kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #41
Sasa hivi tunaandika humu kama mchezo lakini hakika maandishi yetu haya yatakuja kutafutwa kwenye archives ili yasomwe Na wajukuu wetu kama hatua mojawapo ya ukombozi wa taifa kiuchumi.
Ni heri ya anaetafuta wawekezaji kuliko anayetafuta misaada, hakuna cha bure ndugu zangu tuambine ukweli. Vya bure vina madhara, vina ndoana nyingi sana ambazo zitalinasa taifa kooni huko mbele ya safari, ni heri watoto Na wajukuu wetu wakute msululu wa orodha ndefu za majina ya watanzania wenzetu tuliowanyonga sisi wenyewe kwa makosa ya ufisadi, rushwa Na uzembe wa kuingia mikataba mibovu kuliko kukuta msululu wa watu Na mataifa wanaotudai. Watatudharau sana kama tunavyowabeza Leo akina Chief Mangungo wa Msovero dhidi ya akina Karl Peters.