Adult Talks: Kwa kupitia ndoa yako. Unawashauri vipi ambao hawajaoa?

Adult Talks: Kwa kupitia ndoa yako. Unawashauri vipi ambao hawajaoa?

Bible kwenye Mithali 5 nadhani kuna mistari inasema hivi "heri kuwa wawili kuliko mmoja maana wapata ijara njema kwa Bwana, tena walalapo wawili wanaweza kupata joto, ni rahisi kuvunja kijiti kimoja kuliko vitano" haya maneno hayako hivyo ila yapo kwa mtindo huo.
Nadhani wengi wanapenda kuoa mapema, ila mazingira ndio yanawabana. Ni nadra sana kukuta mwanaume anaoa ni early 20's. Ila all in all unachoongea ni points.
 
Big mistake unatakiwa ufanye vitu ambavyo unaweza kuvimaintain ili baadae isilete mtafaruku ukiwa huvifanyi ndio unaonekana muongo kwasababu rangi zako za ukweli zinaanza kuonekana!Kwenye mahusiano yote nashauri watu wawe wakweli na wawazi iwezekanavyo!
Nimekuelewa sana dada angu.
 
You can read all about marriage but the real test is when you get married and your marriage lasts 5-8 years.
Ndio maana nikasema, real life experience ni muhimu sana, thats why nikataka kujua kutoka kwa wadau waliopo kwenye ndoa tayari.
 
Yes brother, mpaka unakuta baba na mama zetu wanafanya jubilee ya miaka 40 ya ndoa, haloo sio mchezo hata kidogo. Kunakuwaga na ups na downs nyingi sana zimetokea hapo kati lakini wanazidi kuvumiliana kwa maana kila mmoja ni size sahihi ya mwenzake.
Nimekuelewa vizuri mkuu.
 
Nadhani wengi wanapenda kuoa mapema, ila mazingira ndio yanawabana. Ni nadra sana kukuta mwanaume anaoa ni early 20's. Ila all in all unachoongea ni points.
Watu wanaamini eti hadi uwe na nyumba, uwe na gari, sijui uwe na uwekezaji gani ndio uoe. Kwa mtazamo wangu ni mistake kubwa sana ila kwa leo wacha tumalize kwanza Idd
 
Ushauri wa bure kwa vijana wa kike na wa kiume ukiwa upo katika harakati za kutafuta jiko hakikisha unaoa/unaolewa mtu ambae unaweza kuvumiliana nae na anayekubali mapungufu yako na anakukubali jinsi ulivyo(anakuheshimu).

Muhimu kati ya yote upendo uwe nanga kuu.

Mkiwa katika mahusiano be yourself's usijifanye kila kitu kiwe perfect kuridhisha upande mwengine (fake personality) show your true selfbeing.Hakuna aliyekamilika ila mwenye upendo wa dhati atakukubali jinsi ulivyo.
Facts
 
Kila kitu na zama zake. urahisi wa ndoa ni lazma awepo muongozaj na muongozwaji, yan master and servant. sasa zama hizo ndo zimeyeyuka! ugum wa ndoa uko hapo. mana neno kuvumiliana linalohubiriwa linamaanisha kuacha hiki au kufanya kile kwa furaha ya mtu mwingine. jambo la uhakika la kuhubiriana kwa sasa ni kila kiumbe na kiwajibike kukabiliana na changamoto za asili za kuishi, katika usawa.
 
Kila mtu aingie ili akutane nayo huko, hakuna pie katika ndoa, kila ndoa ni unique na ina experience yake tofauti na nyingine.

Ila ukiingia kwa ndoa, epuka kuongea madhaifu ya mwenzako kwa wengine, hata watu wako wa karibu.
 
Ndoa bhana ni kitu tata sana wakuu!!!!mtu aoe kwa matakwa yake na si kulazimishwa.

Mimi nimeishi na mwanamke kwa miaka 8 ila nimemuacha yapata miezi 3 sasa na siku 4.tulibahatika kupata watoto 2(ke/me),ila changamoto mi nilikuwa nazo tangu mwanzo huku mwisho uvumilivu ukanishinda ikanibidi kila mmoja achukue hamsini zake.

Mwanamke hakuna unachompa akafanikiwa.ni lazima afeli,hajui kujisimamia ila haya yote niliyakubali sababu ni chaguo langu mwenyewe sikulazimishwa na mtu.
Watoto hawajawahi kuuliza mama yuko wap na anarudi lini daaah🤣🤣🤣🤣
 
Achana na ile misemo ya mtaani, kwamba kama unapata kila kitu kwenye mahusiano, basi ndoa haina umuhimu. Au wale wanaosema ukishamuweka ndani basi anaota mapembe.

