Adolf Mkenda, Ndumbaro, Mwana FA wajiuzulu sakata la wanafunzi kuchezeshwa wimbo wa Zuchu 'Honey"

Adolf Mkenda, Ndumbaro, Mwana FA wajiuzulu sakata la wanafunzi kuchezeshwa wimbo wa Zuchu 'Honey"

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
15,835
Reaction score
23,776
Baada ya kipande cha video kinachowaonesha watoto wa shule za msingi wakicheza wimbo wa msanii Zuchu ‘Honey’ wilayani Tunduma kusambaa mitandaoni, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Adolf Mkenda ameagiza walimu wakuu wawili wa shule hizo wavuliwe vyeo.

Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum, Dkt. Dorothy Gwajima amempongeza Profesa Mkenda kwa kukemea kitendo hicho na kutoa wito kwa watoa huduma wote na wanaohudumia watoto kusimamia malezi na makuzi ya watoto.

MASIKITIKO: Mkenda anajichomoa betri kwa kufungia / na kushasha cheo mwalimu badala ya ku-deal na wimbo, unachezwa na watoto na watu wazima harusini.

Nani aliyeema wimbo ni mbaya kwa watoto lakini wimbo huo huo hao watoto wakikua unakuwa mzuri?

Wimbo unao hamasisha kufir*** na ngono isiyo salama ni mbaya kwa watoto na mzuri kwa watu wazima?
MWANA FA yeye yupo Wizarani amekaa kimya haoni wala hasemi lolote kwakuwa ni washkaji zake.​

NB: NDUMBARO, MWANA FA hamtoshei, yaani Katibu mkuu wa Wizara anawafunika sema basi tu, mtu kwa kubebwa bebwa.

DIAMOND, ZUCHU, HARMO na wengineo wanaimba nyimbo zinazohamasisha ngono, mapenzi ya jinsia moja na madawa/shisha huku zikichezwa hata kwenye sherehe ambazo watoto wapo, BASATA wapo, na wanyonge wapo.​

#Acheni unafki BASATA ifumuliwe pale hamna kitu.

Pia soma >Tunduma: Wakuu wa shule wavuliwa nyadhifa kisa wimbo wa Zuchu (Honey)

Waziri anakuwepo huko maporini kwenu mkivunja maadili? Viongozi wakuu huwa hawako huko maporini kwenu huko

Mkenda yuko vizuri ila nilimdharau mno alipoituhumu bodi ya mikopo.kwa maslahi yake vitu visivyokuwepo na alipobanwa na bunge akajitia ohh sijui mimi sikusema hovyo sana kwenye lile swala la bodi ya mikopo. Walimbana athibitishe kamati ya bunge ikaundwa hadi tume akaruka utafikiri kibaka wa uswahilini kuwa ohh mimi sikusema tena mbele ya bunge alivyo mjinga.

Kumbe ubinafsi alitaka watu wake wapate mikopo OK kuna mengi pale yalimfanya aufyate anyamaze kimya.lakini noted somewhere.

Pamoja na kuruka maili mia ile kitu ilikuwa noted.

Otherwise yuko vizuri.
 
Hapa mtaani kwetu watoto wanauimba na kucheza hadi aibu. Hivyo kujifanya kuzuia mashuleni wakati mtaani watoto ndio wimbo wanaucheza sidhani kama itasaidia.

Kwa nini usipigwe marufuku wimbo? Wimbo wenyewe unajitangaza maudhui yake.

Kuna nyimbo zinaibwa mitaani utakuta bodaboda wanashikana matako.
 
Serikali ipige marufuku muziki mashuleni au sehemu yoyote yenye watoto. Kama ni muziki basi ziwekwe nyimbo za uzalendo na kulisifia taifa.
 
Salam atawapa mama Samia nanyi mtajibu kazi iendelee.

Kuna matamko nimesikia yametolewa yakiwataka walimu wakuu kushushwa vyeo. Naomba walimu hao waachweeeee na wasiguswe Kwa lolote. Ninaowatemea nyongo ni Hawa wafuatao.
1: Mtoa tamko, sijui ni waziri wa elimu au wajinsia wanajuana wenyewe lakini alietoa tamko ni mshamba. Hivi kwenye Ile video umeona Kama Kuna makosa yakinidhamu yamefanyika? Na je katika wizara Yako Hilo ni jambo kubwa kuliko Mambo mengine yote? Ile video inaonesha ni Kama walikua kwenye hafla au sherehe na walikua mwishoni, kilichofanya useme wakuu washushwe vyeo ni Nini? Wimbo?, Wanafunzi kucheza na kuimba!, Walimu kufurahi na watoto! Au ulevi wa madaraka. Kama ni wimbo watoto wanaufahamu na walikua wakiimba na waliufurahia, walimu pia walifurahi sometimes stress zetu walimu hupungua Kwa kuona watoto wamefurahi.

2: Mpiga picha. Kwenye video hiyo mpiga picha alikuwepo na alilipwa na shule au kamati kurekodi matukio mhimu lakini Kuna kimtu kimetumia Tecno yake na kujifanya kupost. Ninaamini kabisa alietupia video ni mwalimu Tena alikua mbele ya huyo mwalimu wakike. Nauliza Hivi , ni kitu gani kilifanya arekodi na kupost bila kupima faida na hasara? Sasa umepost umepata Nini? Hivi tukisema Kila mwalimu apost wanachokifanya shuleni kwaoau kwenye sherehe zao mitandaoni kutakalika? Acheni ulimbukeni ndugu zanguni.

