Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Adhabu ya kifo kwa kuchinjwa mbele ya kadamnasi (Tahadhari: maelezo, picha na video za ukatili)

Status
Not open for further replies.
kumbe yaliyofanywa na mudy ni matus sasa mbona mnatetea ukatili uliokwenye sheria za kislamu
Kama kweli unataka kujua usitumie lugha ya matusi wala kejeri. Weka swali na hoja zako ujibiwe.
Kama umekusudia kuleta kejeri basi baki mwenyewe na kejeri zako.
Nasubiri jibu lako wewe upo upande gani?
 
Kama kweli unataka kujua usitumie lugha ya matusi wala kejeri. Weka swali na hoja zako ujibiwe.
Kama umekusudia kuleta kejeri basi baki mwenyewe na kejeri zako.
Nasubiri jibu lako wewe upo upande gani?
mimi siongelei kejel na kama kuongea ukwel ni kejeli basi nitaendelea kuzisema hizo kejeli na hoja yangu ninalaani uislamu kwa sheria zao za kikatili au wewe kwako ni furaha jinsi damu zinavyomwagika kila iitwapo leo?
 
Vingunguti ya Saudi Arabia katika ubora wake. Halafu wanajifanya wanamjuwa Mungu kwa kujifanya wao ni zaidi yake, shida kweli kweli. Hii dunia hii jamani mbona tunajitakia laana wenyewe?
 
Hii thread imejaa mihemko ya kidini kutoka kwa wachangiaji..

Yaani hadi mashehe nao wameona ni thread chonganishi wakaamua kuleta utetezi wao, wanachekesha kweli.

Hakuna dini yeyote ya kweli duniani inayompa binadamu mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu mwenzie hata kama amefanya kosa gani.

Wake up folks!!
 
Sasa Vatican kununua sauna inahusiana nini na adhabu ya kuchinjwa?
Badala kunilalamikia mimi kuhusu sauna, kwanini husienda Vatican kulalamika juu ya kununua sauna?
Wajinga na wauaji ndiyo wanashabikia vifo vya kuchinjwa binadamu kama kuku. Kesi zenyewe haziendeshwi kwa hski, mf. mzuri ni kesi ya Rizana, yule binti alionewa kabisa. Ila hakuwa na mtetesi akiwa katikati ya wapenda damu za watu in the name of religion. These are nothing but killers of innocent blood
ADHABU YA KIFO KWA KUCHINJWA MBELE YA KADAMNASI




SEHEMU YA PILI





Katika sehemu ya kwanza ya makala hii niliandika kwa kina sana juu ya mfumo was adhabu ya kifo inavyotekelezwa nchini Saudi Arabia. Sikuishia hapo tu bali pia nilijadili kuhusu mtelelezaji wa adhabu hiyo (mchinjaji) Muhammad al-Besh.

Katika sehemu hii ya pili ya makala hii nataka nijadili visa vichache vilivyopo nyuma ya maisha ya ya watu ambao walihukumiwa adhabu hii na hatimaye kuchinjwa hadharani. Nataka kujadili ilikuwaje hasa mpaka kupelekea kuhukumiwa visa hivyo?

Katika mjadala wangu huu nitagusia zaidi visa ambavyo viligusa hisia za watu wengi na visa vingine kusababisha hata hasira ya kimataifa dhidi ya nchi ya Saudi Arabia.


911fca0601e1e4dde262cde849f0bb13.jpg




KISA #1: RIZANA NAFEEK


Umri: Miaka 24

Uraia: Sri Lanka

Kazi: Msaidizi wa Kazi za Ndani


Tarehe ya kuchinjwa: January 9, 2013, Saa 5 dakika 40 Asubuhi.





Nini hasa kilimkuta?



Rizana Nafeek binti muadilifu wa kiislamu, alizaliwa February 4, 1988 na kukulia katika kijiji cha Moothoor, wilaya ya Trincomalee nchini Sri Lanka.
Kutokana na wazazi wake kuwa wacha Mungu sana ndio maana hata alipozaliwa walimchagualia jina la Rizana mtoto wao likimaanisha "kuomba" (to pray).

Rizana ndiye mtoto wa kwanza kwenye familia yao yenye watoto wanne.

Familia yao ilikuwa ni moja kati ya familia masikini zaidi hapo kijijini, waliishi katika kijumba cha "mbavu za mbwa" kilichojengwa kwa nyasi.

