Adui mkubwa wa Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe!

Adui mkubwa wa Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe!

Afrika, na hususan Tanzania siyo Marekani wewe hayawani. Wewe na werevu na ujasiri wako, ulikuwa wapi kupinga hilo katazo wakati wa utawala wa JPM? Mnasubiri jambo litokee halafu mnakuja kuonyesha unafiki wenu. Siasa waachieni Wanasiasa: mikutano ya kisiasa nje ya chaguzi ni watu wachache sana wanahudhuria.
 
Afrika, na hususan Tanzania siyo Marekani wewe hayawani. Wewe na werevu na ujasiri wako, ulikuwa wapi kupinga hilo katazo wakati wa utawala wa JPM? Mnasubiri jambo litokee halafu mnakuja kuonyesha unafiki wenu. Siasa waachieni Wanasiasa: mikutano ya kisiasa nje ya chaguzi ni watu wachache sana wanahudhuria.
Old ass nigga…you already know whenever me and you cross paths, it’s on-site.

I’ll fold you like a pretzel and dunk you in some Sweet Baby Ray’s Hickory & Brown Sugar barbecue sauce.

Watch your Twitter fingers.
 
....Na. Adui mkubwa wa CCM ni CCM wenyewe.

Kuwa "Ndivyo Tulivyo"

Kuna ulazima wa kubadilika Fikra.

Hayati alijaribu hayo(Kubadilisha Fikra za Wananchi wake) tunaona yanayojiri...Uhasama hasi toka mwanzo...

Hakuogopa, Wananchi nao Wakaanza kuondoa woga. Ni kwa sababu ya Ujasiri,ni kwasababu ya kuwa Kiongozi ndipo kulitupeleka kuanza Kuamini kuwa Tunaweza fanya /kuleta, mabadiliko....

Walakin...
Tumerudi kwenye Uwoga, Tumerudi Kukubali kuambiwa hatuwezi hili wala lile Kwamba bila Misaada wala Mikopo hatuwezi sogea mbele... n.k .Ni woga toka juu unatiririka chini...

Ni Uongozi tu. Na uongozi huo ni wa CCM
Tutajirudi, Lazima Tujirudi

...vile vile, sio Lazima kukubali Maadili na Utamaduni wa Nje, Iwe mwiko Kukubali. Sio kila kitu cha nje kinaweza leta Mafanikio ambayo kwa namna moja au nyingine tunakataa kuwa Tunayo hayo Mafanikio. Muda utaeleza



Bado mbichi hiyo...
Mie nimeshakubali Kwenda kuzikwa Chato, Mie nimeshakubali sihami kwenda Burundi, Mie nimeshakubali kujitoa Mhanga. Siogopi sasa kama huko Nyuma. Nawashukuru wadhalimu wote kwa kunifikisha nilipo-Kifikra, Kimawazo Uhasam wenu umenifanya kutokuwa na Uwoga.
Asanteni.

Aluta Continua
 
Old ass nigga…you already know whenever me and you cross paths, it’s on-site.

I’ll fold you like a pretzel and dunk you in some Sweet Baby Ray’s Hickory & Brown Sugar barbecue sauce.

Watch your Twitter fingers.
Duh

Ova
 
Rais hayuko juu ya sheria, hata kwa hii katiba ya sasa.

Ni ujinga na uoga wetu sisi Watanzania ndo unaowapa uthubutu hao watawala wa kupora haki za watu.
Kama katiba hii inamruhusu rais kuwa dikteta, basi tambuwa dikteta huwa juu ya sheria.

Kama sikosei, the late mwalimu Nyerere alilisema hili.
 
Naomba nizungumzie kiujumla, licha ya kwamba kati yetu binafsi, wapo ambao wako tofauti na walio wengi.

Watanzania wengi ni wajinga [wasiozijua haki zao] na ni waoga sana.

Mchanganyiko wa hizo sifa mbili ni kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya jamii.

Huwezi kupata maendeleo yoyote yale ya maana endapo idadi kubwa ya watu kwenye hiyo jamii wana hizo sifa za ujinga na uoga.

Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu, pale mtu asiye na mamlaka ya kukupora haki zako anapokupora, na wewe humpingi huyo mporaji kwa nguvu na uwezo wako wote, ni kitu gani kingine utakachoweza kukipigania kwa hali na mali?

Watanzania tumeshuhudia kuporwa baadhi ya haki zetu kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia takriban 2016 mpaka hivi sasa. Na tumekuwa wapole na wanyonge mno.

Alianza Rais Magufuli kukiuka katiba na kuvikataza vyama vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa, kikubwa kikiwa ni mikutano ya kisiasa.

Magufuli kaondoka, kaja Rais Samia naye akaendeleza huo uvunjaji wa katiba.

Wote hawa wawili wamevunja katiba waziwazi kabisa. Na sisi wananchi wenye nchi hakuna lolote la maana tulilolifanya kuwapinga hao wawili!

Tunaburuzwa buruzwa tu. Juzi hapa Samia eti katoa ruhusa ya vyama vya siasa kuanza kufanya mikutano ya kisiasa!

Hiyo ruhusa kaitoa kwa msingi gani wa mamlaka aliyonayo kisheria na kikatiba?

Sisi ni banana republic. Hatuongozwi na sheria wala katiba. Tunaongozwa na hisia, hisani, na matakwa ya mtu ambaye kimsingi ni mtumishi wetu, lakini kiuhalisia ni kama vile sisi ndo tunamtumikia yeye na si vinginevyo.

Kuna wakati kule Marekani, kipindi ambacho Donald Trump alikuwa Rais, kulikuwa na mjadala kuwa endapo angetoa agizo kwa jeshi la nchi hiyo, agizo lililo haramu kisheria na kikatiba, viongozi wa jeshi walikuwa wako tayari kabisa kulikaidi hilo agizo. Hawakuwa tayari kutekeleza agizo lolote linaloenda kinyume na sheria na katiba yao.

Hao ni watu wanaojitambua. Ni watu wasio waoga. Ni werevu na ni majasiri pia.

Hapa kwetu jambo kama hilo bado sijaona kama linawezekana.

Magufuli na Samia walipaswa kupingwa vikali sana.

Maagizo yao haramu ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani yalipaswa kukaidiwa na watekelezaji wa sheria.

Mtu kama kweli unajitambua, si mjinga wala muoga, kwa nini utekeleze amri ambayo si halali?

Kwani ukikataa kutekeleza amri ambayo si halali, nini kitakutokea?

Ije katiba mpya au isije, hii tuliyonayo sasa hivi inayotupatia haki tulizonazo sasa hivi, inakiukwa waziwazi kabisa na hatufanyi chochote kulinda hizo haki zetu, hiyo mpya tunayoitaka tutailinda kweli?

Kwa sasa nimeshahitimisha kuwa tatizo letu kubwa wala siyo katiba mpya. Tatizo ni sisi wenyewe. Bado tupo wajinga sana, wapole sana, na waoga sana.

Kwa hizi sifa, hata ije katiba mpya, hakutokuwa na tofauti yoyote ile. Tutaendelea kuburuzwa tu hadi pale tutapobadilika.

Na kwa kizazi hiki kilichopo, sitegemei tubadilike.

Adui wetu mkubwa ni sisi wenyewe!

Rais Samia hastahili pongezi yoyote ile kwa ‘kuruhusu’ vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa.

Hakuwa na haki ya kukataza hiyo mikutano. Hivyo hana haki ya kuruhusu mikutano hiyo.

Hastahili kabisa pongezi.

Anachopaswa kufanya ni kuomba radhi. Aombe radhi kwa kukiuka katiba.

Akiomba radhi kwa hilo, mimi nitakuwa wa kwanza kumpongeza kwa kuona kosa lake na kuamua kujirudi.

Nje ya hapo, siwezi kumpongeza mporaji aliyeamua kunirudishia kilicho changu.
Most Tanzanians are lazy and sloppy, let's face the facts.
 
Kama katiba hii inamruhusu rais kuwa dikteta, basi tambuwa dikteta huwa juu ya sheria.

Kama sikosei, the late mwalimu Nyerere alilisema hili.
Actually sidhani kama katiba hii inamruhusu Rais kuwa dikteta.

