Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
kumbe yaliyofanywa na mudy ni matus sasa mbona mnatetea ukatili uliokwenye sheria za kislamu
Kama kweli unataka kujua usitumie lugha ya matusi wala kejeri. Weka swali na hoja zako ujibiwe.
Kama umekusudia kuleta kejeri basi baki mwenyewe na kejeri zako.
Nasubiri jibu lako wewe upo upande gani?
 
Kama kweli unataka kujua usitumie lugha ya matusi wala kejeri. Weka swali na hoja zako ujibiwe.
Kama umekusudia kuleta kejeri basi baki mwenyewe na kejeri zako.
Nasubiri jibu lako wewe upo upande gani?
mimi siongelei kejel na kama kuongea ukwel ni kejeli basi nitaendelea kuzisema hizo kejeli na hoja yangu ninalaani uislamu kwa sheria zao za kikatili au wewe kwako ni furaha jinsi damu zinavyomwagika kila iitwapo leo?
 
Usiwe unazungumzia watu ambao uislam wenyewe ubawapiga vita kisha ukasema wametumwa na uislam.
 
Vingunguti ya Saudi Arabia katika ubora wake. Halafu wanajifanya wanamjuwa Mungu kwa kujifanya wao ni zaidi yake, shida kweli kweli. Hii dunia hii jamani mbona tunajitakia laana wenyewe?
 
Hii thread imejaa mihemko ya kidini kutoka kwa wachangiaji..

Yaani hadi mashehe nao wameona ni thread chonganishi wakaamua kuleta utetezi wao, wanachekesha kweli.

Hakuna dini yeyote ya kweli duniani inayompa binadamu mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu mwenzie hata kama amefanya kosa gani.

Wake up folks!!
 
Sasa Vatican kununua sauna inahusiana nini na adhabu ya kuchinjwa?
Badala kunilalamikia mimi kuhusu sauna, kwanini husienda Vatican kulalamika juu ya kununua sauna?
Wajinga na wauaji ndiyo wanashabikia vifo vya kuchinjwa binadamu kama kuku. Kesi zenyewe haziendeshwi kwa hski, mf. mzuri ni kesi ya Rizana, yule binti alionewa kabisa. Ila hakuwa na mtetesi akiwa katikati ya wapenda damu za watu in the name of religion. These are nothing but killers of innocent blood
 
Safi sana kwa kuleta huu Uzi.

Watu wanatakiwa wafunguke/wapate ufahamu na taarifa mbalimbali katika ulimwengu huu wa leo ambao ni digital.

Kama nyekundu ni nyekundu,,,nyeupe ni nyeupe tu.


Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Kwa mfululizo wa makala za huyu bwana tutajitahidi kusahihisha ufahamu kadri ambavyo patakua na upotoshaji ili kuitakasa sheria ya uislam iliyisalimika na mapungufu. Na hili si kwasababu yakuitetea Saudia kama Saudia bali kutetea yale wanayoyasimamia katika hukmu za mola wetu alizowahukumia waja wake.

Hukumu za uislam zilizofungama na adhabu ya kifo zipo nyingi mara nyingi hukumu hizo anahukumiwa nazo mwanaume au mwanamke ambaye tayari ameshafika baleghe, mwenye akili timamu, na pakiwepo na sura ya kukusudia kufanya hilo kosa litalomlazimu auwawe. Kwa hali hiyo ambao hawajafika baleghe na wasio na akili timamu hawatazingatiwa. Kwa wale waliofanya bila kukusudia nao wanamlolongo na taratibu zao.

Katika kesi iliyoletwa kuhusiana na huyu dada inaingia upande wa adhabu ya kifo kwa aliyeua moja kwa moja mf. Kwa kupiga risasi, kuchoma kisu n.k au aliesabisha kifo kwa mwingine(kwa kuweka sumu kwenye chakula/kinywaji, kutega mtego utaosababisha mtu kufa n.k.

Ufafanuzi upo kama ifuatavyo.
Kwanza sheria hii imetajwa katika
qur'an 17.33
"Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa."

Hapa tunaona imekatazwa kuuliwa nafsi isipokua kwa haki. Na haki hapa ya kuua moja wapo ni kisasi atacholipiziwa yule aliyeua nafsi. Na kisasi hiki kitasimamiwa/au kutekelezwa na mtawala.

