Adui hatari nambari wani wa taifa letu Tanzania ni CCM, je unaafiki?

Adui hatari nambari wani wa taifa letu Tanzania ni CCM, je unaafiki?

Nakiri kuwa sijawahi kuishabikia CCM hata kwa bahati mbaya. CCM ni chafu na inanuka. Siwezi kuishi kwenye nyumba inayonuka, nikijifunika blanketi moja na wanaonuka, nikikesha na wenzangu wanaonuka halafu nidanganye watu kwamba sinuki. Kuwa mwanachama wa CCM maana yake ni kwamba huo uvundo haukusumbui, unauona kama marashi ya Pemba.

Kuwa mwanachama wa CCM ni hatua ya kwanza katika kulisaliti taifa kwa kukubaliana na tulipokuwa, tulipo na tunakoelekea. Hata mwenyekiti muasisi wa CCM, Baba wa Taifa, alishindwa kuvumilia huo uvundo na kutishia kujitoa kama juhudi za makusudi hazikufanyika kukisafisha chama kilichoonekana wazi kabisa kukosa dira lakini masikini, hata yeye akapotezwa!

Niliipinga CCM kabla ya mfumo wa vyama vingi, nikaendelea kuipinga baada ya mfumo mpya na nitaendelea kuipinga hadi itoke madarakani. Hii ni kwa sababu ninaamini kwa dhati kwamba chama ambacho kwa muda zaidi ya nusu karne haikuweza kutuopoa katika lindi la ujinga, maradhi na umasikini, imechoka, imezeeka na haina uhalali wowote wa kubaki madarakani.

CCM inaamini katika kuhodhi kila kitu kuhodhi nchi, kuhodhi uraia, kuhodhi Katiba, kuhodhi utawala, kuhodhi haki (mahakama), kuhodhi madaraka, kuhodhi fikra, kuhodhi hoja (bunge), kuhodhi akili, kuhodhi uhai na kuhodhi hata ujinga! Naam, ukianza kuhodhi kila kitu, umekuwa sawa na kokoro na si ajabu kuhodhi hadi ujinga! Angalia ilipofikia CCM imehodhi hadi ulevi wa madaraka!

Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli kaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu, hata hivyo la kuvunda halina ubani na mwisho wake hauko mbali.
Wazii..
 
Upo sahihi kwa asilimia mia moja (100%).
CCM ni chanzo cha kila uovu.
 
True rejea maakubaliano yao na shetani mapangoni bagamoyo umasikini ni moja masharti.

CCM ni iwafanye watz masikini ili itawale. Pasipo umasikini CCM itakufa.

na ndiyo maana kundi kubwa la watu wanaoipenda ccm ni kutoka ktk mikoa masikini
 
Siyo Magufuli tena?

Mimi nilifikiri mbaya wetu hii nchi ni Magufuli, na hata zile shangwe za wana chadema baada ya kifo chake nilifikiri sasa mtajiona mko Newyork!

Mmakwama wapi mabavicha?

unazini kila anaepinga ccm ni bavicha tupo tusio na chama na tunaipinga ccm
 
Sasa chama kiingie mkataba na Shetani na limwenge Lao halafu waipende hii nchi!! Tangu lini shetani akawa na mahaba na watu??
 
Naafiki chama Cha majambazi kwa sets zao mbovu ndo adui was taifa Hilo.
 
na ndiyo maana kundi kubwa la watu wanaoipenda ccm ni kutoka ktk mikoa masikini
Na mtaji mkubwa wa CCM ni ujinga. CCM haitaki watu waelimike kwa sababu wakielimika hawatakubali tena mambo ya kijinga. Ujinga na umasikini ni kama pete na kidole.
 
Hata sijasoma japo nimesoma kichwa cha habari.

Adui ni wewe mwenye mawazo mgando, vyama havisaidii chochote kwa mahala popote,adui ni mtu mvivu anaye chagua cha kufanya
Kweli wewe ni zumbukuku wa mambo ya siasa
 
Hata sijasoma japo nimesoma kichwa cha habari.