Kinachompa fursa Rais kuwa dikteta ni ujinga na uoga wa wananchi.

Magufuli na Samia walitumia kipengele gani cha katiba hii kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa?
 
Actually sidhani kama katiba hii inamruhusu Rais kuwa dikteta.

Kinachompa fursa Rais kuwa dikteta ni ujinga na uoga wa wananchi.

Magufuli na Samia walitumia kipengele gani cha katiba hii kupiga marufuku mikutano ya vyama vya siasa?
Rais ambaye hawezi kushitakiwa popote na yeyote akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu, anaweza kupingwa na nani? Kumbuka dola yote iko mikononi mwake. Siyo jeshi, polisi wala usalama tu. Hadi mahakama hakuna mwenye uwezo wala uthubutu wa kwenda kinyume na rais.

Wakati maandamano yalipotaka kufanyika sijui yale ya “ukuta”, rais alituma jeshi la wananchi mtaani.

Rais akilalamika juu yako huna lako. Usipopotezwa unaweza kufia jela kwa kesi ya kupewa.
 
Mimi nilidhani mleta mada unakuja na hoja inayogusa jamii ya wananchi kwa ujumla wake kumbe ni maslahi ya kisiasa na vyama vya siasa.

Kwa hio kama hao viongozi wasingezuia hio mikutano ya kisiasa wasingekua na ubaya wowote.

Hivo mikutano ya kisiasa ilikuwepo kipindi kile cha uongozi wa Kikwete mbona faida yake haionekani katika jamii.

Kwamba kuruhusiwa hio mikutano ya kisiasa ndio mwanzo wa taifa na wananchi kwa ujumla wataondokana na umaskini na kadhia zote zilizo kati yetu?
Kwa comment hii, nimemwamini Nyami Ngabu.
 
Rais ambaye hawezi kushitakiwa popote na yeyote akiwa madarakani na hata baada ya kustaafu, anaweza kupingwa na nani? Kumbuka dola yote iko mikononi mwake. Siyo jeshi, polisi wala usalama tu. Hadi mahakama hakuna mwenye uwezo wala uthubutu wa kwenda kinyume na rais.

Wakati maandamano yalipotaka kufanyika sijui yale ya “ukuta”, rais alituma jeshi la wananchi mtaani.

Rais akilalamika juu yako huna lako. Usipopotezwa unaweza kufia jela kwa kesi ya kupewa.
Nimezungumzia ujinga wa Watanzania na kutolea mfano majenerali wa Marekani walivyokuwa tayari kukaidi amri haramu toka kwa Trump.

Ukiwa mjinga na muoga utakubali kutekeleza amri zilizo haramu.

Ukiwa mjinga na muoga, hata katiba ikiruhusu Rais kushitakiwa mahakamani, huko mahakamani utakutana na majaji wajinga na walio waoga, hivyo hayo mashitaka dhidi ya Rais hayatakuwa na maana yoyote ile maana hakuna atayethubutu kumkuta na hatia Rais.

Inaonekana point yangu umeshindwa kuielewa.
 
06 January 2023

Balozi Wilbrod Slaa azungumzia tamko haramu la JPM kuzuia mikutano na tamko la kufutwa la kufutwa kwake


Dr. Wilbrod Slaa achambua kwa kina kuhusu zuio haramu kuondolewa na rais Samia Hassan. Tamko haramu la John Magufuli halikuandikwa ktk gazeti la serikali ( Govt Gazette) kama tangazo kwa kuwa lilikuwa haramu pia lilikuwa linapingana na katiba. Bunge kukaa kimya wakati ni jukumu lake kutunga sheria ni udhaifu mwingine. Ashangaa wanasheria wasomi kushindwa kuliona hilo na anadhani ndiyo maana wanasheria wengi wamefeli mitihani ya shule ya sheria baada ya kumaliza digrii zao kwakuwa hawajapikwa vizuri....
 