Sheria imempata mrithi wa yule aliyeuliwa chaguzi baina ya kulipa kisasi kwa maana ya kutaka muuaji nae auliwe au asamehe kwa kupewa diya, au asamehe bila ya kupewa chochochote kwa hiyari yake iwe hakuombwa kusamehe au ameombwa. Hivyo basi hukumu hii itafatilizwa kwa matakwa ya warithi.
Kuna hekma kubwa sana imewekwa katika utekelezaji wa hukumu hii. Kwanza imetakiwa isimamiwe na mtawala ili usitokee utata baina ya familia mbili ikiwa familia ya warithi watachukua sheria mkononi. Pili utekelezaji wake una sura ya kutisha ili watu wengine wapate funzo na hofu ya kuua nafsi. Ikiwa sheria hii haikutekelezwa kuna uwezekano mkubwa wa muuaji kuendelea kufanywa na huyu muuwaji kwa kujua hakuna atalofanywa pia watu wengine watachukua mfano huo na wanaweza wakawaua wenziwao kwa kujua hakuna mtu atakae wachukulia sheria. Kwa hivyo kuna funzo kubwa kwa wengine na kwa hali hiyo hofu inapatikana kwa watu na uwoga wa kuua unaingia katika nyoyo zao hivyo kuzisalimisha damu za watu wengine ambazo zingemwagwa kwa tabia chafu ya kuuwana watu wao kwa wao.
Na kuhifadhi damu za watu ni lengo moja kati ya malengo ya sheria ya uislam.

Laiti ungejua uthibitishaji wa fulani kumua fulani ulivyo usingesema hayo. Mlolongo wake unafanywa kwa uadilifu mkubwa sana.
Pili ikiwa kuna uthibitisho wa uwongo umetolewa ili tu huyo dada auliwe basi aliyeongopa amebeba mzigo wake wa madhambi mpaka kiyama na atalipwa kwa hayo aliyoyafanya.
 
Kuzungumza ili hali umetanguliwa na ujuzi ni jambo bora sana kuliko kuzungumza bila elimu yoyote. Na hakika hujui uislam unawazingatia vipi watawala. Dini haikandamizi mtu dini ina mpa kila mtu haki yake. Sisi tuliopita darasa za dini tunajua haki kubwa ya mtawala iliyojuu yetu ni kumtii madamu hajatuarisha kumuasi mola wetu. Sasa usichukizwe na watu waliokubali kua chini ya utii wa Mfalme ili mambo yao yatengemae. Utii unaofanywa na raia kwa mtawala unalinda damy za watu wengi sana lau ingetokea siku watoke katika utii wake na wamuasi(wafanye jaribio la kupindua) zitamwagika damu za watu wengi sana na mali pia zita angamia uhalisia ni kwamba maafa makubwa sana yatapatina. Kwa sababu hiyo sheria imewalazimisha waislamu kumtii mtawala wao ili kulinda hayo nilioweka hapo juu.
 
Kama utanisaidia kuelezea jambo ntakutatulia kitendawili chako.
Elezea namna uislam unavyochanganya dini na utawala.
 
