Aisee ulipotelea wapi?Naomba nizungumzie kiujumla, licha ya kwamba kati yetu binafsi, wapo ambao wako tofauti na walio wengi.
Watanzania wengi ni wajinga [wasiozijua haki zao] na ni waoga sana.
Mchanganyiko wa hizo sifa mbili ni kikwazo kikubwa sana katika maendeleo ya jamii.
Huwezi kupata maendeleo yoyote yale ya maana endapo idadi kubwa ya watu kwenye hiyo jamii wana hizo sifa za ujinga na uoga.
Kwa nini nasema hivyo? Nasema hivyo kwa sababu, pale mtu asiye na mamlaka ya kukupora haki zako anapokupora, na wewe humpingi huyo mporaji kwa nguvu na uwezo wako wote, ni kitu gani kingine utakachoweza kukipigania kwa hali na mali?
Watanzania tumeshuhudia kuporwa baadhi ya haki zetu kwa miaka ya hivi karibuni kuanzia takriban 2016 mpaka hivi sasa. Na tumekuwa wapole na wanyonge mno.
Alianza Rais Magufuli kukiuka katiba na kuvikataza vyama vya upinzani kufanya shughuli zao za kisiasa, kikubwa kikiwa ni mikutano ya kisiasa.
Magufuli kaondoka, kaja Rais Samia naye akaendeleza huo uvunjaji wa katiba.
Wote hawa wawili wamevunja katiba waziwazi kabisa. Na sisi wananchi wenye nchi hakuna lolote la maana tulilolifanya kuwapinga hao wawili!
Tunaburuzwa buruzwa tu. Juzi hapa Samia eti katoa ruhusa ya vyama vya siasa kuanza kufanya mikutano ya kisiasa!
Hiyo ruhusa kaitoa kwa msingi gani wa mamlaka aliyonayo kisheria na kikatiba?
Sisi ni banana republic. Hatuongozwi na sheria wala katiba. Tunaongozwa na hisia, hisani, na matakwa ya mtu ambaye kimsingi ni mtumishi wetu, lakini kiuhalisia ni kama vile sisi ndo tunamtumikia yeye na si vinginevyo.
Kuna wakati kule Marekani, kipindi ambacho Donald Trump alikuwa Rais, kulikuwa na mjadala kuwa endapo angetoa agizo kwa jeshi la nchi hiyo, agizo lililo haramu kisheria na kikatiba, viongozi wa jeshi walikuwa wako tayari kabisa kulikaidi hilo agizo. Hawakuwa tayari kutekeleza agizo lolote linaloenda kinyume na sheria na katiba yao.
Hao ni watu wanaojitambua. Ni watu wasio waoga. Ni werevu na ni majasiri pia.
Hapa kwetu jambo kama hilo bado sijaona kama linawezekana.
Magufuli na Samia walipaswa kupingwa vikali sana.
Maagizo yao haramu ya kuzuia mikutano ya kisiasa ya vyama vya upinzani yalipaswa kukaidiwa na watekelezaji wa sheria.
Mtu kama kweli unajitambua, si mjinga wala muoga, kwa nini utekeleze amri ambayo si halali?
Kwani ukikataa kutekeleza amri ambayo si halali, nini kitakutokea?
Ije katiba mpya au isije, hii tuliyonayo sasa hivi inayotupatia haki tulizonazo sasa hivi, inakiukwa waziwazi kabisa na hatufanyi chochote kulinda hizo haki zetu, hiyo mpya tunayoitaka tutailinda kweli?
Kwa sasa nimeshahitimisha kuwa tatizo letu kubwa wala siyo katiba mpya. Tatizo ni sisi wenyewe. Bado tupo wajinga sana, wapole sana, na waoga sana.
Kwa hizi sifa, hata ije katiba mpya, hakutokuwa na tofauti yoyote ile. Tutaendelea kuburuzwa tu hadi pale tutapobadilika.
Na kwa kizazi hiki kilichopo, sitegemei tubadilike.
Adui wetu mkubwa ni sisi wenyewe!
Rais Samia hastahili pongezi yoyote ile kwa βkuruhusuβ vyama vya siasa kufanya mikutano ya kisiasa.
Hakuwa na haki ya kukataza hiyo mikutano. Hivyo hana haki ya kuruhusu mikutano hiyo.
Hastahili kabisa pongezi.
Anachopaswa kufanya ni kuomba radhi. Aombe radhi kwa kukiuka katiba.
Akiomba radhi kwa hilo, mimi nitakuwa wa kwanza kumpongeza kwa kuona kosa lake na kuamua kujirudi.
Nje ya hapo, siwezi kumpongeza mporaji aliyeamua kunirudishia kilicho changu.
Uko sahihi,
Mfano Lisu alipotugeuka na kuanza kutetea mafisadi ya Acacia kisa tu wamemhonga hela.
Ni umaskini tuβ¦..sikuwa na hela ya vocha πAisee ulipotelea wapi?
Kufanya mikutano non stop ndo uadui wenyewe wa mtanzania.
