kavulata
JF-Expert Member
- Aug 2, 2012
- 13,778
- 14,214
- Thread starter
- #101
Mtoto anajifunza kukomba mboga kutoka kwa mzazi wake, huwezi kuwa mzalendo kama viongozi sio wazalendo. Mimi huwa naangalia tamthilia ya Ertugul pale Azam two kila SAA 4 usiku. Wale jamaa wanaigiza historia ya kweli kuhusu Ottoman empire. Ertugul bay ndio viongozi wao, lakini anaishi maisha yanayofanana Na watu anaowaongoza, wezi Na wasaliti wanachinjwa baada ya kujiridhisha kuwa kweli wana makosa. Maisha kama Yale ndiyo waliyoyapitia watu weupe tangu enzi hizo hadi Leo hii, kila MTU anafahamu kitakachompata kama atatenda kosa lolote LA kiuhujumu Na makosa mengine. Hawana huruma wanachinja baada ya kuthibitika pasipo shaka kuwa umetenda kosa.Sio katiba mkuu, ni uzalendo mtakuja kugundua mzizi wa yote ni ukosefu wa uzalendo unaochagizwa na katiba mbovu.
Uzalendo unapelekea usimamizi thabiti na usimamizi thabiti unapelekea kufuata katiba kwa ukamilifu!
Mihimili mitatu yote ifanye kazi bila kuwa na muingiliano na Head of State. Ili kuwe na uwezekano wa kumuwajibisha head of state bila kuogopa kwamba ndio mwenyekiti wa chama ama atawafutia uanachama.
Pia head of state asiwe mwenyekiti wa chama wala kuwa na influence yeyote kwa wanachama. Hii itasaidia sana chama kiwe stand alone entity.
Separate body ya kuwawajibisha wanachama iwepo kulingana na katiba na asie tekeleza jukumu lake la kumuwajibisha mkosefu kwa mujibu wa katiba aidha kwa upendeleo au kwa namna yeyote ile aachie ngazi straight away anakuwa amejifukuzisha kazi within stated days!
Hapa kwetu wanaotuibia na kuuza madawa ya kulevya tunayo orodha yao vifuani mwetu, wanafahamika lakini watanzania wanashindwa kuwaondoa wala kuwaadhibu. Hali hii ni mpaka lini?