Adui hatari nambari wani wa taifa letu Tanzania ni CCM, je unaafiki?

Adui hatari nambari wani wa taifa letu Tanzania ni CCM, je unaafiki?

Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli kaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu...hata hivyo la kuvunda halina ubani!View attachment 1920398

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Laana hii
 
Hata sijasoma japo nimesoma kichwa cha hbr.
Wala sishangai, huwezi kwani juhudi kubwa inahitajika na kwa mwana CCM hata kumudu kusoma kichwa lazima umeteseka kweli kweli!
Adui ni wewe mwenye mawazo mgando,vyama havisaidii chochote kwa mahala popote,adui ni mtu mvivu anaye chagua cha kufanya
Mwana CCM kindandaki G'taxi, ndipo uwezo wako ulipofikia baada ya akili kuathirika kwa kuishi kwenye nyumba yenye uvundo. Fungua angalau dirisha uonje harufu ya hewa safi!
 
%100 ccm ni adui namba moja wa hii nchi, ndio mana hata wanapopeana madaraka kila mmoja anaingia na yake,tunapozungumzia CCM ni pamoja na police
 
Ila tunakoelekea nadhani itabidi jwtz (tpdf) jeshi la wananchi wa Tanzania) liingilie Kati dhulma ya polisi na ccm dhidi ya watanzania.
Hao ni zao la CCM. Wametengenezwa walivyo na ndiyo maana ni wakuu wa mikoa, wilaya, wakurugenzi, Makatibu tawala, n. K, n.k.
 
Binafsi Naona mtazunguka Sana mfumo wetu wa utawala na kifikra wa UJAMAA ndio uliotufikisha hapa

Ujamaa umetufanya tuwe waoga tushindwe kuhoji na Kama ukihoji bas utahoji ukiwa chumban kwako au mtandaon kwa fake ID ili usijulikane kuogopa mkono was dola hiz zote n athari za ujamaa ambazo zmetufanya tuwe waoga wa kila kitu

Wachache wakijitokeza kuhoji juu ya utendaji mbovu wa serikali wanaoonekana wasaliti wasioipenda nchi na hata support wanayoipata n chache Sana toka kwa raia hii yote sababu ya hofu kutokana na mifumo

Mungu awabariki hata hawa wachache wanaojaribu kupigania demokrasia katika nchi yetu naamin ipo siku mwanga tutauona

WATANZANIA N WAZURI KUONGEA MDOMONI LAKN VITENDO N HOVYOOO USIMTEGEMEE MTANZANIA KATIKA JAMBO LA KUPIGANIA DEMOKRASIA YA WOTE

lakn MTANZANIA huyo huyo akiguswa maslah yake anataka wote tumsaidie ili apate haki yake

Sent from my TECNO F1 using JamiiForums mobile app
 
Naunga mkono hoja. Hongera Sana Mkuu Kwa uchambuzi wako uliotukuka.

Hivi sasa wameanza kubaguana wenyewe Kwa wenyewe. Mf kwenye sakata la Gwajiboy mmewaona watoa hoja walivyofika mbali Kwa kusema eti Gwaji hakuwa mwanachama wa CCM Bali wa Magu. Ni wazi kuwa hawana tena mbinu za kupambana na wale wasiowapenda.

Ukizoea Kula nyama za watu kamwe hotoiacha, by Mwl. Nyerere.
 
Siyo Magufuli tena?

Mimi nilifikiri mbaya wetu hii nchi ni Magufuli, na hata zile shangwe za wana chadema baada ya kifo chake nilifikiri sasa mtajiona mko Newyork!

Mmakwama wapi mabavicha?
Nyoka akiwa mrefu hujikuta akigonga mkia wake mwenyewe akidhani ni adui. Endelea na kejeli zako lkn iko siku utarudi humu JF Kwa ID mpya kuishambulia Chama chako chakavu baada ya kukujeruhi.
 
Chama dola,sasa bora wangekuwa kama ccp ya china wawe na vitengo competent kwenye idara mbalimbali na ziweze kuja na suluhu ya matatizo unfortunately hapo ndio hakuna kuna wachumia tumbo na waganga njaa.
 