Ukweli ni kwamba huwa inafikia point in this life unahitaji kusettle down. Kwamba hata kama ni kichomi au
Nitakupa elimu baadae nikiweka kfurushi maana Nina mi nimemezeshwa gb za kutosha kichwani
 
Sijamaliza kuisoma vizuri Ila Nina neno.

Clinging to people,ideas, expectations,events,outcome, tomorrow and yesterday is what brings sufferings in life.
Unakomaa ukiwa mdogo kuwa ukifanya ivi Kuna hili litatokea Ila mwishowe hulipati.
Dunia unachotakiwa uelewee haijakamilika pia mioyo ama nafsi zetu haziridhiki hata uzipe Nini.

Ivyoivyo don't expect much like happiness to be tied kwa mtu siku ukimfumania anaikatikia litango la mwingine Tena kitandani kwako ndo utakufa kwa presha .
Usiamini mtu amini aliyekuumba tu.
Mana mkewe anaweza akaolewa na jamaa akikuzidi pesa.
Ni Kama ridhiwani akitamka mkeo ama christianoRonaldo ama mesi akimpenda huko insta akamtumia mwaliko ili apewe viza na milioni 500 awajengee wazazi wake nyumba ya maana waishi akija kumtembelea afikie mahali pazuri.
Na tiketi ya ndege akamtumia. Pia na poketi money yake Kama 200M. Walahi anakuacha mchana kweupe kabisa.

So don't expect much from people,even your parents or children.
Hakuna Cha Mana kuwa ukioa Kuna kigeni maisha yanabaki kuwa maisha ama watu wanabakia kuwa ni watu nothing more nothing less.
 
Ninachofahamu mimi ni kwamba, kila mwanamke (mwanadamu) ana changamoto zake lakini mke mwema ni yule ambaye unaweza kubebeana changamoto zenu. Kama hauwezi kuzibeba changamoto zake achana naye huyo sio ubavu wako.

Kama unamjua tangia kipindi cha uchumba kwamba yeye ni mvivu/mchoyo lakini unaweza kuvumilia uvivu/uchoyo wake, basi huyo ndio size yako, mchukue kaa naye.

Yangu mimi ni hayo tu kaka mkubwa.
Njoo chukua zawadi aiseee
 
Ndoa hazikosi changamoto ,uvumilivu Jambo la muhimu Cha msingi tafuta mtu anaye kuelewaa madhaifu yako kwa at least 2/3.
 
1. Mwenza wako ni binadamu. Usimuamini asilimia zote hata kwa jambo dogo tu la kukusaidia, anaweza asijali.

Uweke mipaka binafsi ya vitu ambavyo waweza kuvibeba au kuvumilia. Vingine ikiwezekana mweleze mapema kabisa.

2. Kuna vitu kumhusu unaweza usijue kabla. Au ufikiri kwa zile heri zake anaweza akukugaia au kukusaidia kiroho safi. Kuna vitu waweza usivijue hadi kaburini.
Jitahidi uhusike na nafsi yako uwezavyo. Ukipata msaada au push iwe heri. Ukikosa usiache kuzitafuta heri zako kisa huna support.

3. Watu hubadilika kwa namna zote. Haswa wanapokutana na mazingira yanayowaumiza au pale wakikutendea wema na wewe usirejeshe basi mambo yanabadilika.
Jitahidi kujifunza kurejesha wema uwezavyo. Jitahidi usiwe chanzo cha mwenzio kuwa mbaya. Hapatakalika.

4. Mara nyingi mambo huenda ndivyo sivyo. Kumbukumbu za fadhila za mwenza wako ndio zitakazofuta machozi nyakati za maumivu. Ni vizuri ukatengeneza nyakati za heri au uwepo wakati anakuhitaji zaidi ili muongeze kibaba cha kumbukumbu nzuri za kufutia machozi.

5. Jifunze, usiige kwa kucopy and paste. Wakati mwingine utalazimika kujifunza vitu vya kawaida ambavyo ulitegemea mwenza wako atakufanyia na asiweze au asipende kufanya. Yaliyowezekana kwa wengine yawezekana kwako yawe kaa la nyongeza kwenye moto.
 
Back
Top Bottom