Adhimisha kwa vitendo Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika

Adhimisha kwa vitendo Siku ya Kimataifa ya Mtoto wa Afrika

Lady Whistledown

JF-Expert Member
Joined
Aug 2, 2021
Posts
1,147
Reaction score
2,008
Siku hii ilianzishwa kama Kumbukumbu ya uasi uliotokea 16 Juni 1976 kwa Wanafunzi walioandamana kupinga Elimu Duni huko Soweto Nchini Afrika Kusini.

Maadhimisho ya Mwaka 2022 yanaangazia vitendo vya kikatili vinavyowakabili Watoto katika maisha yao ya kila siku, na tathmini ya hatua zilizofikiwa kuhakikisha Watoto wanalindwa.

Kama mtu mmoja mmoja kuna namna ambazo unaweza kusherehekea au kuadhimisha siku hii, zifuatazo ni mojawapo ya njia hizo.

Changia miradi au “Charity Events” inayojihusha na kusaidia watoto ikiwemo vituo vya kulelea watoto waishio katika mazingira duni au yatima kwa Msaada wa vyakula, vifaa vya shule au vifaa tiba.

Jitolee masaa machache ya kutembelea shule au vituo vya watoto, na tumia muda huo kuongea nao pamoja na kucheza nao.

Tumia muda kidogo kujifunza zaidi kuhusu changamoto zinazowakabili watoto ili kuwa sehemu ya ushiriki wenye kuleta mabadiliko katika kupambana na kutokomeza changamoto hizo.

Je, ni kwa namna gani unaweza na ungependa kuadhimisha siku hii?
 
Back
Top Bottom