Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
Katika amri kumi za mungu. Kuna katazo kuwa usiue.hivyo dunia hakuna kosa lolote ambalo anaweza Fanya na adhabu ikawa kifo.hivyo hurusiwi kuua binadamu kwa namna yoyote ile
Mzee unachanganya habari.Katika ulimwengu wa uislamu na sheria za haki,hukumu zina misingi yake kadhalika masharti yake.

Adhabu ya kifo katika ulimwengu wa kiislamu ni haki na ikikidhi vigezo,lazima itekelezwe na hutakiwi kusita au kutekeleza amri ya Mola mlezi mwenye kujua.Adhabu ya kifo ina hekima zake na lengo ni kutokomeza maouvu katika mtindo huo.

Sheria ya kiislamu imekuja kusimamia haki na kuwaadabisha waouvu na kuwalipa mema wale wema,sheria ya kiislamu imekuja kuweka sawa mambo na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.

Sheria ya kiislamu imekuja kulinda akili ya binadamu isichafuliwe,imekuja kulinda vizazi na nasaba,imekuja kumlinda mwanamke na mfano wake,ndio maana ikawa uzinifu ni harafu,mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi na mtoto wa nje ya ndoa ni wa mwanamke si wa mwanaume.

Adhabu ya kifo katika uislamu haitekelezwi kibubusa yaani kichwa mchunga,katika uislamu kuna sheria ambazo hazitekelezwi mpaka sehemu husika iwe iko chini ya utawala wa kiislamu na kuwe kuna mtawala.
Mfano wa nchi hizo ambazo hutekeleza sheria hizo ni saudi Arabia.

Halafu sisi waislamu hatuna amri kumi mzee,sisi tuna kitabu na mwenendo wa mtume amani ya Allaah iwe juu yake,yaani tuna zaidi ya hivyo....

Kuna tofauti kati ya mtu kumuua mwenzie na dola kusimamia sheria,hivi ni vitu viwili tofauti.Jambo la kwanza ni haramu mtu kuiua nafsi ya mwenzie pasi na haki,na ukibainika umefanya hivyo basi adhabu yako ni kuuwawa.Kwenye hiyo ahdabu ya wewe kuuwawa inasimamiwa na dola.Kwahiyo ni jambo lisilo epukika...
 
Nchi kama Saudi Arabia inaongozwa direct Na agents wa kuzimu hizo zinazoitwa Sharia laws Ni Sheria kutoka kuzimu Na ibilisi ndio anayezisaini Ni Sheria za kishenzi sioni mantiki yake. Wanawake Ni miongoni mwa wanaopata sana shida juu ya Sheria hizi
Mzee naona unatumia hisia kuwasilisha
 
Utashangaa katika hao ndugu yupo alotenda kosa sawa na la anayeenda kuchinjwa ila tu tofauti ni kwamba hakuonekana na mtu!!!!

Wasaudi sijui IQ yao ngapi
Hivi ushawahi kujiuliza kwanini kipimo cha IQ hakitumiki katika kupima uwezo kutambua mambo mema na mabaya na kujua vipi ujilinde na maovu na ufanye juhudi ya kufanya mema.Kipimo cha IQ kimejikita katika mambo ya kipuuzi na kukariri machambo itu ambacho kukariri au kuhifandhi majambo si kipimo cha mtu kuwa na akili nyingi....

Sasa nafasi ya IQ ni kwa wajinga mfano wao,wajinga ambao hawajui akili iko wapi,huku wakisema akili ipo kichwani.Binadamu si mkamilifu vipi ajue kipimo cha akili za watu ?

Unajifaragua n IQ mfano wako ni sawa sawa na wale wanaojifaragua kwa elimu ya falsafa elimu ambayo haina hata uwezo wa kumfundisha mwanadamu jinsi ya kuchamba akitoka haja au jinsi ya kula ?

Mnasafari ndevu sana,katika kujikwamua katika utumwa wa kifikra...

Halafu saudia mzee katika kutekeleza sheria za Allah aliyejuu hakuna cha huyu mtoto wa mfalme au mtoto wa nani kama umekutwa una hatia unahukumiwa mzee,tafuta matukio ya hukumu hizo utajionea.
 
Mzee adhabu ya kifo ipo na ni ya tangu na tangu,hapa duniani lazima wawepo watu ambao wanasimamia sheria za Allah mlezi.Mzee dunia ni yetu sote,haitakubalika waouvu wafanye maovu yao na ufisadi halafu wakaachiwa wanatamba.Mambo hayo huyakuti katika nchi za kiislamu zenye kuendeshwa na sheria,mambo hayo utayakuta katika nchi za kidemokrasia,nchi za utawala wa kifedhuli na ujinga ulivuka mipaka.Ndio maana katika uislamu DEMOKRASIA NI HARAMU NA NI UKAFIRI.
 
Sheria za mwanadam sio za Mungu timiza au usitimize utahukumiwa na Mwanadam mwenzio... Ila za Mungu utahukumiwa na Mungu Mwenyewe...
Sheria za Mola kwa hapa duniani zinasimamiwa na waja wake.Allah aliyejuu aamjiwekea mipaka na kujiharamishia majambo,mathalani Allah aliyejuu amejiwekea hali ya kutomdhulumu mja wake yoyote awaye,na amejiharamishia kutokumuadhiu mja mpaka awe ameshafikiwa na ujumbe wa haki juu ya kile anachokifanya mja huyo.

Sheria za Allah aliyetukuka zilitufikia sisi kupitia waja wake wateule,waja ambao walilazimishwa kuzifanyia kazi sheria hizo ili nidhamu iwepo katika uso huu wa dunia...
 