Umasikini wao uliokithiri ulichangiwa kwa kiasi kikubwa kutokana na hali tete ya kiafya ya baba yake ambayo ilikuwa haimruhusu kufanya shughuli nzito. Enzi ambazo baba yake alikuwa timamu kiafya, alikuwa anajishughulisha na ukataji mbao msituni, na akasitisha shughuli hizo baada ya afya yake kuzidi kuzorota kadiri siku zilivyoenda.

Kitokana na afya ya mzee Nafeeq kuwa mbaya na kushindwa kufanya kazi, ili waweze kujikimu kimaisha, Rizana na wadogo zake walikuwa wakiokota kuni msituni na kwenda kuuza kijijini, wakati ambapo mama yao alikiwa anasaidia shughuli ndogo ndogo vibarua kwa wanakijiji wengine na kulipwa ujira.
Katika mtindo huu kwa miaka kadhaa ndivyo ambavyo waliweza kuendesha maisha yao.

Kama jinsi ilivyo kwa watoto wote wanaokua katika umasikini wa kupindukia, Rizana akajikuta anapata kiu ndani yake ya kuwa mkombozi wa familia yake. Akajikuta anapata kiu ya kutaka kuitoa familia yake katika aibu ya kuwa familia inayodharaurika na walau aweze kuipa familia yake maisha yenye staha na heshima mbele za wanakijiji wengine.
Ndipo hapa ambapo moja ya binamu zake aliyepo hapo hapo kijijini Moothoor akamshauri Rizana ajaribu "bahati" yake kwenda kutafuta ajira 'Uarabuni'.

Rizana akarudi na wazo hili nyumbani na kuwaeleza wazazi wake kuwa anataka ajaribu "bahati" ya kutafuta ajira Uarabuni.
Wazazi wake walilipinga suala hili mara moja baada tu ya Rizana kulitamka. Hoja yao kuu ilikuwa ni kwamba wanaogopa mtoto wao kwenda kunyanyasika Uarabuni. Walikuwa wamesikia 'stori' nyingi sana kuhusu wafanya kazi wa ndani namna ambavyo walikuwa wananyanyaswa na mabosi wao wakifika kwenye nchi za kiarabu. Hawakutana mtoto wao Rizana naye aende akanyanyaswe, waliona ni bora aendelee kuokota kuni kijijini.


Lakini Rizana alikuwa na kiu haswa ya kuindoa familia yake kwenye umasikini wa aibu, akajitahidi kwa uwezo wake wote kujieleza kwa wazazi wake na hasa hasa ni namna gani ambavyo kwenda kwake Uarabuni kutaleta 'neema' kwenye familia yao. Baada ya kujieleza sana kwa wazazi wake hatimaye wakakubaliana naye kuhusu kwenda kujaribu "bahati" yake huko Uarabuni.


Huu ulikuwa ni mwaka 2005, Rizana alikuwa ni kabinti ka miaka 17 tu.


f06cdf483dab4f266403f680a704bead.jpg

Hapa ndio nyumbani kwa kina Rizana Nafeek, kijijini Moothoor, nchini Sri Lanka

349f4f6cbd2f65d876dba0351e731e8c.jpg

Baba na mama mzazi wa Rizana Nafeek

c17fc722545ce81ec37a4207d4e428a3.jpg

Mama mzazi wa Rizana akiwa na wadogo zake Rizana



Baada ya wazazi kukubali Rizana aende kujaribu "bahati" yake Uarabuni, ikafanyika mipango ya kuwasiliana na makampuni ya uwakala wa kutafuta watumishi wa ndani ("mahausigeli") na kuwaunganisha na 'ajira' kwenye nchi za kiarabu. Kampuni hii iliitwa Badurdeen.


Lakini Rizana alikuwa na changamoto kubwa mbili.

Mosi, alikuwa hajui hata neno moja la kiarabu au kingereza. Lugha pekee aliyokuwa anaifahamu ilikuwa ni Tamil.

Pili, Rizana alikuwa hajafikisha umri wenye kumruhusu kwa mujibu wa sheria za kimataifa kupata ajira kwenye nchi ya kigeni.


Lakini madalali hao walimtia moyo kwamba hakuna changamoto yoyote ambayo wao watashindwa kuisawazisha alimradi tu akiwa tayari kwenda kufanya kazi Uarabuni.

