Adui wa legacy ya Rais Magufuli: Kuminya Demokrasi au kushindwa kudhibiti maambukizi ya Corona?

Adui wa legacy ya Rais Magufuli: Kuminya Demokrasi au kushindwa kudhibiti maambukizi ya Corona?

Ni kwasababu hatujuani ila inaonyesha huna akili.

Hakuna chombo Cha habari kitaripoti ishu ya korona itakayosemwa na opposition.

Kiufupi tuko 2021 ila tumelazimishwa kuishi miaka ya 1943.

Adui wa JPM ni yeye mwenyewe. Hashauriki na hapangiwi watu pekee anaowagwaya ni jwtz kwasababu anawaelewa.
kwani umekatazwa kuvaa barakoa, umekatazwa kujiwekea, lock down mkuu? Acha unafiki
 
Mambo mengi mnayotaja yananweza kuwa ni mambo makubwa kweli lakini siyo mambo transitional yaliyojitokeza ghafla bila control ya serikali yake; hayaingii kwenye record ya legacy yeyote. Legacy ya George Bush marekani hisyo wizi wa kura uliompa madaraka, uingiliaji wa uhuru wa watu alioleta kutokana na patriot act, au tengano aliojenga baina ya democrats na republicans; la! Legacy yake inapimwa na mambo mawili tu, alivyosimamia nchi wakati wa janga la katrina, na alivyoongoza nchi baada ya 9/11 ikiwa ni pamoja na kupeleka nchi vitani.
Basi Maduhu hataacha Legacy yotote sababu hakuna jambo transitional amesimamia vizuri.
1. Tetemeko Bukoba
2. Corona
3. Mafuriko kila siku Dar es salaam tangu akiwa waziri wa mabarabara N.K
 
Chuki zote zinasababishwa na JPM anatibua maisha ya watu na kusababisha tuukumbuke utawala wa KIKWETE a.k.a utawala wa mafisadi
 
Mleta mada COVID si issue Tanzania, ilishaombew na Mungu anesikiliza sala zetu kuliko hata sala za Baba Mtakatifu kule Rome aliyasikia maombi yetu. Italy pamoja na idadi ya watawa waliokua nao lakini COVID iliwachapa haswa.

Demokrasia Tanzania ni kubwa sana. Viongozi wa juu karibu wote walipita bila kupingwa katika majimbo yao ilhali wapinzani wao wakibambikiwa kesi za jinai.

Kuombea Covid kwa sala siyo jambo baya, lakini kuwaambia wananchi kuwa wasichukue tahadhali zozote baada ya sala hizo ni makosa makubwa sana.Katika kugawa chanjo ya Covid, inawezekana Tanzania haitapata chanjo yoyote kwa vile tunadai hatuna Covid. Lakini ukweli ni kuwa Tanzania hatuishi kisiwani; kama Kenya na Rwanda wana ugoinjwa huo, ni lazima na sisi tutakuwa nao japo kwa viwango tofauti kulingana na life styela za jumuia zetu. In fact Tanzania tunaweza kuwa nayo kubwa sana, ingawa siyo lazima tuwe na vifo vingi lakini baada ya muda madhara yake yataonekana. Hii Ostrich philosophy ya kuficha kichwa kwenye mchanga kutomuanoa adui yako siyo suluhu.

Hilo la demokrasi nakuachia kwa sababu mbili. Hakuna chama chochote cha upinzani kinachoonyesha kuwa na demokrasi ndani yake: Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa CHADEMA, Zitto ni Supreme Leader wa ACT wazalendo ambaye hachaguliwi. Kwa hiyo wanapolalamika kuhusu demokrasi, jibu lake ni kwamba huenda hawajui maana ya demokrasi ni nini- wanadhani demokrasi ni kwa vyama vyao kushinda uchaguzi. Ni hivyo vilio vyao ndivyo vinakuwa reflected hapa JF na wafuasi wao wengi. Pili, viongozi kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi siyo jambo la ajabu kwani katiba inaruhusu.
 
Kuombea Covid kwa sala siyo jambo baya, lakini kuwaambia wananchi kuwa wasichukue tahadhali zozote baada ya sala hizo ni makosa makubwa sana.Katika kugawa chanjo ya Covid, inawezekana Tanzania haitapata chanjo yoyote kwa vile tunadai hatuna Covid. Lakini ukweli ni kuwa Tanzania hatuishi kisiwani; kama Kenya na Rwanda wana ugoinjwa huo, ni lazima na sisi tutakuwa nao japo kwa viwango tofauti kulingana na life styela za jumuia zetu. In fact Tanzania tunaweza kuwa nayo kubwa sana, ingawa siyo lazima tuwe na vifo vingi lakini baada ya muda madhara yake yataonekana. Hii Ostrich philosophy ya kuficha kichwa kwenye mchanga kutomuanoa adui yako siyo suluhu.

