Adui mkubwa wa Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe!

Adui mkubwa wa Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe!

na ndiyo maana Mh. Mbowe kaamua ku- reconcile na Dola ili kuangalia namna bora ya kudai haki kwa mazungumzo sababu kaona hakuna njia nyingine zozote ambazo nchi zingine walifanya wakafanikiwa kwetu zimedunda zote.

Kwa mfano watanzania mnapanga maandamano kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu kesho unajikuta peke yako mtaani na bango lako...unakula mkongoto wa haja unakwenda kuuza majeraha kwa pesa yako na kesi juu.
 
Naomba nizungumzie kiujumla, licha ya kwamba kati yetu binafsi, wapo ambao wako tofauti na walio wengi.

Watanzania wengi ni wajinga [wasiozijua haki zao] na ni waoga sana.

Mchanganyiko wa hizo sifa mbili ni kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya jamii.

Huwezi kupata maendeleo yoyote yale ya maana endapo idadi kubwa ya watu kwenye hiyo jamii wana hizo sifa za ujinga na uoga.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu, pale mtu asiye na mamlaka ya kukupora haki zako anapokupora, na wewe humpingi huyo mporaji kwa nguvu na uwezo wako wote, ni kitu gani kingine utakachoweza kukipigania kwa hali na mali?

Watanzania tumeshuhudia kuporwa baadhi ya haki zetu kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia takriban 2016 mpaka hivi sasa. Na tumekuwa wapole na wanyonge mno.

Alianza Rais Magufuli kukiuka katiba na kuvikataza vyama vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa, kikubwa kikiwa ni mikutano ya kisiasa.

Magufuli kaondoka, kaja Rais Samia naye akaendeleza huo uvunjaji wa katiba.

Wote hawa wawili wamevunja katiba waziwazi kabisa. Na sisi wananchi wenye nchi hakuna lolote la maana tulilolifanya kuwapinga hao wawili!

Tunaburuzwa buruzwa tu. Juzi hapa Samia eti katoa ruhusa ya vyama vya siasa kuanza kufanya mikutano ya kisiasa!

Hiyo ruhusa kaitoa kwa msingi gani wa mamlaka aliyonayo kisheria na kikatiba?

Sisi ni banana republic. Hatuongozwi na sheria wala katiba. Tunaongozwa na hisia, hisani, na matakwa ya mtu ambaye kimsingi ni mtumishi wetu, lakini kiuhalisia ni kama vile sisi ndo tunamtumikia yeye na si vinginevyo.

Kuna wakati kule Marekani, kipindi ambacho Donald Trump alikuwa Rais, kulikuwa na mjadala kuwa endapo angetoa agizo kwa jeshi la nchi hiyo, agizo lililo haramu kisheria na kikatiba, viongozi wa jeshi walikuwa wako tayari kabisa kulikaidi hilo agizo. Hawakuwa tayari kutekeleza agizo lolote linaloenda kinyume na sheria na katiba yao.

Hao ni watu wanaojitambua. Ni watu wasio waoga. Ni werevu na ni majasiri pia.

Hapa kwetu jambo kama hilo bado sijaona kama linawezekana.

Magufuli na Samia walipaswa kupingwa vikali sana.

Maagizo yao haramu ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani yalipaswa kukaidiwa na watekelezaji wa sheria.

Mtu kama kweli unajitambua, si mjinga wala muoga, kwa nini utekeleze amri ambayo si halali?

Kwani ukikataa kutekeleza amri ambayo si halali, nini kitakutokea?

Ije katiba mpya au isije, hii tuliyonayo sasa hivi inayotupatia haki tulizonazo sasa hivi, inakiukwa waziwazi kabisa na hatufanyi chochote kulinda hizo haki zetu, hiyo mpya tunayoitaka tutailinda kweli?

Kwa sasa nimeshahitimisha kuwa tatizo letu kubwa wala siyo katiba mpya. Tatizo ni sisi wenyewe. Bado tupo wajinga sana, wapole sana, na waoga sana.

Kwa hizi sifa, hata ije katiba mpya, hakutokuwa na tofauti yoyote ile. Tutaendelea kuburuzwa tu hadi pale tutapobadilika.

Na kwa kizazi hiki kilichopo, sitegemei tubadilike.

Adui wetu mkubwa ni sisi wenyewe!

Rais Samia hastahili pongezi yoyote ile kwa ‘kuruhusu’ vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa.

Hakuwa na haki ya kukataza hiyo mikutano. Hivyo hana haki ya kuruhusu mikutano hiyo.

Hastahili kabisa pongezi.

Anachopaswa kufanya ni kuomba radhi. Aombe radhi kwa kukiuka katiba.

Akiomba radhi kwa hilo, mimi nitakuwa wa kwanza kumpongeza kwa kuona kosa lake na kuamua kujirudi.

Nje ya hapo, siwezi kumpongeza mporaji aliyeamua kunirudishia kilicho changu.
Aisee ulipotelea wapi?
 
Haya mambo tunayapigia lip service, lakini kiukweli wengi tumepandishiwa tu.

