Mzee unachanganya habari.Katika ulimwengu wa uislamu na sheria za haki,hukumu zina misingi yake kadhalika masharti yake.Katika amri kumi za mungu. Kuna katazo kuwa usiue.hivyo dunia hakuna kosa lolote ambalo anaweza Fanya na adhabu ikawa kifo.hivyo hurusiwi kuua binadamu kwa namna yoyote ile
Adhabu ya kifo katika ulimwengu wa kiislamu ni haki na ikikidhi vigezo,lazima itekelezwe na hutakiwi kusita au kutekeleza amri ya Mola mlezi mwenye kujua.Adhabu ya kifo ina hekima zake na lengo ni kutokomeza maouvu katika mtindo huo.
Sheria ya kiislamu imekuja kusimamia haki na kuwaadabisha waouvu na kuwalipa mema wale wema,sheria ya kiislamu imekuja kuweka sawa mambo na kuifanya dunia kuwa sehemu salama ya kuishi.
Sheria ya kiislamu imekuja kulinda akili ya binadamu isichafuliwe,imekuja kulinda vizazi na nasaba,imekuja kumlinda mwanamke na mfano wake,ndio maana ikawa uzinifu ni harafu,mtoto wa nje ya ndoa hana haki ya kurithi na mtoto wa nje ya ndoa ni wa mwanamke si wa mwanaume.
Adhabu ya kifo katika uislamu haitekelezwi kibubusa yaani kichwa mchunga,katika uislamu kuna sheria ambazo hazitekelezwi mpaka sehemu husika iwe iko chini ya utawala wa kiislamu na kuwe kuna mtawala.
Mfano wa nchi hizo ambazo hutekeleza sheria hizo ni saudi Arabia.
Halafu sisi waislamu hatuna amri kumi mzee,sisi tuna kitabu na mwenendo wa mtume amani ya Allaah iwe juu yake,yaani tuna zaidi ya hivyo....
Kuna tofauti kati ya mtu kumuua mwenzie na dola kusimamia sheria,hivi ni vitu viwili tofauti.Jambo la kwanza ni haramu mtu kuiua nafsi ya mwenzie pasi na haki,na ukibainika umefanya hivyo basi adhabu yako ni kuuwawa.Kwenye hiyo ahdabu ya wewe kuuwawa inasimamiwa na dola.Kwahiyo ni jambo lisilo epukika...