Adult Talks: Kwa kupitia ndoa yako. Unawashauri vipi ambao hawajaoa?

Ushauri wa bure kwa vijana wa kike na wa kiume ukiwa upo katika harakati za kutafuta jiko hakikisha unaoa/unaolewa mtu ambae unaweza kuvumiliana nae na anayekubali mapungufu yako na anakukubali jinsi ulivyo(anakuheshimu).
Sasa utamjuaje mtu ambaye unaweza kuvumiliana kabla ya kuishi naye ?
 
Nukta ya 2,4 na 5,umeandiks uongo wa wazi walio kinyume chake wanalia na kusaga meno.

Mimi mke wangu mkubwa nimetafutiwa,ni goli kipa na sijawahi kuishi nae kinyumba na bado tuko pamoja.

Shida yenu vijana hamjui ni watu gani sahihi wa kuwakabidhi mambo yenu.

Shukrani.
 
Mkuu huu uzi hauwezi kuisha bila mimi kutoa shuhuda na darasa kwa vijana....

Ngoja tumalizie pilika za eid el-fitir kwanza..

Nakubali mkuu Analyse
 
Mkuu according to your marriage experience, unatoa ushauri gani kwa ambao bado hawajaingia kwenye ndoa?
 
Ikitokea mtu anataka kuoa/kuolewa leo, then akaomba ushauri wako. Using your marriage as example, utamshauri nini?
 
Kila mtu aingie ili akutane nayo huko, hakuna pie katika ndoa, kila ndoa ni unique na ina experience yake tofauti na nyingine.

Ila ukiingia kwa ndoa, epuka kuongea madhaifu ya mwenzako kwa wengine, hata watu wako wa karibu.
Sawa chief
 
Watu wanaamini eti hadi uwe na nyumba, uwe na gari, sijui uwe na uwekezaji gani ndio uoe. Kwa mtazamo wangu ni mistake kubwa sana ila kwa leo wacha tumalize kwanza Idd
Idi ikiisha, uje na nondo zaidi cheif
 
Kwa wanaume: Ukishaoa, usichepuke. Ukithubutu, kujinasua ni kazi kubwa sana. Na zaidi, usiombe uzae tena huko nje......shida sana.

Sawa sawa?
Sawa chief.
 
Mkuu according to your marriage experience, unatoa ushauri gani kwa ambao bado hawajaingia kwenye ndoa?
Nawashauri vijana kwanza wabalishe tabia,kama wana tabia mbaya zote waziache kisha waanze kutafuta wenza wenye tabia nzuri.

Lingine vijana wawahi kuoa katika raha miongoni mwa raha za dunia ni kuoa mapema yaani katika umri mdogo.
 
Ndoa Ndoa Ndoa , nakuita hunisiniki kwa nn lakini,hapo zamani ulikuwa ukiitwa mara moja unakuja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…