1. Elimu ya darasani.
2. Demokrasia ya kiliberali.
3. Fikra za kisayansi.
4. Maendeleo ya uchumi wa kisasa.
5.Research and Development.
6. Heshima kwa utu wa kila mtu na ushirikishwaji wa umma.
7. Fikra tunduizi na dhahania.
8. Fikra hojaji.
9. Ukweli.
10. Haki.

Hivyo, nchi zinazodharau umuhimu wa haya, kuendelea ni vigumu.
 
Njoo uandamane, sio unaandika uko chini ya uvungu.

Halafu wewe ndio ulikuwa mshabiki mkubwa wa Jiwe alivyokuwa akikandamiza watu na kuteka, kisa ni msukuma mwenzio.

Sasa Leo wewe uliyeunga mkono ukandamizaji unahoji kwanini waliokandamizwa hawakuandamana
 
na ndiyo maana Mh. Mbowe kaamua ku- reconcile na Dola ili kuangalia namna bora ya kudai haki kwa mazungumzo sababu kaona hakuna njia nyingine zozote ambazo nchi zingine walifanya wakafanikiwa kwetu zimedunda zote.

Kwa mfano watanzania mnapanga maandamano kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu kesho unajikuta peke yako mtaani na bango lako...unakula mkongoto wa haja unakwenda kuuza majeraha kwa pesa yako na kesi juu.
Inakatisha tamaa kweli!

Hivi unakumbuka yake maandamano ya Tahrir Square kule Misri?

Kitu kama hicho hapa Tanzania hakiwezekani.
 
Mimi nilidhani mleta mada unakuja na hoja inayogusa jamii ya wananchi kwa ujumla wake kumbe ni maslahi ya kisiasa na vyama vya siasa.

Kwa hio kama hao viongozi wasingezuia hio mikutano ya kisiasa wasingekua na ubaya wowote.

Hivo mikutano ya kisiasa ilikuwepo kipindi kile cha uongozi wa Kikwete mbona faida yake haionekani katika jamii.

Kwamba kuruhusiwa hio mikutano ya kisiasa ndio mwanzo wa taifa na wananchi kwa ujumla wataondokana na umaskini na kadhia zote zilizo kati yetu?

Mbona mikutano haikufanyika miaka Saba Sasa na Bado Deni limeongezeka mpaka Trilioni 92?. Mfumuko wa Bei, mgao wa umeme , na maji, Hali ngumu ya Maisha.

Halafu yeye kaongelea siasa, wewe waweza ongelea uchumi.
 
Ulichosema ni sahihi sana

Naweza kuongezea kidogo, watanzania nashindwa namna nzuri ya kuongea lakini ni aina ya watu ambao wanaamini ukishakua kwenye madaraka basi umefanikiwa kimaisha wao hawatamani kuongoza ili walete mabadiliko chanya lakini wao wanatamani waongoze wajiletee mabadiliko chanya kwao ( ubinafsi wa hali ya juu)
Kila anayeingia kwenye nafasi yeyote hata mtendaji wa kijiji anawaza namna gani aile keki ya taifa hawazi namna gani anaweza kuilinda au aongeze keki zingine


Pili sisi ni watu wa mizaha na masihara sana Kila mtanzania ni mtu wa hivyo ni wepesi wa kuongea na si vitendo hili na uhakika nalo asilimia Mia mtanzania yeyote yule ni mtu wa aman aisee tuna extremists wachache sana nchini na sijui kwann hili limetokea wengi ni wanyonge wasio na sauti lakini wacheshi na wenye furaha basi maisha yanaenda haka ni kama ka immune flani hivi kanazuia mengi sana kwa haya mambo ya ccm watu wangekua washauana sana lakini tunaishi

Tatu na mwisho hili ntatoa kwa mfano then utaona mwenyewe watanzania ni watu wa namna gani mfano, 1.utakuta wanamshukuru raisi kuruhusu mikutano ya kisiasa
2. Wanamshukuru raisi kuwajengea let's say barabara
3. Vifurushi vikipandishwa vikashushwa na rais watamshukuru raisi

Kila jambo wao wanaona ni hisani so Unaweza kufikiria mwenyewe hawa watu ni wa namna gani si wasomi na ambao hawajasoma wote huwa wana behave hivi

Nini haswa kifanyike ngoja ninywe maji nirudi.!.
 
Kama katiba iliyopo inakiukwa na hatufanyi kitu, hiyo mpya ikikiukwa tutafanya nini?

Sisi ni watu wa ajabu sana.
elimu yetu yenyewe bado haisaidii kujitambua ndo kwanza inazidisha ujinga na uoga, vijana wanaomaliza vyuo kila siku wanajiunga kwenye mapambio na kuendeleza uchawa wakati tulitegemea hawa waje kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi wengine kaujitambua ili kupingana na udhulumati.

Unakuta muda mwingine bora hata wazee ambao hawana elimu za vyuo vikuu wanatambua haki zao ipasavyo kuliko vijana wa sasa wenye degree.
 