Hilo la demokrasi nakuachia kwa sababu mbili. Hakuna chama chochote cha upinzani kinachoonyesha kuwa na demokrasi ndani yake: Mbowe ni mwenyekiti wa maisha wa CHADEMA, Zitto ni Supreme Leader wa ACT wazalendo ambaye hachaguliwi. Kwa hiyo wanapolalamika kuhusu demokrasi, jibu lake ni kwamba huenda hawajui maana ya demokrasi ni nini- wanadhani demokrasi ni kwa vyama vyao kushindwa uchaguzi. Ni hivyo vilio vyao ndivyo vinakuwa reflected hapa JF na wafuasi wao wengi. Pili, viongozi kupita bila kupingwa kwenye uchaguzi siyo jambo la ajabu kwani katiba inaruhusu.
Wananchi kibao hatuna vyama, na tunataka demokrasia iwepo nchini.

Kutokuwepo kwa demokrasia katika vyama mbalimbali vya siasa nchini haimpi uhalali Magufuli kutoheshimu demokrasia aliyoapa kuilinda pindi alipoapa kuheshimu katiba.

Two wrongs don't make it right
 
Ni kwasababu hatujuani ila inaonyesha huna akili.

Hakuna chombo Cha habari kitaripoti ishu ya korona itakayosemwa na opposition.

Kiufupi tuko 2021 ila tumelazimishwa kuishi miaka ya 1943.

Adui wa JPM ni yeye mwenyewe. Hashauriki na hapangiwi watu pekee anaowagwaya ni jwtz kwasababu anawaelewa.
Malizia tu mkuu, anaogopa watamwondoa madarakani
 
Wananchi kibao hatuna vyama, na tunataka demokrasia iwepo nchini.

Kutokuwepo kwa demokrasia katika vyama mbalimbali vya siasa nchini haimpi uhalali Magufuli kutoheshimu demokrasia aliyoapa kuilinda pindi alipoapa kuheshimu katiba.

Two wrongs don't make it right
Kama huna chama, na ulipiga kura ni wapi ulipokosa demokrasi. Maana halisi ya demokrasi ni utawala uliochaguliwa na watu. Na vile vile katika uchaguzi huo, kura za wengi nzizo zinatoa uamuzi. sasa iwapo ulipiga kura, halafu mtu uliyempigia kura hakupigiwa na wengi, basi kubali kuwa ndiyo hivyo demokrasi inavyofanya kazi.

malalamiko mengi ya demnokrasi hutoka kwa viongozi walioshindwa uchaguzi, hayatoki kwa waliopiga kura! Halafu kwangu mimi kwa vile malalamiko hayo yapo tangu nchi inaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, ndiyo maana siyaoni kama ni Legacy ya Magufuli. Hakuna uchaguzi ambao wapinzani waliwahi kukubali kushindwa!.
 
Behaviourist , Taisho fuyaki , Bengal , REALNEGRONEVABROKE Idugunde
Majibu yenu nyote kwenye thread hii ni ya watu wa aina moja wanaotasoma mambo wakitegemea wasome wanayotaka. Ni watu wenye akili zilizodumaa ambazo kila siku zinataka kulishwa mambo ya aina ile ile aliyozowea
Wewe ndiye unaetaka kusoma mambo unayoyataka ndiyo maana ukikutana na mawazo tofauti tofauti kutoka kwa watu uliotutaja hapo juu inakuvuruga akili na kuishia kutulaumu!Tuna uhuru wa kuchangia kulingana na maono yetu,hakuna wa kutupangia cha kuchangia.
 
Haiwezi tokea, Mungu apendi ujinga, wala mtu asiye na maarifa ikiwa amekupa akili utaki tumia!
 
Mleta mada COVID si issue Tanzania, ilishaombewa na Mungu anesikiliza sala zetu kuliko hata sala za Baba Mtakatifu kule Rome aliyasikia maombi yetu. Italy pamoja na idadi ya watawa waliokua nao lakini COVID iliwachapa haswa.

Demokrasia Tanzania ni kubwa sana. Viongozi wa juu karibu wote walipita bila kupingwa katika majimbo yao ilhali wapinzani wao wakibambikiwa kesi za jinai.
Na soon tutawaombea na Wenzetu, lakini ngoja kwanza iwachape chape.
 
Hee! Hata huko wanaiba kura? Kumbe Trump anaweza kuwa kaibiwa kweli.
Kesi ya wizi wa kura mwaka 2000 huko Florida inajulikana sana. In fact haukuwa "wizi" kama unavyadhani au kama Trump anavyoaminisha watu, bali ule ulikuwa ni udanganyifu wa kuacha kuhesabu kura za Al Gore ambao ulifanywa na mdogo wake Jeb Bush ambaye aliikuwa Gavana wa Florida wakati huo pamoja na Catherine Harris aliyekuwa Secretary of state wa Florida. Trump anadai kuwa kuna kura ambazo hazikuwa halali zilihesabiwa jambo ambalo siyo kweli bali anataka kura za mwenzake zisihesabiwe kama ilivyofanyika wakati huo huko Florida.
 
