Jamani, nimeona uchungu sijawahi upata tena maisha yangu yote. Kidogo tu nikufuru niseme "Hakuna Mungu" ila nimekosea. Mungu yupo na anaruhusu haya yatendeke ili hukumu yake itendeke.
Huwezi mchinja mwenzio ka kuku tena huku ukifurahia kilio chake cha mwisho cha kuomba msaada. Hivi, mtu kama huyu, ukimkunjia kwenye kona usiku bila hilo jambia, atakaa arudie tena kweli?? Nyie mnaotengeneza majini, si mmtengenezee jini limtishe usiku na hilo jambia lake mara 2 wadhani atathubutu tena kwenda chinja wengine??
Ameiharibu kabisa dini yangu ya amani.