Na ndo maana Kenyatta alishawahi kumwambi Nyerere "anaongoza wafu"

Tatizo watanzania hatuna sauti ya umma na umoja kuanzia ngazi za chini kabisa mfano nyumbani ,mitaanii. mtu anaweza dhulumiwa haki yake na akashindwa kujitetea akasubiri atokee mtu mwingine aje amtetee, na huyo mtu anaweza asitokee kumsaidia.
Mfano,
Imagine, dala dala inaweza kuwafaulisha kwa gari lingine bila sababu ya msingi utakuta watu wanalalamika chini kwa chini wanashindwa kuunganisha sauti zao kugomea kwa kitendo walichofanyiwa, na anapotokea mtu mmoja kuonyesha msimamo unakuta wengine wanaogopa wanashindwa kumuunga mkono.

Mfano mwengine,
Siku hizi barabara za mjini kuna Traffic wengi sana, kazi yao kubwa ni kukusanya ushuru barabarani kila gari linalopita wanachukua buku mbili mpaka buku tano tena unakuta wametanda kila mahali mpaka unafika mwisho wa gari ushakutana hata na watano ila cha kushangaza madereva wanabaki kulalamika tu ila wanashindwa kuweka msimamo kwenye haki zao, na kuhoji kuhusu huu utaratibu unabaki kuona ujinga tulionao wengi wetu.

ukiangalia hii mifano ndo unapata aina ya watu waliopo Tanzania na ndo unapokuja kujua nini Alimaanisha kenyatta kutuita sisi Wafu.
maisha ya janja janja ya kutotaka kufata sheria na utaratibu ndio yametufikisha hapa,unakuta magari yana issue nyingi sana kiasi kwamba ukifatwa utaratibu basi hela itakayotolewa ni kubwa bila kujali kwamba hata hizo buku mbili mbili angeweza kuclear issue zote zisingekuwa zimtoka sasa kinachofanyika madereva wanaepusha shari na kuamua kulipa buku mbili ili mambo yaende kuliko kufanya kitu ambacho sheria itamlinda na hatopata usumbufu....janja janja tunaipenda sana na ndio tunaiishi kwa kujiaminisha kwamba ni nafuu
 
Ndio inavyotakiwa. Yaani polisi, jeshi na usalama wanapaswa kukataa maagizo yoyote ambayo ni kinyume na sheria. Yena wakiona wanasiasa wanazingua wanawapindua tu 😂😂😂😂. Yaaani libaba lizima na bunduki na silaha zote na kozi zote eti unaagizwa kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na wewe unakubali 😂😂😂. Unakuta libaba lizima linaagizwa kuchakachua uchaguzi na lenyewe linakubali.

Wengi wa wanaopewa vyeo huko kwenye vyombo vya dola, aidha wana uwezo mdogo,na pia huongozwa na ubinafsi. Hivyo mtu anajua akitaka mwanasiasa afuate sheria atamtoa kwenye hicho cheo, na kumuweka mwingine kisha yeye binafsi atakosa mshahara mnono na posho kedekede.
 
Iko sababu ya kimaadili na elimu.

WaTanzania wengi hawana maadili mazuri, ujanja ujanja, majizi, unafiki, rushwa, siyo watu wa kupenda haki.

Hili tatizo ni kubwa sana hata kwa mtu mmoja mmoja kila akipata nafasi atataka akuibie, achukue rushwa hii hata ukienda ofisi tu za uma za kawaida utakutana nayo.
Wengine wanafikia hatua kusema maisha hayawezi kwenda bila kufanya hayo, wanaona fahari.

Sasa watu wa hivi wasiojua na kufahamu misingi ya haki na uadilifu hawawezi kuhoji haki zao zikivunjwa wanajionea sawa tu.

Sababu hata wenyewe wako vilevile, yani mwizi anamkemea mwizi hii ni ngumu sana.

Elimu inayotolewa huko mashuleni kuanzia msingi hadi vyuoni haina ubora.

Hili ni janga la kitaifa.

Inawadumaza tu wengi yani bila juhudi binafsi ya mtu kutafuta maarifa sahihi ataondoka na vyeti vina A lakini kichwani mtupu.

Hata wasomi vyuo vikuu hawawezi hata kuhoji, wamekua majuha tu sababu wamefundishwa kwa mazingira kama hayo siyo rahisi kuuliza maswali kwa uhuru kwa lecturer atakufelisha Tanzania, ataona unampinga.

Kwa hivyo hatokuja kuweza kudai haki zake au kuhoji mamlaka, kuwadhibiti walio kwenye mamlaka wanapovunja sheria na katiba.

Watanzania kukosa maadili na Elimu duni.
 
Prof. Lumumba aliwahi kusema kuwa;
Demokrasia ya Marekani haiwezi kuwa sawa na demokrasia ya Afrika/ Tanzania, wala hatulazimiki kufuata demokrasia za mataifa ya ulaya.

Sisi kama watanzania tuna aina yetu ya demokrasia iliyo ambatana na desturi zetu sisi.
usituletee mambo ya waamarekani ambao wao hata ushoga kwao ni haki!! na wala hawaoni aibu kudai haki hiyo.
 
Back
Top Bottom