Ukitumia hisia wewe ndo mjinga maana utaishia kuishi maisha ya mateso hadi kufa ila ukiishi kwa akili ukajua kwamba hapa niwe mpole tu utaishi kwa amani... Watu ambao wapo kimya sio kwamba ni waoga au wajinga hapana ila wanajua matokeo, Unaweza ukafa na upumbavu ukabaki palepale. Upumbavu upo kwa viongozi hadi kwa wanaowaongoza, mean what ? Hiyo ni kumaanisha elimu ndo mkombozi kwa vizazi vijavyo kama ikianza kuvaliwa njuga watu wakaanza kufunzwa haki zao, Uzalendo n.k.... ila hivi vizazi vya sasa ni Too-late tulichotoka nacho kwenye shule tulizosoma ni vyeti na stori za moments... Upumbavu unarisiwa, Huwezi kupambania haki yako ambayo huijui.... Kmmake kuna vitu vinakera sana kwenye mataifa yetu ya Africa imagine viongozi wanajua kabisa mitaala tunayotumia kufundishwa shuleni haina maana yoyote kwenye maisha yetu ila still bado hata hawana habari.... Acha tu nisiongee na umri wangu huu mdogo ntaambiwa sijui kitu kwenye hii nchi nanuka mavi.
 
Prof. Lumumba aliwahi kusema kuwa;
Demokrasia ya Marekani haiwezi kuwa sawa na demokrasia ya Afrika/ Tanzania, wala hatulazimiki kufuata demokrasia za mataifa ya ulaya.

Sisi kama watanzania tuna aina yetu ya demokrasia iliyo ambatana na desturi zetu sisi.
usituletee mambo ya waamarekani ambao wao hata ushoga kwao ni haki!! na wala hawaoni aibu kudai haki hiyo.
Eti wewe pia ni Great Thinker!
 
na ndiyo maana Mh. Mbowe kaamua ku- reconcile na Dola ili kuangalia namna bora ya kudai haki kwa mazungumzo sababu kaona hakuna njia nyingine zozote ambazo nchi zingine walifanya wakafanikiwa kwetu zimedunda zote.

Kwa mfano watanzania mnapanga maandamano kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu kesho unajikuta peke yako mtaani na bango lako...unakula mkongoto wa haja unakwenda kuuza majeraha kwa pesa yako na kesi juu.
Unataka kusema mkuu watanzania hawana rekodi za kuandamana huko nyuma na kupata misukosuko ya polisi katika nchi hii?
 
Nimezungumzia ujinga wa Watanzania na kutolea mfano majenerali wa Marekani walivyokuwa tayari kukaidi amri haramu toka kwa Trump.

Ukiwa mjinga na muoga utakubali kutekeleza amri zilizo haramu.

Ukiwa mjinga na muoga, hata katiba ikiruhusu Rais kushitakiwa mahakamani, huko mahakamani utakutana na majaji wajinga na walio waoga, hivyo hayo mashitaka dhidi ya Rais hayatakuwa na maana yoyote ile maana hakuna atayethubutu kumkuta na hatia Rais.

Inaonekana point yangu umeshindwa kuielewa.
Labda wewe ndiyo umeshindwa kuilewa point yangu.

Mkuu katiba ya marekani huwezi kuifananisha hata kidogo na ya kwetu.

Tangu Nyerere alipotaka kupinduliwa jeshi, katiba ilibadilishwa, ni vigumu kwa jeshi kwenda kinyume na rais. Ikitokea anaondolewa tu na kushitakiwa. Mwingine anateuliwa mambo yanaendelea.

Uoga wa watanzania umechangiwa na mambo kama hayo. Katiba mpya ndo mwanzo mzuri.

Kama kutakuwa na uwajibishwaji wa hao viongozi, wananchi wataona “halaa! Kumbe inawezekana?”

If there’s no way out, ni ngumu kumpata panya atakayethubutu kumfunga paka kengele.

Kama kiongozi ataruhusiwa kushitakiwa, hapo hata upande wa majaji watafanya inavyotakiwa. Lazima kuwepo na pahala pa kuanzia. Ndiyo point yangu kuwa katiba mpya ni mwanzo mzuri.

Fear can be instilled! And our leaders have just done that. Through many ways. Including by using the constitution.

Rais ni kama Mungu mtu kwa Tanzania.
 
Back
Top Bottom