Adui ni wewe mwenye mawazo mgando, vyama havisaidii chochote kwa mahala popote,adui ni mtu mvivu anaye chagua cha kufanya
Ccm ni adui nambari moko kwa ustawi wa mtanzania
 
Hakuna uongozi umetokea kwa Bahati mbaya dunia,nimekuja kuamini Hivyo hivi majuzi. Mungu karuhusu ccm itawale ili watanzania tuujue upumbavu wetu.
Mungu hata shusha Akina Elia ama Isaya ili kutuambia watanzania kuwa ni wapumbavu, bali anatumia ccm kutuambia na kutuonyesha upumbavu wetu. Dunia inajua kuhusu ilo, hata yule mkenya aliwai sema ( magufuli RIP) anaswaga ng'ombe M 60..
Adui mkubwa wa Tanzania sio CCM, ADUI wa Tanzania ni upumbavu wa watanzania wenyewe,ccm wametake advantages tu kupitia HAKO kagep ndiyo Maana ni wachungu kweli hawana ladhi na mtu yoyote atakae jaribu kuwaamsha ng'ombe wao.
Ukiwashinda kwa hoja, watakutungia kashfa, kashfa ikishindwa Wanatumia polisi kukudhoofisha, polisi na mahakama wakishindwa wasiohulikana wanaingia mzigoni.
 
unazini kila anaepinga ccm ni bavicha tupo tusio na chama na tunaipinga ccm
Wasamehe hao, ndivyo wanavyokaririshwa kwenye hilo jumba linalonuka.
 
Mwinyi aliingia na yake, Mkapa akaingia na yake, Kikwete akaingia na yake, Magufuli kaingia na yake na sasa Mama naye kaingia na yake lakini washiriki bado ni wale wale na nyumba inayonuka bado ni ile ile. Baada ya kupoteza mvuto kwa wananchi, ikaamua kung'ang'ania madaraka kwa ulaghai na matumizi ya nguvu...hata hivyo la kuvunda halina ubani!

View attachment 1920398

Sent from my Infinix X692 using JamiiForums mobile app
Umenena mkuu
 
unazini kila anaepinga ccm ni bavicha tupo tusio na chama na tunaipinga ccm
Nmekuzini lini?

Mibavicha hamjifichi wewe!

Mwanzo mlifikiri matatizo yenu ni sababu ya Magu na alipofariki makashangilia.

Taratibu mtapata akili tu
 
Mnabadirika badirika ni mdudu gani ndugu yangu au ni yale yale ya nireteeni Gwajima! Je una undugu na mwendakuzimu? Lakini kama ulitaka kusema nabadilika badilika, naomba nikukumbushe kidogo...

Toka siku ya kwanza nilipojiunga na Jamii Forums mwaka 2008 nilisema kuwa adui mkubwa wa taifa hili ni CCM. Leo miaka 13 toka nijiunge bado narudia kuwa adui nambari wani wa taifa ni CCM...hata siku moja sijabadilika.

Mwendakuzimu ndiye aliyevaa sura halisi ya CCM labda kupita waliomtangulia. Alihodhi kila kitu hadi uhai wa Watanzania. Alikuwa mchezaji, mshika kibendera na mwamuzi vyote kwa pamoja. Watu waliishi kwa huruma zake na ole wako utofautiane naye, hatma yako ilikuwa mikononi mwake.

Bahati mbaya huwezi kuelewa chochote hata ukikutana nacho uso kwa uso. Uvundo wa CCM umekulemaza.
Kwa hiyo wewe una akili tofauti na hawa mibavicha wa humu?
.
Kama ni ndiyo, wewe unatoka katika bavicha ipi?

Huyo mwendakuzimu ndio nani?
 
Nyoka akiwa mrefu hujikuta akigonga mkia wake mwenyewe akidhani ni adui. Endelea na kejeli zako lkn iko siku utarudi humu JF Kwa ID mpya kuishambulia Chama chako chakavu baada ya kukujeruhi.
Kwani sasa hivi bado mnajeruhiwa?

Si aliekuwa anawajeruhi alishakufa?

Sasa hivi mnapumua, mko huru, maisha mazuri.!
 
Nmekuzini lini?

Mibavicha hamjifichi wewe!

Mwanzo mlifikiri matatizo yenu ni sababu ya Magu na alipofariki makashangilia.

Taratibu mtapata akili tu

chanzo cha matatizo ni ccm alafu kwani kuna ubaya watu kushangilia kifo cha meko hii nichi huru kila mtu anahaki ya kufanya anacho jisikia hii mradi havunji sheria, meko alikuwa janga la taifa, ilikuwa lazima tushangilie tu,
 
Akikuwa janga na amekufa mkashangilia!

Maksema sasa mko huru, mnapumua, mama anaupiga mwingi, maisha mazuri sanaaaaa!

Bado mnalalamika tena?
 
Akikuwa janga na amekufa mkashangilia!

Maksema sasa mko huru, mnapumua, mama anaupiga mwingi, maisha mazuri sanaaaaa!

Bado mnalalamika tena?

hakika kifo cha meko ilikuwa furaha kubwa,
 
Back
Top Bottom