Kuhusu kutojua kiarabu au kingereza, walimtia moyo kwamba wako wasichana wenzake wengi tu ambao nao walikuwa kama yeye wanafahamu 'lugha ya mama' pekee na Kiarabu walikwenda kukijulia huko huko kwenye ajira zao. Suala hili lilikuja kumgharimu sana Rizana huko mbeleni.

Pia kuhusu umri, mawakala hao wa ajira walimtengenezea Rizana cheti kingine cha kuzaliwa cha kughushi ambacho kilionyesha kuwa Rizana ana umri wa miaka 23.


Baada ya mipango hii yote kukamilika, familia ya Rizana wakakopa fedha kutoka kwa ndugu jamaa na marafiki na kuwalipa kampuni ya Badurdeen ada ya huduma hii ya kumuunganisha binti yao na ajira Uarabuni.

Mkopo huu waliokopa familia ya Rizana kutoka kwa ndugu, jama na marafiki walikuwa wameahidi kuulipa pindi tu ambapo Rizana akifika Uarabuni na kuanza kupokea mshahara.


*********


Siku ya tarehe 1April 2005, Rizana aliwasili kwenye mji wa *Dhawadhimi* (wengine hutamka "Dwadmi") nchini Saudi Arabia, karibu kabisa na mji mkuu wa nchi hiyo, Riyadh.

Muajiri wake ambaye alikwenda kukabidhiwa kwake alikuwa ni Bw. Naij Jiziyan Khalaf al Otaibi ambaye alikuwa ni afisa wa ngazi za juu katika wizara ya fedha ya Saudi Arabia.

Kwa mujibu wa taratibu za kazi nchini Saudi Arabia, kazi ya Uyaya (Nanny) na 'uhausigeli' (house maid) huwa zinatenganishwa lakini mara nyingi binti akiajiriwa anajikuta akifanya shughuli zote hizi mbili, yaani shughuli za nyumbani kama upishi na usafi (house maid) na shughuli za uangalizi wa watoto wadogo (nanny).
Hiki pia ndicho kilichomba Rizana kwa muajiri wake Familia ya Otaibi. Alijikuta anawajibika kufanya shughuli zote za nyumbani za usafi na upishi na papo hapo akiwajibika kuwa muangalizi wa watoto wadogo waliopo kwenye familia ya Otaibi akiwemo mtoto mchanga wa miezi minne ambaye aliitwa Kayed.


Kwa wiki kadhaa Rizana alichapa kazi pasipo kuwepo na mgogoro wowote na mabosi wake wala kuwepo kwa malalamiko kutoka upande wake.

Kazi ikaendelea, huku ndoto yake kichwani ya kuitoa familia yake katika umasikini uliokithiri ikizidi kuchanua kichwani mwake.




"Siku ya hatma, kiza hakichelewi"


Miezi miwili baada ya Rizana kuwa katika ajira, yaani siku ya tarehe 22 May 2005, Bw. Otaibi na mkewe waliondoka nyumbani asubuhi kama ilivyo ada.

Rizana naye aliendelea na shughuli zake kama kawaida ya siku zote.

Mnamo majira ya kama saa 6 na nusu mchana akaanza kumpatia maziwa mtoto mchanga Kayed ambaye naye alikuwa ni jukumu lake kama siku zote. Maziwa haya alikuwa anampatia kwa kutumia chupa ya watoto ya kunyonyeshea.

Akiwa anaendelea kumpa mtoto maziwa, alipokuona ameshiba akamuachia chupa achezee na kisha kwenda jikoni kuangalia maendelea ya chakula alichokuwa anapika. Ilimchukua dakika kadhaa akiwa jikoni, takribani dakika tano nzima na aliporejea alishapigwa na butwaa kumkuta mtoto mchanga Kayed chupa ameweka mdomoni kama anainyonya lakini amefumba macho.

Rizana akamuinua Kayed na kuanza kumfungua macho. Lakini kila akimfungua macho mara moja yanafunga tena. Lakini pia akagundua kuwa Kayed alikuwa hapumui.

Baada ya kumchunguza akagundua kwamba, Kayed alikuwa amebanwa pumzi (ame-suffocate) kutokana na kunyonya vibaya chuchu ya chupa ya maziwa na kusababisha kuziba koo la kupitisha hewa.

Kutokana na utoto wake (kumbuka ni binti wa miaka 17 tu) akaanza kulia na yeye papo hapo asijue afanye nini.


