Nadhani hii inakuwa na manufaa sana kwako sababu kama mtu alimuua ndugu yako kwa mateso au hawa wanaotoa kiungo cha binadamu (au hata rape) inaweza kuacha kovu la maisha kwa mtu ambalo ni mateso kuliko hata kifo..., nadhani watu kama hawa kupewa instant kifo inakuwa ni kama wameget off lightly
Binadam ni myama kama wanyama wengine. Tofauti yetu kubwa na wanyama ni kuwa tuna kitu cha ziada (Utu) yaani kutambua mazuri na mabaya, ambacho wenzetu hawana."Why do we Kill People who Kill People to Show that Killing People is Wrong ?"
Je ni sawa kuwa na Hukumu ya Kifo?
Baada ya yule Chizi wa Norway kuua kadamnasi ya watu (ukizingatia Norway life Sentence ni limited kwa miaka 21 tu) Je ni muhimu kuwa na hukumu ya kifo? Ni nini hasa faida ya hukumu ya kifo?
Je hukumu ya kifo inafanya watu waogope kutenda maovu kwahiyo ni njia nzuri au ni kuonyesha hata sisi hatuna tofauti na waliofanya hayo maovu?
I can argue kwamba huenda hukumu ya kifo ni adhabu rahisi sababu badala ya kumfanya mtu ku-suffer kwa kosa lake, tunampumzisha...Je sio vema kumfunga mtu maisha na kumfanyisha kazi ngumu kwa maisha yake yaliyobaki na kila alichonacho au atakachokitengeneza kiende kwa wale aliowatenda....
What do you think?.....
ni thahiri kua binadamu wa kawaida atafikiri km ww mi niongoze jambo moja biblia inasema ukiuwa kwa upanga nawe utauwawa kwa upanga hiyvo kuua kwa kusudia,kwa nia ovu(malice aforethought) ni sawa mtu kupewa athabu ya kifo cha msingi maadili ya sheria yazingatiwe ili kuwe na justice.Hii issue ni ngumu sana, mara nyingine huwa nakaa nafikiria naona kama adhabu ya kifo sio nzuri, kwa sababu mhusika anaponyongwa kimsingi waliodhurika na matendo yake hawapati chochote na yeye pengine anaweza asipate nafasi ya kujifunza na kujuta kwamba nilichokifanya hakikuwa sawa, lakini mara nyingine unafikiri unaona kuna watu akili zao ni mboovu na adhabu yao ni hiyo hamna kitu kingine, mfano majambazi wanaovamia na kuua labda familia nzima watu kama hao unadhani utawafanyaje?
Unamaanisha kwamba mtu akajisingizia mwenyewe kwamba ameuwa ili kumuokoa mtu mwingine? Kama kuna kesi kama hizo, ambazo ni nadra sana, kwa maslahi ya umma mimi sioni tatizo. Maana, hata kwenye vita kuna wapambe ambao wanaweza kujitokeza kukinga vifua vyao ili risasi isimpate kamanda au kiongozi wao wanaomlinda. Huwezi kusema askari wa upande mwingine wasubiri kwanza hadi huyu aliejitokeza aondoke.
Uwezekano mdogo kama huo upo pia hata katika makosa mengine yasiyohitaji adhabu ya kifo. Kwamba, mtu anaweza kufungwa maisha kwa kosa ambalo hakulifanya. Tukufuata maoni yako inabidi hata adhabu ya kifungo cha maisha au kifungo chochote isitolewe maana hamna uwezekano wa kuthibitisha mashitaka asilimia mia moja.