Raia wa nchi za mashariki ya kati yaani waarabu bado hawajazoea utawala wa democrasia.
Sadam Hussein alifanikiwa kutawala kwa mabavu ktk nchi ya Irak.
Muamal Gadafi naye alifanikiwa kutawala kidikteta nchini Libya.
Walipoondolewa kimabavu, nchi hizo hazijatengemaa hadi leo.
Hivyo ndicho kinachofanyika Saudi Arabia, Iran, Syria, Yemen nk.
Waarabu bado hawajazoea utawala wa vyama vingi.
Ndio maana watawala wa huko wanatumia mabavu, vitisho, sheria kali, adhabu kali ili kuweza kuwanyamazisha wapinzani wao kisiasa na kitamaduni.
Sadam hussein aliwaua sana wapinzani wake wa kisiasa, na nchi ikatulia.
Kwakuwa Msahafu unasheria kali basi watawala wa baadhi ya nchi za mashariki ya kati wanautumia kama msumeno wao wa kujilinda.
Hata iwe kwa heri au shari kumchinja mtu hadharani na jambia hakukubaliki kwa maisha ya kisasa.
Ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Sidhani kama utawala wa Sharia unakubalika na waislamu wote.
kwani kuna nchi zinawaislamu wengi lakini hazitumii amri za Sharia,
kama Zanzibar kabla ya Muungano.
Amri za Sharia kwa mimi kama mchambuzi huru naziona zimepitwa na wakati. kwasababu hazitoi nafasi ya mkosaji kuelimishwa ubaya wa kosa lake na hatimaye kuacha tabia yake mbaya.
Kwamfano
Wafungwa wa makosa ya wizi, huko jera pamoja na mambo mengine wanafudishwa tabia mjema, na kazi za ufundi, kilimo nk, ili kuweza kujitegemea.
Jambo hili hupelekea mfungwa kujirekebisha na hatimaye kuwa raia mwema badala ya kilema.
Huwa na uwezo wa kuzalisha mali, na kusaidia jamii yake.
Mfano mwingine,
Sharia inamhukumu kifo aliye badili dini kutoka Uislamu na kuwa muumini wa dini nyingine kama ya Kikristo, Kihindu nk.
Sasa hapo kuna tatizo gani wakati tendo la kuabudu ni la hiari na mtu anao uhuru wa kuabudu dini anayotaka. Mtu anaweza akawa mwislamu wa kurithi toka kwa wazazi, ukubwani inawezekana akaenda kusoma vyuo vyenye watu wa imani tofauti, huko wakamshawishi na akaona inafaa kwake kuwa muumini wa dini nyingine. Sasa hapo dhambi yake ninini hadi ahukumiwe kuchinjwa hadharani ?
Baadhi ya watawala wa nchi za mashariki ya kati wanatumia Sharia kama fimbo yao ya kuwaumiza na kuwatisha wapinzani wao,
Na kwakuwa raia wa nchi hizo wengi ni waislamu, wanashindwa kuikataa Sharia maana ipo kwenye kitabu chao cha dini wanayoiamini.
Kwao kukataa Sharia ni kama kukufuru, hivyo hawana cha kujitetea zaidi ya kuzikubali hata ikiwa kwa shingo ipande.

Ni uchambuzi wa kisiasa tu.

Ramadhan njema.
 
Nionavyo mimi kimsingi wenye chuki dhidi ya uislam kwanza hawataki kujua malengo ya uislam pia hawataki kukubali kua wao uislam hawaujui wao wanataka kulinganisha uislam na wazungu kitu ambacho hakiwiani kwasababu wazungu wao mambo yao wanajipangia wenyewe na siyo maagizo ya mamlaka fulani hata likifika suala la mamlaka huwa ni kule kuhalalisha mawazoyaotu lkns si uhalisia wa hayo mamlaka. lkn uislama hakuna mawazo ya watu bali ni mamlaka pekee ktk hilo watu nafasiyao ni kufanya uchambuzi wakina ili kujiridhisha kama wameelewa vizuli sasa ukitafuta iwiano wa mambo hayo kwa mawazo yalio beba chuki dhi ya kingine itakua ni shidatu ndiomaana mtu yupo tayari aropoketu wakati hana ushahidi kimaandishi wala hoja zake hazitokani na maandishi bali ni mawazo yaketu nawapeni pongezi sana nyie waalimu wakiislam mnaoweza kuelimisha watu wenye mtazamo wa chuki bila kutafuta usahihi wa jambo mungu awabariki sana mimi binafsi siwezi kujenga hoja na mtu ambae unaona kabisa hayupo kwa ajili ya kuelewa yeye yupo kwaajili ya kuhaributu mimi siezi hongereni sana.
 
Said una hakika hayo nilosema hayapo vitabuni mwenu?
1. nieleze/ueleze uwanja huu, kwanini kwenye misikiti yenu mmeweka alama ya NYOTA na MWEZI( a star & Crescent moon) na ni kwanini lazima mfunge na kufungua mpaka uonekane MWEZI?
2. Unaposema msemaji hajui hata ameyatoa wapi maneno yake, na amekurupuka!! je, mimi niliyeandika humu ama Muhammad ayesema hayo 1400yrs ago na wewe unamfuata ndiyo alikurupuka?
3. Je, ukipewa ref. utazikubali?
 
Sasa kwanini auliwe? ikiwa aliingia mwenyewe kwa hiyari yake na kutoka ni hiyari yake? kuna siri gani ndani Allah anaogopa mtu akiijua akiwa huko kwenye uislam kisha akatoka na hamsini zake. ikiwa kweli DINI ya allah ni njema ama inahubiri wema. hofu ya nini??

1. Umeanza na KUMTAKASA mola wako kutokana na kuwa na HOFU ya watu kuuhama uislam. mola wako ni wa aina gani mpaka awe na HOFU? na ahitaji msaada wa utakaso toka waumini wake?
 
Status
Not open for further replies.
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…