Inakatisha tamaa kweli!na ndiyo maana Mh. Mbowe kaamua ku- reconcile na Dola ili kuangalia namna bora ya kudai haki kwa mazungumzo sababu kaona hakuna njia nyingine zozote ambazo nchi zingine walifanya wakafanikiwa kwetu zimedunda zote.
Kwa mfano watanzania mnapanga maandamano kupinga ukiukwaji wa haki za binadamu kesho unajikuta peke yako mtaani na bango lako...unakula mkongoto wa haja unakwenda kuuza majeraha kwa pesa yako na kesi juu.
Okay sawa!Nazungumzia haki zilizopo kikatiba.
Au hujaelewa nilichokiandika?
Kwa akili yako fupi unadhani Lisu alijitolea kuwatetea bure Acacia?Good question.
Nadhani afafanue zaidi with solid proof otherwise ni hadithi za kwenye vijiwe vya kahawa tu.
Mimi nilikaa kati mkuu kusubiri ubainifu.Wewe uliziamini hizo taarifa?
Mimi nilidhani mleta mada unakuja na hoja inayogusa jamii ya wananchi kwa ujumla wake kumbe ni maslahi ya kisiasa na vyama vya siasa.
Kwa hio kama hao viongozi wasingezuia hio mikutano ya kisiasa wasingekua na ubaya wowote.
Hivo mikutano ya kisiasa ilikuwepo kipindi kile cha uongozi wa Kikwete mbona faida yake haionekani katika jamii.
Kwamba kuruhusiwa hio mikutano ya kisiasa ndio mwanzo wa taifa na wananchi kwa ujumla wataondokana na umaskini na kadhia zote zilizo kati yetu?
elimu yetu yenyewe bado haisaidii kujitambua ndo kwanza inazidisha ujinga na uoga, vijana wanaomaliza vyuo kila siku wanajiunga kwenye mapambio na kuendeleza uchawa wakati tulitegemea hawa waje kuwa mabalozi wazuri kwa wananchi wengine kaujitambua ili kupingana na udhulumati.Kama katiba iliyopo inakiukwa na hatufanyi kitu, hiyo mpya ikikiukwa tutafanya nini?
Sisi ni watu wa ajabu sana.
Na mpenzi wakoNimeachiwa na nani we Muree?
maisha ya janja janja ya kutotaka kufata sheria na utaratibu ndio yametufikisha hapa,unakuta magari yana issue nyingi sana kiasi kwamba ukifatwa utaratibu basi hela itakayotolewa ni kubwa bila kujali kwamba hata hizo buku mbili mbili angeweza kuclear issue zote zisingekuwa zimtoka sasa kinachofanyika madereva wanaepusha shari na kuamua kulipa buku mbili ili mambo yaende kuliko kufanya kitu ambacho sheria itamlinda na hatopata usumbufu....janja janja tunaipenda sana na ndio tunaiishi kwa kujiaminisha kwamba ni nafuuNa ndo maana Kenyatta alishawahi kumwambi Nyerere "anaongoza wafu"
Tatizo watanzania hatuna sauti ya umma na umoja kuanzia ngazi za chini kabisa mfano nyumbani ,mitaanii. mtu anaweza dhulumiwa haki yake na akashindwa kujitetea akasubiri atokee mtu mwingine aje amtetee, na huyo mtu anaweza asitokee kumsaidia.
Mfano,
Imagine, dala dala inaweza kuwafaulisha kwa gari lingine bila sababu ya msingi utakuta watu wanalalamika chini kwa chini wanashindwa kuunganisha sauti zao kugomea kwa kitendo walichofanyiwa, na anapotokea mtu mmoja kuonyesha msimamo unakuta wengine wanaogopa wanashindwa kumuunga mkono.
Mfano mwengine,
Siku hizi barabara za mjini kuna Traffic wengi sana, kazi yao kubwa ni kukusanya ushuru barabarani kila gari linalopita wanachukua buku mbili mpaka buku tano tena unakuta wametanda kila mahali mpaka unafika mwisho wa gari ushakutana hata na watano ila cha kushangaza madereva wanabaki kulalamika tu ila wanashindwa kuweka msimamo kwenye haki zao, na kuhoji kuhusu huu utaratibu unabaki kuona ujinga tulionao wengi wetu.
ukiangalia hii mifano ndo unapata aina ya watu waliopo Tanzania na ndo unapokuja kujua nini Alimaanisha kenyatta kutuita sisi Wafu.
Ndio inavyotakiwa. Yaani polisi, jeshi na usalama wanapaswa kukataa maagizo yoyote ambayo ni kinyume na sheria. Yena wakiona wanasiasa wanazingua wanawapindua tu ππππ. Yaaani libaba lizima na bunduki na silaha zote na kozi zote eti unaagizwa kufanya vitendo ambavyo ni kinyume na sheria na wewe unakubali πππ. Unakuta libaba lizima linaagizwa kuchakachua uchaguzi na lenyewe linakubali.