Labda utusaidie hapa.
hukumu inayozungumzwa hapa inahusishwa na Quran kitabu cha Allah na pia mchinjaji anasema anafanya kazi ya Allah. Kwa kifupi uislam unahusika katika hili.
Je, hao mosad,USA-guantano na wengineo wanapofanya majanga yao, wanahusanisha na udini? iwe uislam ama ukristo?
na kwanini kila ikitokea kuzungumzia machafu yote yanayohusishwa na uislam, badala ya kutoa jibu la kueleweka mnaleta hoj dhaifu, ooh mbona america wameua kule Afrighan, Israel wanawaua palestina, kwani walishasema tunafanya haya kwaajili ya ukristo au kupromote upagani??
 
Halafu kuna watu walitaka mahakama ya kadhi! Nahisi walikuwa na kisa na mtu.
Wengi katika waislamu waliokuwa wanataka mahakama ya kidini walikuwa hawana elimu sahihi juu ya mahakama hiyo,mahakama ya kidini haipangiwi vya kuhukumu,yaani ishughulikie mambo ya mirathi na ndoa halafu mambo ya kuwaadabisha watu isishughulikie,haikuwa kuwepo mahakama ya kiislamu ya namna hiyo,nio maana kwa wale wenye kujua dini walikuwa wanawapa nasaha baadhi ya viongozi wa kiislamu kutolishupalia jambo hilo.Mahakama ya kiislamu ni katika dola ya kiislamu,kwa maana majambo yao yote yahukumiwe chini ya mahakama hiyo sio majambo fulani tu....Na hakuna dola chini ya dola,yaani hakuna dola mbili sehemu moja yaani hakuna dola mbili katika nchi moja,sharti lazima dola moja itoke ibaki moja...
 
Da!! Hii inasikitisha
Inasikitisha nini mzee ? Katika vitu ambavyo vinanihuzunisha sana ni utupu wa waislamu juu ya dini yao.Hakuna sheria ambayo inatoka kwa Allah ikawa haina maslahi na binadamu yaani ikawa haina maslahi na sisi.

Ulimwengu ama dunia imepita katika hatua nyingi sana katika safari ya kustaarabika.Katika kuliweka sawa hilo na kuondoa tabia za kinyama za baadhi ya wanadamu dhidi ya wanadamu wenzao,Allah akaleta wajumbe wajumbe ambao aliwapa kila kitu,yaani mpaka ubavu wa kupigana na maadui na kusimamia haki,yaani hata mnyonge na yeye aheshimike mambo utayaona katika uislamu tu kwa namna yalivyopewa kipaumbele kisicho na mfano.

Vipi uwe muislamu halafu uzitilie shaka sheria za Mola wako mlezi Mola ambaye hakosei ? Waislamu wengi ni waislamu jina.Mtume amani ya Allah iwe juu yake anasema "uislamu ulikuja mgeni na utaondoka ukiwa mgeni kama ulivyokuja,na bishara njema kwa wale watakao onekana wageni"

Waislamu wa zama za leo hawani wanauchukulia poa sana uislamu,hawana muda wao wala hawana muda wa kujifunza uislamu wao,kutokana na hivyo inawapelekea mpaka kukufuru.Allah atuepushe na hilo.

Tujifunze uislamu ukweli wa kujifunza ili tuutetee mbele ya wale wenye kuupiga vita...Inasikitisha sana kuona waislamu wakizipinga sheria za Mola wao mlezi mjuzi wa kuadhibu.
 
Nilikuwa nikitafuta huruma ya binadam mpka kumshikia upanga mwenzio ss nimefahamu fika ni tag niongeze ghathabu na uelewaa
 
Wale binadamu hata kama waalifu huoni Ni unyama kukata kichwa cha mtu Ile inaonyesha Ni jinsi gani wasivostaarabika
Kwahiyo kukata kichwa cha mtu ndio kutostaaribika ? Maana hii ya ustaarabu umeipata wapi ?
 
Kusema kwake hivyo hakukupinga sheria hiyo au kubatilisha sheria hiyo....Bila shaka walikuwa wana utaratibu mmbaya wa kutekeleza sheria hizo...
 
Na Sisi bila Yesu Nadhan tungekuwa kwenye mkenge wa mzee Lucifer
Yaani nyinyi sema hamjui tu wazee,ila muda wa sheria za huyo mnayemuita yesu umeshapita.Wewe unachotakiwa ni kuchukua hii akiba ya maneno....Je ukifa katika hali hiyo ya ukiristo utaenda kumueleza nini Mola aliyekuumba ?

Ujumbe nimeshakufikishia mzee....
 
Mzee naona unatoa tafsiri yako,tafsiri ambayo sio sahihi.Yawezekana unajaribu kuutetea uislamu lakini kumbe unapotosha.Huyo mtu wala hakubanwa sababu swali lilikuwa rahisi na amelijibu kwa ufasaha na usahihi.

Sheria za Allah katika utekelezaji wake lazima zisimamiwe na sisi binadamu tena miongoni mwetu ambao wana vigezo.Yeye kuteuliwa na kulipwa kwa ajili ya kazi hiyo si jambo na wala si makosa.sababu yupo katika kutekeleza sheria ya Allah aliyejuu,na Allah mwenyewe ameshatuambia "Wala tusiwe wazito katika kutekeleza amri zake".

Sasa sijui umeyasema hayo kwa kutokujua au vip ?
 
Naona umepewa sanamu ya ng'ombe ya kwa sura ya binadamu...
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…