Watoto wengine wadogo wa familia ya Otaibi waliokuwa wanacheza chumba kinachofuata waliposikia kilio cha Rizana walikimbilia chumba hicho alichomo na kumkuta analia huku anampindua pindua mtoto na kujaribu kumuamsha Kayed.

Watoto hao nao wakabaki wamepigwa butwaa tu wasijue nini kinaendelea au wamsaidieje Rizana au Kayed.


Ghafla muda huo huo Mke wa Otaibi akarejea nyumbani na moja kwa moja akaelekea chumba ambacho alisikia kilio kinatoka huko tangu yuko getini.

Alipofika alimkuta Rizana amembeba Kayed mikononi huku analia. Mara moja mke wa Otaibi akamchukua Kayed kutoka mikononi mwa Rizana na mara tu baada ya kumgusa ndani ya sekunde chache aligundua kuwa mtoto mchanga Kayed ameshafariki.

Kama vile mbogo aliyejeruhiwa, Mke wa Otaibi alimrukia Rizana kwa hasira na kuanza kumshambulia huku akipiga yowe la kilio, akirudia neno moja tena na tena….

"KWANINI UMEMUUA MWANANGU..!!"




Itaendelea post inayofuata hapo chini...
 
Safi sana kwa kuleta huu Uzi.

Watu wanatakiwa wafunguke/wapate ufahamu na taarifa mbalimbali katika ulimwengu huu wa leo ambao ni digital.

Kama nyekundu ni nyekundu,,,nyeupe ni nyeupe tu.


Sent from my SM-J110H using JamiiForums mobile app
 
Wajinga na wauaji ndiyo wanashabikia vifo vya kuchinjwa binadamu kama kuku. Kesi zenyewe haziendeshwi kwa hski, mf. mzuri ni kesi ya Rizana, yule binti alionewa kabisa. Ila hakuwa na mtetesi akiwa katikati ya wapenda damu za watu in the name of religion. These are nothing but killers of innocent blood
Kwa mfululizo wa makala za huyu bwana tutajitahidi kusahihisha ufahamu kadri ambavyo patakua na upotoshaji ili kuitakasa sheria ya uislam iliyisalimika na mapungufu. Na hili si kwasababu yakuitetea Saudia kama Saudia bali kutetea yale wanayoyasimamia katika hukmu za mola wetu alizowahukumia waja wake.

Hukumu za uislam zilizofungama na adhabu ya kifo zipo nyingi mara nyingi hukumu hizo anahukumiwa nazo mwanaume au mwanamke ambaye tayari ameshafika baleghe, mwenye akili timamu, na pakiwepo na sura ya kukusudia kufanya hilo kosa litalomlazimu auwawe. Kwa hali hiyo ambao hawajafika baleghe na wasio na akili timamu hawatazingatiwa. Kwa wale waliofanya bila kukusudia nao wanamlolongo na taratibu zao.

Katika kesi iliyoletwa kuhusiana na huyu dada inaingia upande wa adhabu ya kifo kwa aliyeua moja kwa moja mf. Kwa kupiga risasi, kuchoma kisu n.k au aliesabisha kifo kwa mwingine(kwa kuweka sumu kwenye chakula/kinywaji, kutega mtego utaosababisha mtu kufa n.k.

Ufafanuzi upo kama ifuatavyo.
Kwanza sheria hii imetajwa katika
qur'an 17.33
"Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa."

Hapa tunaona imekatazwa kuuliwa nafsi isipokua kwa haki. Na haki hapa ya kuua moja wapo ni kisasi atacholipiziwa yule aliyeua nafsi. Na kisasi hiki kitasimamiwa/au kutekelezwa na mtawala.

