Mkuu 'Kalunya',
Kwa hiyo tufanyeje, tuikubali tu hali hiyo kuwa ndiyo kawaida?
Kwanza sikubaliani kabisa na mawazo yako haya. Wewe unasema "Wenzetu weupe wao utengeneza maisha ya Jamii nzima ifaidike..."
Unao uhakika kwamba huko nako hakuna majizi? Bila shaka hata hao wachina, mfano tunaoutumia hapa, nao unawaweka kwenye "wenzetu weupe", sasa huoni kwamba inawalazimu kuweka adhabu hizo za kifo katika taratibu zao kwa kujuwa kwamba wanalo tatizo kubwa upande huo?
Hao "wenzetu weupe" unaowasema, hata kama una maana ya wazungu, unaelewa sheria zao zinazobana mafisadi na wezi zilivyo nchini mwao; na zinatekelezwa?
Jibu lako ni aina ya majibu yale yale yanayotolewa humu jamvini na kwingineko, ni jibu la kivivu kabisa ambalo hukuchukuwa muda kufikiri juu yake.
Mimi ninaamini kwa dhati kabisa, kwamba inawezekana sana hata hapa kwetu kuondoa au hata kupunguza tatizo la ufisadi na wizi kama viongozi watakuwa na nia ya kuliondoa tatizo hilo.
Tatizo linalelewa na viongozi wenyewe waliomo serikalini. Hawa ndio tatizo.