Wewe ndiye unaetaka kusoma mambo unayoyataka ndiyo maana ukikutana na mawazo tofauti tofauti kutoka kwa watu uliotutaja hapo juu inakuvuruga akili na kuishia kutulaumu!Tuna uhuru wa kuchangia kulingana na maono yetu,hakuna wa kutupangia cha kuchangia.
Hujazuiwa kuchangia, lakini elewa kuwa kuchangia mada na kumshambulia mtoa mada ni vitu viwili tofauti. Jibu langu hilo ni response ya mliyoandika kuhusu mimi, siyo mlioyoandika kuhusu mada; wale wote walioandika kuhusu mada nimewajibu tofauti katika post nyingine.
 
Kama huna chama, na ulipiga kura ni wapi ulipokosa demokrasi. Maana halisi ya demokrasi ni utawala uliochaguliwa na watu. Na vile vile katika uchaguzi huo, kura za wengi nzizo zinatoa uamuzi. sasa iwapo ulipiga kura, halafu mtu uliyempigia kura hakupigiwa na wengi, basi kubali kuwa ndiyo hivyo demokrasi inavyofanya kazi.

malalamiko mengi ya demnokrasi hutoka kwa viongozi walioshindwa uchaguzi, hayatoki kwa waliopiga kura! Halafu kwangu mimi kwa vile malalamiko hayo yapo tangu nchi inaingia kwenye mfumo wa vyama vingi, ndiyo maana siyaoni kama ni Legacy ya Magufuli. Hakuna uchaguzi ambao wapinzani waliwahi kukubali kushindwa!.

Ule ulikuwa uchaguzi au maigizo?

Demokrasia siyo uchaguzi peke yake, ni pamoja na uwanja mpana wa kufanya shughuli za kisiasa.
Kama unamanipulate tume
Unaonea wapinzani kwa kuwaengua kihuni.
Unawazushia kesi za kubambika critics.
Unatumia usalama kuvuruga chaguzi.

Kuna demokrasia hapo?
 
Hujazuiwa kuchangia, lakini elewa kuwa kuchangia mada na kumshambulia mtoa mada ni vitu viwili tofauti. Jibu langu hilo ni response ya mliyoandika kuhusu mimi, siyo mlioyoandika kuhusu mada; wale wote walioandika kuhusu mada nimewajibu tofauti katika post nyingine.
Unamaanisha kuwa mtu mpumbavu au mjinga hapaswi kuambiwa kuwa ni mpumbavu/mjinga?Unamaanisha kuwa mtu mpumbavu au mjinga akiambiwa ukweli kuwa ni mpumbavu/mjinga hiyo inakuwa ni personal attack?
 
Watu wengi kwenye kambi ya upinzani wamekuwa wanadai kuwa Magufuli kabinya demokrasi ilihali huwa wanashiriki uchaguzi na ama wanashinda au wanashindwa kama ilivyo ada ya demokrasia. demokrasia haiana maana kuwa upinzani ndio ushinde tu.

Viongozi huwa hawapimwi kwa mambo ya kawaida bali yale ya kupita (transitional). Jambo transitional ambalo litamhukumu sana Maguful ni jinsi alivyosimamia maambukizi ya Korona. Amelisimamia vibaya sana kiasi kuwa hata wafuasi wake wanaweza kuwa wanakufa bila kujua kuwa wana virusi vya korona. Alizima information yoyote inayohusu korona, na kusahahu kuwa information is power.

Wakati wa ujana wetu (pamoja na yeye) tulipewa information zote kuhusu AIDS na ilitusaidia sana kujua jinsi ya kuikwepa. Sasa hivi information ya Corona haipo kabisa, na watu hawajui namna ya kuikwepa.

Watu wanajoifanya kuwa wanajua kusimamia interests za Watanzania wote wanapiga kelele kwa mambo yanayowahusu interests zao tu, kama kuruhusiwa kufanya maandamano, ambacho siyo kipimo kabisa che demokrasia, lakini sijasikia hata mmoja akizungumzia uongozi wa hili la korona linalohusu umma wa Watanzania wote. Hata wanaoliongelea, wanatumia njia hiyo hiyo ya kuhimiza maslahi yao binafsi.
Kama umeelimika basi ni nusunusu.
Huji kitu kuhusu demokrasia.Use etymology to learn about democracy.
 
Unamaanisha kuwa mtu mpumbavu au mjinga hapaswi kuambiwa kuwa ni mpumbavu/mjinga?Unamaanisha kuwa mtu mpumbavu au mjinga akiambiwa ukweli kuwa ni mpumbavu/mjinga hiyo inakuwa ni personal attack?
Hiyo siyo mada.

Ni kawaida sana kwa watu wajinga na wapumbavu kudhani kuwa wengine ndio wapumbavu zaid yao!. Maneno yako ni reflection hiyo. Uliambiwa kuwa unapomnyooesha mwenzako kidole chapete, vile vingine vyote vinakuwa vinakuoonyesha wewe mwenyewe. Ukishakuwa na busara hiyo utabadili lugha zako kuhusu watu wengine.
 
Kama umeelimika basi ni nusunusu.
Huji kitu kuhusu demokrasia.Use etymology to learn about democracy.
Hujaongea kitu chochote kujibu mada hii; demokrasi msingi wake mkuu ni huo wa utawala wa haki uliochaguliwa na watu.
 
Back
Top Bottom