Adui hatari nambari wani wa taifa letu Tanzania ni CCM, je unaafiki?

Hoja hii imeungwa mkono.

Everyday is Saturday............................... 😎
 
Hoja imekubaliwa. Ipo siku CCM nayo itaingia kwenye dampo la historia
 
Upuuzi wa chadema ni kubrainwash vijana kwamba wao ni wapigania haki wakati wengi wao ni wapigania tumbo.
Kaka pembe, hebu ongezea nyama kidogo, ni kwa namna gani Chadema hawapiganii haki na badala yake wanapigania tumbo?

Unaweza kuwataja hao Chadema wanaopigania tumbo na namna wanayotekeleza harakati hizo za kupigania tumbo? Ninavyosikia hawaruhusiwi hata kukutana na wakijaribu, polisi huwakamata, kuwatupa selo na kuwafungulia mashtaka!

Mwagika tu ndugu yangu, hii ni JF tunapomkoma nyani ngeledi bila kumtazama uso. Hiyo nafasi ya kupigania tumbo wanaipataje huko korokoroni?
 
wabongo nimewanyooshea mikono
 
Mkuu 'Mag3', wahenga husema kulitambua tatizo ni mwanzo wa ufumbuzi wa tatizo hilo.

Ni mara nyingi sana nimepiga kelele nyingi humu JF, watu watambue adui hasa wa nchi yetu kwa wakati huu ni nani, lakini watu ni wazito sana kuondoa mawazo yao kwa watu, kama mwenyekiti wa chama hicho kuwa ndiye adui yao mkubwa, wanasahau kwamba ni chama anachoongoza ndiye adui mkubwa wa taifa letu. Tofauti hapa atakuwa Magufuli, kwa sababu wakati wake Magufuli ndiye alikuwa CCM na CCM ikawa ndiye Magufuli.

Kwa hiyo ukitaka kuleta mabadiliko, ni lazima utambue ni nani hasa unayehitajika kupambana naye ili upate mafanikio unayotafuta.

Kwa hiyo, sasa tukitambua kwamba CCM ndiye adui, ni lazima tujue ndani ya CCM hiyo, ni watu gani hasa wanaoshikilia na kuendesha chama hicho kiendelee kutuletea madhara. Kuna kundi maalum, ndani ya chama hicho, kundi la watu wasiosikika wala kuonekana jinsi wanavyokiendesha chama hicho kuendelea kuleta maumivu kwa wananchi. Watu hawa hawasiskiki lakini matendo yao ndiyo yanayoleta matokeo tunayoyaona.

Ni watu hawa ndio wanaong'ang'ania pasiwepo na katiba mpya na mambo mengine yasiyoliletea tija taifa letu. Mwenyekiti anacgukua maamuzi yao na kuyatangaza. Ndiyo maana wengi hudhani mwenyekiti ndiyye mwamuzi ya haya mambo yote.

Kwa hiyo basi, katika kutafuta mbinu za kupambana na adui huyu, ni lazima kuwatambua hawa watu wachache walioko huko ndani ya CCM. Watu hawa inatakiwa wajulkikane kwa wananchi kuwa ndio kikwazo kikubwa katika mabadiliko yanayohitajika. Watu kama Mizengo Pinda, ndio wanaoishikilia CCM iendelee kuleta madhara makubwa kwa nchi yetu.
 
Siyo Magufuli tena?

Mimi nilifikiri mbaya wetu hii nchi ni Magufuli, na hata zile shangwe za wana chadema baada ya kifo chake nilifikiri sasa mtajiona mko Newyork!

Mmakwama wapi mabavicha?
Wakati wake CCM haikuwepo. Kwa hiyo isingewezekana kuilaumu CCM badala ya kumlaumu Magufuli ambaye aliitwaa CCM.
 
Hata sijasoma japo nimesoma kichwa cha habari.

Adui ni wewe mwenye mawazo mgando, vyama havisaidii chochote kwa mahala popote,adui ni mtu mvivu anaye chagua cha kufanya
sikulaumu, nalaumu kichwa chako kuwa na uji badala ya akili
 
Naafiki 100%
 
Hata Ndugai nae kaja na yake......Mwenyeji wa Galilaya,Kapernaumu,Nazareth na Bethlehemu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…