Sheria imempata mrithi wa yule aliyeuliwa chaguzi baina ya kulipa kisasi kwa maana ya kutaka muuaji nae auliwe au asamehe kwa kupewa diya, au asamehe bila ya kupewa chochochote kwa hiyari yake iwe hakuombwa kusamehe au ameombwa. Hivyo basi hukumu hii itafatilizwa kwa matakwa ya warithi.
Kuna hekma kubwa sana imewekwa katika utekelezaji wa hukumu hii. Kwanza imetakiwa isimamiwe na mtawala ili usitokee utata baina ya familia mbili ikiwa familia ya warithi watachukua sheria mkononi. Pili utekelezaji wake una sura ya kutisha ili watu wengine wapate funzo na hofu ya kuua nafsi. Ikiwa sheria hii haikutekelezwa kuna uwezekano mkubwa wa muuaji kuendelea kufanywa na huyu muuwaji kwa kujua hakuna atalofanywa pia watu wengine watachukua mfano huo na wanaweza wakawaua wenziwao kwa kujua hakuna mtu atakae wachukulia sheria. Kwa hivyo kuna funzo kubwa kwa wengine na kwa hali hiyo hofu inapatikana kwa watu na uwoga wa kuua unaingia katika nyoyo zao hivyo kuzisalimisha damu za watu wengine ambazo zingemwagwa kwa tabia chafu ya kuuwana watu wao kwa wao.
Na kuhifadhi damu za watu ni lengo moja kati ya malengo ya sheria ya uislam.

Laiti ungejua uthibitishaji wa fulani kumua fulani ulivyo usingesema hayo. Mlolongo wake unafanywa kwa uadilifu mkubwa sana.
Pili ikiwa kuna uthibitisho wa uwongo umetolewa ili tu huyo dada auliwe basi aliyeongopa amebeba mzigo wake wa madhambi mpaka kiyama na atalipwa kwa hayo aliyoyafanya.
 
Umeongea point kwamba watawala wanatumia sheria za Quran kulinda viti vyao. Na mfano mkubwa ni Saudi Arabia chimbuko la uislamu! Wao wanatumia dini kukandamiza watu. Cha ajabu, waislamu wana support hizo hukumu kama ulivyosema "uzinzi, kuhama dini na mengi mengineyo ni capital punishment.

Kabisa! Hamna mtu anataka kwenda kwa waarabu maana hawachelewi kubadilikiana wenyewe na kubadilikia wageni pia! Nchi zao hazifai kabisa maana hamna uhuru wowote zaidi kwenda msikitini 24 hours kuomba kwa Allah ambaye hajibu sala za kuacha mauwaji na vita vyao visivyo kwisha.

Mpaka karne hii bado wanajiendesha na kuishi maisha ya kibedui ya kuchinjana chinjana eti Allah alisema! Tukisema ukweli kwa faida yao wanadai eti tunatukana dini na mtume wao.
Kuzungumza ili hali umetanguliwa na ujuzi ni jambo bora sana kuliko kuzungumza bila elimu yoyote. Na hakika hujui uislam unawazingatia vipi watawala. Dini haikandamizi mtu dini ina mpa kila mtu haki yake. Sisi tuliopita darasa za dini tunajua haki kubwa ya mtawala iliyojuu yetu ni kumtii madamu hajatuarisha kumuasi mola wetu. Sasa usichukizwe na watu waliokubali kua chini ya utii wa Mfalme ili mambo yao yatengemae. Utii unaofanywa na raia kwa mtawala unalinda damy za watu wengi sana lau ingetokea siku watoke katika utii wake na wamuasi(wafanye jaribio la kupindua) zitamwagika damu za watu wengi sana na mali pia zita angamia uhalisia ni kwamba maafa makubwa sana yatapatina. Kwa sababu hiyo sheria imewalazimisha waislamu kumtii mtawala wao ili kulinda hayo nilioweka hapo juu.
 
Mkuu, unajua uislamu unachanganya dini na utawala. Ukristo na mafundisho ya biblia hauwatakiwi kuchanganya dini na utawala. Inaweza ikahojiwa kwamba nchi zisizo za kiislamu zina ustaarabu kuliko nchi za waislamu.

Huwezi kuta nchi inajiita serikali ya kikristo au nchi ambayo inahukumu kwa sheria kutoka kwenye biblia! Yesu alifundisha wafuasi wake wasiwe moja ya serikali.

Serikali nyingi za waarabu au uislamu zinahusisha Quran kama kitabu cha sheria kwa kuchanganya dini na utawala. Quran inafundisha wanadamu kuwa makatili kwa kuchukua sheria mikononi mwao, huo ni mfano wa UUNGU MTU kwa Ufalme wa Saudia!

Kwa kweli inasikitisha sana binadamu wana enjoy kuona mwanadamu mwenzao kukatwa kichwa kama mbuzi mbele ya kadamnasi! Mimi sijui ustaarabu wa waarabu huko wapi ingawa neno "ustaarabu" ni neno lenye asili ya kiarabu!!? Imagine ustaarabu gani wa kunywa mkojo wa ngamia, wakati mkojo wake usababisha magonjwa lakini waarabu wanakunywa eti ni dawa! Nini sababu? kasema Mtume Muhammad!
Kama utanisaidia kuelezea jambo ntakutatulia kitendawili chako.
Elezea namna uislam unavyochanganya dini na utawala.
 
