu viongozi.

Hayo maneno yapo sana hata Maofisini na mitaani huko ,Mabosi wakijibu kwa vitendo mnawaona wabaya lakini hizo kauli ni mbaya sana kuambiwa kiongozi.

Kapicha Haka pia kanazunguza Mengi kwa wale wataalamu wa Body Language
.
IMG-20220726-WA0017.jpg


Haji Manara Huyu


Vs Manara Huyu kimebadilik nini ?



But Yote kwa Yote adhabu ipunguzwe kuna vitu kajifunza tayari
 
rais wa TFF ana mamlaka gani wakati yuko chini ya Watu kibao kuanzia BMT hadi Wizara!
 
Shida moja watu mnachukulia hilo jambo kishabiki sana...
Hata ili kamati ilikuwa ya wahuni tu wasiofuata sheria
 
Utakuwa mwanayanga wewe
Sio yanga hata walisema TFF ni wapumbavu ni msemaji wa simba..
Ila jana nilimsikiliza Haji ni kuna ukandamizaji mkubwa sana TFF na TFF walijibu kiwepesi sana..
 
Back
Top Bottom