Niombe mawaziri waache walimu wachape kazi na aliepost video ashughulikiwe. Kwenye sherehe za shule huwa yanafanyika mengi yasiyo na maadili ila ndio wakati wenyewe tulionao. Kuna maonesho ya mitindo, kusheki, kudensi nyimbo za kizazi kipya, maigizo n.k lakini huishia ndani na maisha yanasonga. Watoto wa saizi wanaangalia mengi majumbani na Wala walimu hatuna la kubadili katika hili.

********* WAKATI UKUTA ********
 
Serikali ipige marufuku muziki mashuleni au sehemu yoyote yenye watoto. Kama ni muziki basi ziwekwe nyimbo za uzalendo na kulisifia taifa.
Wewe hapa akili zako kama za Mkenda kwa mujibu wa mtoa uzi.

So zipigwe marufuku shuleni huku mtaani zinaimbwa na kucheza na kwa ujuha unadhani watoto walioko shuleni ni tofauti na walioko mtaani

Dawa piga marufuku nyimbo za kijinga
 
Miziki ya sahvi wanaimba kuhusu dushes,ku0713 mwanzo mwisho

Ova
 
Kuna channel moja ya TV, tena ni maarufu hapa nchini kuna siku huwa wanavionyesha vitoto vikikata viuno kwa nyimbo zisizoeleweka vikionyesha vipaji. Mbona hatujasikia kelele huko? Watoto wa mtaani ndio haohao wanafunzi.
Kifupi ni kupiga marufuku nyimbo zinazohamasisha ngono.
 
mkuu, Wakijiuzulu wewe utanufaika nini??
Watu weusi huwa wana husda, wivu, roho mbaya na uchawi, huo wimbo watoto unawaathiri nini walimu kuburudika na watoto ni kosa, wasipoimba shuleni watauimba majumbani, akili za watu weusi hasa wabongo huwa wanawaza ngono tu muda wote.
 
Salam atawapa mama Samia nanyi mtajibu kazi iendelee.

Kuna matamko nimesikia yametolewa yakiwataka walimu wakuu kushushwa vyeo. Naomba walimu hao waachweeeee na wasiguswe Kwa lolote. Ninaowatemea nyongo ni Hawa wafuatao.
1: Mtoa tamko, sijui ni waziri wa elimu au wajinsia wanajuana wenyewe lakini alietoa tamko ni mshamba. Hivi kwenye Ile video umeona Kama Kuna makosa yakinidhamu yamefanyika? Na je katika wizara Yako Hilo ni jambo kubwa kuliko Mambo mengine yote? Ile video inaonesha ni Kama walikua kwenye hafla au sherehe na walikua mwishoni, kilichofanya useme wakuu washushwe vyeo ni Nini? Wimbo?, Wanafunzi kucheza na kuimba!, Walimu kufurahi na watoto! Au ulevi wa madaraka. Kama ni wimbo watoto wanaufahamu na walikua wakiimba na waliufurahia, walimu pia walifurahi sometimes stress zetu walimu hupungua Kwa kuona watoto wamefurahi.

2: Mpiga picha. Kwenye video hiyo mpiga picha alikuwepo na alilipwa na shule au kamati kurekodi matukio mhimu lakini Kuna kimtu kimetumia Tecno yake na kujifanya kupost. Ninaamini kabisa alietupia video ni mwalimu Tena alikua mbele ya huyo mwalimu wakike. Nauliza Hivi , ni kitu gani kilifanya arekodi na kupost bila kupima faida na hasara? Sasa umepost umepata Nini? Hivi tukisema Kila mwalimu apost wanachokifanya shuleni kwaoau kwenye sherehe zao mitandaoni kutakalika? Acheni ulimbukeni ndugu zanguni.

Niombe mawaziri waache walimu wachape kazi na aliepost video ashughulikiwe. Kwenye sherehe za shule huwa yanafanyika mengi yasiyo na maadili ila ndio wakati wenyewe tulionao. Kuna maonesho ya mitindo, kusheki, kudensi nyimbo za kizazi kipya, maigizo n.k lakini huishia ndani na maisha yanasonga. Watoto wa saizi wanaangalia mengi majumbani na Wala walimu hatuna la kubadili katika hili.

********* WAKATI UKUTA ********
ila lile vibe la vile vitoto nimelipenda. vitoto vilishaharibika toka makwao ,vinaimba utafikiri ndo vitunzi
 
Yaani mimi sijaona tatizo hapo sema wabongo tunapenda kukuza mambo. Sie wenyewe mashuleni tulikua tunaimbishwa nyimbo na kufundishwa kukatika viuno, kucheza ngoma kwenye somo la utamaduni mbona tumekuwa watu wema tu? Its ok for kids to have fun bana. Stress zimezidi sana, afya ya akili inaenda mrama, wakipata nafasi ya kufurahi na waalimu wao acha wafurahi. Shule sio jela
 
Back
Top Bottom