Adui mkubwa wa Mtanzania ni Mtanzania mwenyewe!


Kwa hiyo unashauri sheria zifuatwe kwakuwa hata zikifuatwa matatizo yetu hayataisha?!
 

Kwahiyo katiba yetu ina sheria za demokrasia ya Marekani?
 
Pole sana nyanu ngabu Ile Layer yako yoote ya Sgang kwisha habari. Naona sasa akili zimekurudi
 
Mkuu mimi siyo mbobezi wa mambo ya katiba na sheria, ila natambua kutokana na katiba yetu, tamko ama agizo la Rais, "presidential decree", huweza kuondolewa na kupitia tamko lingine la Rais mwenyewe, endapo hakutawepo mchakato wowote ule wa kisheria kulipinga tamko hilo.

Kwa kudesa katika nyaraka za kimtandao tunaona;

A decree of that nature is a legal proclamation issued by the president of a republic, according to certain procedures (usually established in a constitution). It has the force of law. The particular term used for this concept may vary from country to country. The executive orders are decrees (although a decree is not exactly an order).

Kwa hiyo kwa mujibu wa katiba ya Tanzania, pale tu JPM alipotoa agizo hilo, vyombo vya dola vikalichukulia kama katazo rasmi, na yeyote ambaye angekwenda kinyume chake angepambana na nguvu ya vyombo hivyo. Kwa hiyo pasipo kujali uharamu wake, Rais SSH ametumia vyema nafasi yake kulikondoa katazo hilo kwa hekima.
 
Kweli sisi ni mazuzu,na hatujuwi mpaka leo tunataka nini?

Eti sahvi dk slaa anaponda katazo la kuzuiwa mikutano ya kisiasa,wakati yeye alipokuwa balozi hakuwahi kuhoji

Ova
 

Nilishangazwa sana na viongozi wa vyama vya upinzani kusimama na kumpigia makofi Rais Samia.

Unampongeza mtu kwa kuwa ametangaza kuacha kuvunja sheria? Huku ndiko nchi yetu ilipofikia, ni aibu mno.
 

Nilishangazwa sana na viongozi wa vyama vya upinzani kusimama na kumpigia makofi Rais Samia.

Unampongeza mtu kwa kuwa ametangaza kuacha kuvunja sheria? Huku ndiko nchi yetu ilipofikia, ni aibu mno.
Lazima wapige makofi maana hyo ndiyo atawapa ruzuku za vyama

Ova
 
Katiba mpya ni mwanzo mzuri.

Kama rais yuko juu ya sheria, hakuna chombo chochote kitakachothubutu kuwa kinyume naye….Iwe jeshi, polisi au mahakama.
 
Ndio maana mimi najiuliza mara nyingi, kama kwa katiba hii hata haki za kikatiba tunashindwa kuzidai ni nini katiba mpya itafanya?

Kwanza isambazwe elimu ya uraia ili tujitambue walau kwa haki za msingi zilizopo. Bila hivyo katiba mpya itakuwa mvinyo mpya kwenye kiriba kikuu.

Sent from my SM-A315F using JamiiForums mobile app
 
Katiba mpya ni mwanzo mzuri.

Kama rais yuko juu ya sheria, hakuna chombo chochote kitakachothubutu kuwa kinyume naye….Iwe jeshi, polisi au mahakama.
Ni kweli kwamba Watanzania wengi hawaitumii kikamilifu hata hii katiba iliyopo, hawaijui vizuri, hili ni tatizo.

Kuna mzee mmoja aliulizwa na Tume ya Warioba anataka nini katika katiba mpya, akasema anataka haki ya kuoa wake wengi, kitu ambacho kinaruhusiwa kikatiba tayari.

Tunahitaji utamaduni wa kuheshimu na kuitumia katiba.

Lakini hii si sababu ya kuacha kudai katiba mpya, kwa maana, hata mazungumzo ya, na mchakato wa kudai katiba mpya tu, vinawafungua macho Watanzania wengi kuhusu si tu umuhinu wa katiba mpya, bali hata utamaduni wa kuheshimu katiba na ukatiba, pamoja na kuitumia vizuri hata katiba ya sasa.
 
Katiba mpya ni mwanzo mzuri.

Kama rais yuko juu ya sheria, hakuna chombo chochote kitakachothubutu kuwa kinyume naye….Iwe jeshi, polisi au mahakama.
Rais hayuko juu ya sheria, hata kwa hii katiba ya sasa.

Ni ujinga na uoga wetu sisi Watanzania ndo unaowapa uthubutu hao watawala wa kupora haki za watu.
 
Hapo ndo unapoona kuwa matatizo yetu ni zaidi ya katiba [mpya].
 

Nilishangazwa sana na viongozi wa vyama vya upinzani kusimama na kumpigia makofi Rais Samia.

Unampongeza mtu kwa kuwa ametangaza kuacha kuvunja sheria? Huku ndiko nchi yetu ilipofikia, ni aibu mno.
Mimi bado nashangaa!
 
05 January 2023

Askofu - Siwezi kumsifia kwa kuchelewa kuondoa amri haramu ya rais aliyepita, alitakiwa siku ya kwanza alipoingia madarakani angeiondoa amri hii haramu ya mtangulizi wake ...

 
Unalinganisha Bongo na Marekani?
Sie wenzetu ni Kenya,Uganda,wabongo sio wajinga kiasi hicho,waliwahi kumpinga Nyerere,na wengine walipoteza maisha!wakati wa Maghu,wengi walimpinga,na walilipa kwa kupoteza maisha yao!!
Wewe unayesema wabongo ni wajinga,hujawahi hata kulala lockup!!
Umekaa sehemu unaandika makala nyuma ya keyboard hutaki hata kujulikana!
 
Naunga mkono..

Tumekuwa watu wakuomba wakati mwingine ni wajibu na hali yetu kupata...
Tumeshazowea kuomba ! Hata dukani tunasemaga naomba kiberiti huku nampa pesa Mangi au Mgosi. !
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…