kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
Mataifa ambayo uchumi wao uko juu sana duniani wana adhabu katili sana kwa watu wao wanaobainika kuhujumu uchumi kunakosababisha mtu afikirie mara mbili kabla ya kuiba mali ya umma. Hapa kwetu adhabu ya kumtia mimba mtoto wa shule ni kubwa kuliko aliyeiba hela za umma kwa mabilioni. Nani katuroga?
Hapa kwetu eti Rais hata akituibia kiasi gani cha fedha eti hahojiwi, hashitakiwi wala kuguswa na yeyote, hivi ni nani ameturoga kwa uzuzu huu?
Adhabu zetu hizo ndio maana mtumishi wa TRA au Bandari haoni ni kwanini asijizolee pesa kabla hajaondolewa kwenye nafasi na kabla ya uzee haujamkuta, maana adhabu zenyewe zinavumilika kabisa.
Mataifa ya Uchina, Marekani, Asia na Ulaya kuiba mali ya umma hakuna kinga kwa yeyoye yule. Sisi hapa hatuko serious, hata anaeonekana kufoka sana kuhusu ufisadi anaigiza tu.