Mag3
Platinum Member
- May 31, 2008
- 13,413
- 23,592
Nakiri kuwa sijawahi kuishabikia CCM hata kwa bahati mbaya. CCM ni chafu na inanuka. Siwezi kuishi kwenye nyumba inayonuka, nikijifunika blanketi moja na wanaonuka, nikikesha na wenzangu wanaonuka halafu nidanganye umma kwamba sinuki. Kuwa mwanachama wa CCM maana yake ni kwamba huo uvundo haukusumbui, unauona kama marashi ya Pemba.
Kuwa mwanachama wa CCM ni hatua ya kwanza katika kulisaliti taifa kwa kukubaliana na tulipokuwa, tulipo na tunakoelekea. Hata mwenyekiti muasisi wa CCM, Baba wa Taifa, alishindwa kuvumilia huo uvundo na kutishia kujitoa kama juhudi za makusudi hazikufanyika kukisafisha chama kilichoonekana wazi kabisa kukosa dira lakini masikini, hata yeye akapotezwa?
Niliipinga CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi, nikaendelea kuipinga baada ya mfumo mpya na nitaendelea kuipinga hadi itoke madarakani. Hii ni kwa sababu ninaamini kwa dhati kabisa kwamba chama ambacho kwa muda zaidi ya nusu karne haikuweza kutuopoa katika lindi la ujinga, maradhi na umasikini, imechoka, imezeeka na haina uhalali wowote wa kubaki madarakani.
CCM inaamini katika kuhodhi kila kitu…kuhodhi uhai, kuhodhi nchi, kuhodhi uraia, kuhodhi Katiba, kuhodhi utawala, kuhodhi haki (mahakama), kuhodhi madaraka, kuhodhi fikra, kuhodhi hoja (bunge), kuhodhi akili na kuhodhi hata ujinga! Naam, ukianza kuhodhi kila kitu, umekuwa sawa na kokoro na si ajabu kuhodhi hadi ujinga! Angalia ilipofikia CCM imehodhi hadi ulevi wa madaraka!
Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli akaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu, hata hivyo la kuvunda halina ubani na mwisho wake hauko mbali.