Raia wa nchi za mashariki ya kati yaani waarabu bado hawajazoea utawala wa democrasia.
Sadam Hussein alifanikiwa kutawala kwa mabavu ktk nchi ya Irak.
Muamal Gadafi naye alifanikiwa kutawala kidikteta nchini Libya.
Walipoondolewa kimabavu, nchi hizo hazijatengemaa hadi leo.
Hivyo ndicho kinachofanyika Saudi Arabia, Iran, Syria, Yemen nk.
Waarabu bado hawajazoea utawala wa vyama vingi.
Ndio maana watawala wa huko wanatumia mabavu, vitisho, sheria kali, adhabu kali ili kuweza kuwanyamazisha wapinzani wao kisiasa na kitamaduni.
Sadam hussein aliwaua sana wapinzani wake wa kisiasa, na nchi ikatulia.
Kwakuwa Msahafu unasheria kali basi watawala wa baadhi ya nchi za mashariki ya kati wanautumia kama msumeno wao wa kujilinda.
Hata iwe kwa heri au shari kumchinja mtu hadharani na jambia hakukubaliki kwa maisha ya kisasa.
Ni uvunjifu mkubwa wa haki za binadamu.
Sidhani kama utawala wa Sharia unakubalika na waislamu wote.
kwani kuna nchi zinawaislamu wengi lakini hazitumii amri za Sharia,
kama Zanzibar kabla ya Muungano.
Amri za Sharia kwa mimi kama mchambuzi huru naziona zimepitwa na wakati. kwasababu hazitoi nafasi ya mkosaji kuelimishwa ubaya wa kosa lake na hatimaye kuacha tabia yake mbaya.
Kwamfano
Wafungwa wa makosa ya wizi, huko jera pamoja na mambo mengine wanafudishwa tabia mjema, na kazi za ufundi, kilimo nk, ili kuweza kujitegemea.
Jambo hili hupelekea mfungwa kujirekebisha na hatimaye kuwa raia mwema badala ya kilema.
Huwa na uwezo wa kuzalisha mali, na kusaidia jamii yake.
Mfano mwingine,
Sharia inamhukumu kifo aliye badili dini kutoka Uislamu na kuwa muumini wa dini nyingine kama ya Kikristo, Kihindu nk.
Sasa hapo kuna tatizo gani wakati tendo la kuabudu ni la hiari na mtu anao uhuru wa kuabudu dini anayotaka. Mtu anaweza akawa mwislamu wa kurithi toka kwa wazazi, ukubwani inawezekana akaenda kusoma vyuo vyenye watu wa imani tofauti, huko wakamshawishi na akaona inafaa kwake kuwa muumini wa dini nyingine. Sasa hapo dhambi yake ninini hadi ahukumiwe kuchinjwa hadharani ?
Baadhi ya watawala wa nchi za mashariki ya kati wanatumia Sharia kama fimbo yao ya kuwaumiza na kuwatisha wapinzani wao,
Na kwakuwa raia wa nchi hizo wengi ni waislamu, wanashindwa kuikataa Sharia maana ipo kwenye kitabu chao cha dini wanayoiamini.
Kwao kukataa Sharia ni kama kukufuru, hivyo hawana cha kujitetea zaidi ya kuzikubali hata ikiwa kwa shingo ipande.

Ni uchambuzi wa kisiasa tu.

Ramadhan njema.
 
Nionavyo mimi kimsingi wenye chuki dhidi ya uislam kwanza hawataki kujua malengo ya uislam pia hawataki kukubali kua wao uislam hawaujui wao wanataka kulinganisha uislam na wazungu kitu ambacho hakiwiani kwasababu wazungu wao mambo yao wanajipangia wenyewe na siyo maagizo ya mamlaka fulani hata likifika suala la mamlaka huwa ni kule kuhalalisha mawazoyaotu lkns si uhalisia wa hayo mamlaka. lkn uislama hakuna mawazo ya watu bali ni mamlaka pekee ktk hilo watu nafasiyao ni kufanya uchambuzi wakina ili kujiridhisha kama wameelewa vizuli sasa ukitafuta iwiano wa mambo hayo kwa mawazo yalio beba chuki dhi ya kingine itakua ni shidatu ndiomaana mtu yupo tayari aropoketu wakati hana ushahidi kimaandishi wala hoja zake hazitokani na maandishi bali ni mawazo yaketu nawapeni pongezi sana nyie waalimu wakiislam mnaoweza kuelimisha watu wenye mtazamo wa chuki bila kutafuta usahihi wa jambo mungu awabariki sana mimi binafsi siwezi kujenga hoja na mtu ambae unaona kabisa hayupo kwa ajili ya kuelewa yeye yupo kwaajili ya kuhaributu mimi siezi hongereni sana.
 
