Kuombea Covid kwa sala siyo jambo baya, lakini kuwaambia wananchi kuwa wasichukue tahadhali zozote baada ya sala hizo ni makosa makubwa sana.Katika kugawa chanjo ya Covid, inawezekana Tanzania haitapata chanjo yoyote kwa vile tunadai hatuna Covid. Lakini ukweli ni kuwa Tanzania hatuishi kisiwani; kama Kenya na Rwanda wana ugoinjwa huo, ni lazima na sisi tutakuwa nao japo kwa viwango tofauti kulingana na life styela za jumuia zetu. In fact Tanzania tunaweza kuwa nayo kubwa sana, ingawa siyo lazima tuwe na vifo vingi lakini baada ya muda madhara yake yataonekana. Hii Ostrich philosophy ya kuficha kichwa kwenye mchanga kutomuanoa adui yako siyo suluhu.
Hilo la demokrasi nakuachia kwa sababu mbili. Hakuna chama chochote cha upinzani kinachoonyesha kuwa na demokrasi ndani yake: Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa CHADEMA, Zitto ni Supreme Leader wa ACT wazalendo ambaye hachaguliwi. Kwa hiyo wanapolalamika kuhusu demokrasi, jibu lake ni kwamba huenda hawajui maana ya demokrasi ni nini- wanadhani demokrasi ni kwa vyama vyao kushindwa uchaguzi. Ni hivyo vilio vyao ndivyo vinakuwa reflected hapa JF na wafuasi wao wengi. Pili, viongozi kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi siyo jambo la ajabu kwani katiba inaruhusu.