kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #61
Katiba yetu imejengwa kwenye misingi ya kikaburu na udikiteta. Yaani ni katiba inayotegemea maadili mema, huruma, utashi na ucha Mungu wa kiongozi Mkuu. Mkipata kiongozi kichaa, kaburu, dikteta na shoga wananchi hawana la kufanya wala cha kufanya kumzuia na kumuondoa zaidi tu ya kuinua mikono yao juu kumuomba Mungu amuondoe mwenyewe kiongozi huyo kwa njia yoyote inayoifahamu yeye.Tunahitaji Katiba na muundo wa utawala wenye kuupa uwekezaji na biashara binafsi imani hadi ya miaka 50 mbele, tunahitaji mfumo wa uongozi unaotabirika sio matamko mapya kila kukicha, tunahitaji mfumo wa uongozi unaojitahidi kupunguza regulations, red tapes na kodi sio unaojitahidi na kujisifia kuongeza vitu hivyo.
Mfumo huo wa uongozi unahitaji kusimikwa juu ya katiba mpya iliyo thabiti na kuelekeza kwamba sisi ni taifa la kibepari. Bila hivyo mawazo ya Ujamaa na hodhi ya dola kwa chama kimoja vitaendelea kutufanya mafukara tunaoenda kwa mwendo wa Kobe.
Katiba hii inamfanya Kiongozi awaone wananchi kama wanyonge na sio mabosi wake anaopaswa kuwasikiliza wanachotaka.