Hufanyi uadilifu katika kuzunguma.
Huoni aibu kusema Allah ni the moon god.
Yani unaongopa mchana kweupu bahat mbaya sana hautaoata nafasi ya kuongopa kisha ukazingatiwa katika porojo zako.
Kwanza nisafishe hapa: ALLAH kwetu sisi ni mola muumbaji wa kila kitu, na yeye pekee ndie mwenye kustahiki kuabudiwa bila kushirikishwa.
Allah hajamuumba mwanaume sawa na mwanamke. Kila mtu anafahamu mwanaume na mwanamke hapo sawa kuanzia maumbile yenye kudhihirika mpaka yasiyodhihirika. Pia kumakinika katika mambo baina ya mwanaume na mwanamke ni tofauti na hayo ndo maumbile waliyoumbiwa.
Hivyo basi hata lilipokuja swala la sheria zao hawa wawili zinatofautiana na hapa ni kuonesha jinsi gani Allah ana hekma. Haikua sawa awatofautishe katika maumbile alowaumba nayo kisha katika maswala smya sheria na hukmu wafanane.
Pia hakuna swala la kusema wanawake wao ni wa kwenda motoni huu ni upotoshaji wa ajabu usio na maana. Msemaji hajui hata ameyatoa wapi maneno yake. Kiufupi amekurupuka.
Said una hakika hayo nilosema hayapo vitabuni mwenu?
1. nieleze/ueleze uwanja huu, kwanini kwenye misikiti yenu mmeweka alama ya NYOTA na MWEZI( a star & Crescent moon) na ni kwanini lazima mfunge na kufungua mpaka uonekane MWEZI?
2. Unaposema msemaji hajui hata ameyatoa wapi maneno yake, na amekurupuka!! je, mimi niliyeandika humu ama Muhammad ayesema hayo 1400yrs ago na wewe unamfuata ndiyo alikurupuka?
3. Je, ukipewa ref. utazikubali?
 
Kwanza kabisa namtakasa mola wangu kutokana na kua na hofu ya watu kuuhama uislam.
Ni kweli uislam haulazimishi mtu kuja katika uislam. Ikiwa mtu kachagua dini isiyokua uislam, uislam hauna shida nae.
Ila mtu anapokua katika uislam kisha akatoka huyu ni mwenye kufarakanisha watu(huyu amefanya usaliti mkubwa) na huenda akawa chanzo cha kufitini waislam wengine walitulizana katika dini.
Kwanza niseme mtu anapotoka katika uislam hukumu hii hamfatilizi papo kwa papo. Bali pamewekwa muda wa mtu huyu kulinganiwa kurudi katika dini na pindi atapokataa kurudi hukumu itafata mkondo. Pia hukumu hii haitekelezwi kiholela kwa maana watu tu wamtaani wachukue hatua, hii husimamiwa na mtawala wa waislam katika nchi husika. Wala wenye kuthibitisha mtu kutoka katika uislam sio mimi wala watu wengine wa mtaani tu ila wanakua ni wanazuoni wenye kutegemewa katika mas-ala ya dini(kutoa fatwa).
Sasa kwanini auliwe? ikiwa aliingia mwenyewe kwa hiyari yake na kutoka ni hiyari yake? kuna siri gani ndani Allah anaogopa mtu akiijua akiwa huko kwenye uislam kisha akatoka na hamsini zake. ikiwa kweli DINI ya allah ni njema ama inahubiri wema. hofu ya nini??

1. Umeanza na KUMTAKASA mola wako kutokana na kuwa na HOFU ya watu kuuhama uislam. mola wako ni wa aina gani mpaka awe na HOFU? na ahitaji msaada wa utakaso toka waumini wake?
 
Status
Not open for further replies.
Back
Top Bottom