Hata sijasoma japo nimesoma kichwa cha hbr.

Adui ni wewe mwenye mawazo mgando,vyama havisaidii chochote kwa mahala popote,adui ni mtu mvivu anaye chagua cha kufanya
Wewe yawezekana ni mvivu wa kusoma yawezekana hata shule hukumaliza Kwa uvivu wako. Ndiyo maana unatumia nguvu hata pale pasipohitajika badala ya akili.
 
Nakiri kuwa sijawahi kuishabikia CCM hata kwa bahati mbaya. CCM ni chafu na inanuka. Siwezi kuishi kwenye nyumba inayonuka, nikijifunika blanketi moja na wanaonuka, nikikesha na wenzangu wanaonuka halafu nidanganye watu kwamba sinuki. Kuwa mwanachama wa CCM maana yake ni kwamba huo uvundo haukusumbui, unauona kama marashi ya Pemba.

Kuwa mwanachama wa CCM ni hatua ya kwanza katika kulisaliti taifa kwa kukubaliana na tulipokuwa, tulipo na tunakoelekea. Hata mwenyekiti muasisi wa CCM, Baba wa Taifa, alishindwa kuvumilia huo uvundo na kutishia kujitoa kama juhudi za makusudi hazikufanyika kukisafisha chama kilichoonekana wazi kabisa kukosa dira lakini masikini, hata yeye akapotezwa!

Niliipinga CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi, nikaendelea kuipinga baada ya mfumo mpya na nitaendelea kuipinga hadi itoke madarakani. Hii ni kwa sababu ninaamini kwa dhati kwamba chama ambacho kwa muda zaidi ya nusu karne haikuweza kutuopoa katika lindi la ujinga, maradhi na umasikini, imechoka, imezeeka na haina uhalali wowote wa kubaki madarakani.

CCM inaamini katika kuhodhi kila kitu kuhodhi nchi, kuhodhi uraia, kuhodhi Katiba, kuhodhi utawala, kuhodhi haki (mahakama), kuhodhi madaraka, kuhodhi fikra, kuhodhi hoja (bunge), kuhodhi akili, kuhodhi uhai na kuhodhi hata ujinga! Naam, ukianza kuhodhi kila kitu, umekuwa sawa na kokoro na si ajabu kuhodhi hadi ujinga! Angalia ilipofikia CCM imehodhi hadi ulevi wa madaraka!

Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli kaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu, hata hivyo la kuvunda halina ubani na mwisho wake hauko mbali.
Tusubiri WaTZ waelimike na kufunguka akili kama Kijana wa Salender alivyowakilisha kuchoshwa na ukandamizaji.
 
Sasa inakuwaje mnabadirika badirika kama vinyonga?
Mnabadirika badirika ni mdudu gani ndugu yangu au ni yale yale ya nireteeni Gwajima! Je una undugu na mwendakuzimu? Lakini kama ulitaka kusema nabadilika badilika, naomba nikukumbushe kidogo...

Toka siku ya kwanza nilipojiunga na Jamii Forums mwaka 2008 nilisema kuwa adui mkubwa wa taifa hili ni CCM. Leo miaka 13 toka nijiunge bado narudia kuwa adui nambari wani wa taifa ni CCM...hata siku moja sijabadilika.
Yule anasema adui ni ccm, wengine adui alikuwa Magu,
Mwendakuzimu ndiye aliyevaa sura halisi ya CCM labda kupita waliomtangulia. Alihodhi kila kitu hadi uhai wa Watanzania. Alikuwa mchezaji, mshika kibendera na mwamuzi vyote kwa pamoja. Watu waliishi kwa huruma zake na ole wako utofautiane naye, hatma yako ilikuwa mikononi mwake.
Tuelewe lipi?
Bahati mbaya huwezi kuelewa chochote hata ukikutana nacho uso kwa uso. Uvundo wa CCM umekulemaza.
 
Back
Top Bottom