Adv. Bashir Yakub: Tatizo siyo Law School

Adv. Bashir Yakub: Tatizo siyo Law School

Linguistic

JF-Expert Member
Joined
Mar 16, 2021
Posts
3,669
Reaction score
8,268
TATIZO SIO LAW SCHOOL.

Tatizo ni vyuo vya sheria. Tatizo linaanza na sifa za udahili wa wanafunzi wanaostahili kusomea sheria katika vyuo, na Pili mfumo wa ufundishaji vyuoni.

Kuna vyuo hadi mwenye D flat, D English, D kiswahili na D history anapata na nafasi ya kusoma sheria.

Sasa hivi karibia hamna chuo hakitoi degree ya sheria. Chuo hata kikiwa kipya moja ya kozi ambazo wanaanza nazo na ya sheria lazima iwemo.

Mchanganyiko huu hauwezi kuwa salama ukifika Law School ambapo maadili na taaluma ya sheria inasimamiwa kwa uthabiti.

Hatusemi vyuo vya sheria visiwe vingi ama watu wasidahiliwe kwa wingi, tunazungumzia ubora wa vyuo hivyo katika kutoa taaluma hiyo, na ubora wa wadahiliwa wenyewe.

Niwaambie kitu, asilimia 90 ya wanafunzi wanaomaliza sheria katika vyuo vyetu hawawezi hata kuandaa kiapo(affidavit). Kiapo tu.

Simsingizii mtu, mahakimu na mawakili mnaokaa na wanafunzi hao wakija field mnajua na mmekuwa mkikilalamika sana kuhusu hili.

Nazungumzia kiapo wala sizungumzii kuandaa mashitaka(Plaint au Charge) au utetezi( Wsd), kiapo tu hawajui.

Mtu kama huyu unataka Law School iseme amefaulu, ili akafanye nini mtaani. Akatoe huduma gani.

Kuna kitu jamii inapaswa kuelewa. Law School haizalishi tu Mawakili bali Mahakimu na Majaji. Tokea ilipoanzishwa hawi mtu Hakimu ama Jaji isipokuwa amefaulu Law School.

Unaonaje mtu kama Jaji ama hakimu mwenye mamlaka ya kuhukumu mtu kunyongwa hadi kufa, kuhukumu kifungo cha maisha jela, kifungo cha miaka 30, kuhukumu upoteze nyumba ama mali yako nk awe mtu aliyefaulu kiujanjaujanja tu ilimradi. Haiwezekani

Law School inahiaji watu "Pure" na wala haimuonei yeyote. Inahitaji watu ambao watabeba majukumu mazito kama hayo niliyoainisha hapo juu.

Hayo majukumu ni mazito sawa na ya udaktari. Ni majukumu ambayo mstari wake ni kati ya kifo na uhai.

Wanafunzi wenyewe wanajua na ndio maana wakifeli wanakimbilia kwenye media. Zipo taratibu za rufaa kwa waliofeli lakin hawataki kuzitumia sababu wanajua hawatatoka kutokana na ukweli. Wanajua kabisa wamefeli kwasababu hawajaiva inavyostahili.

Na suala la kuhakikisha Wakili anaiva vizuri kabla ya kuapishwa halijaanza na Law School. Lilikuwepo hata kipindi cha Bar Exam kabla Law School haijaanzishwa. Mwendo ulikuwa huu huu. Waulizeni waliopitia mfumo huu wa Bar Exam watakuelezeni. Mtu alikuwa akirudia mitihani hii hata mara 15 ili aweze kufaulu na kuapishwa kuwa Wakili.

Lengo ni hilohilo kumuandaa mtu sahihi atakayebeba haya majukumu mazito ya kifo na uhai.

Kwa ufupi, kama kuna sehemu ya kushugulikia kuondokana na kadhia hii ni vyuo vya Sheria. Mifumo ibadilike kuanzia sifa za udahili hadi ufundishaji.

Sifa za udahili wa shetia zimeshushwa mno, Pili Wajitoe katika kufundisha Theory na wajikite katika Practical. Law is about practise 80% and theory 20%.

Tusitafute mchawi Law School. Na ukitaka kujua ukweli wa hili ni nadra mno tena mno mtu ambaye amemaliza chuo akapractise kwa muda aidha kwa mawakili au mahakamani then akaenda Law School, kumkuta amefeli.

Hao wachache mnaosikia wanafaulu wengi sio fresh from school. Ni watu ambao wametoka ofisi za mawakili au wamepractise mahakamani.

Hawa wa kutoka chuo moja kwa moja Law School hufeli karibia wote, itokee tu.

Kwahiyo ni muhimu kuangalia hayo mambo mawili, Kwanza sifa za udahili wa wanafunzi ambao wanatakiwa kusomea sheria, Pili mfumo wa vyuo ubadilike kutoka theory na kuwa practical zaidi.

Tuachane na Law School iandae watu Mahiri. Tunahitaji watu mahiri wabebe majukumu mazito ya kifo na uhai.
 
Umeandika vizuri sana, una hoja ya msingi umeandika. Good!:

swali: Mbona majaji/mawakili wanafanya vitu vya hovyo? Nimesoma sana Law reports zetu, mengine huwezi kuamini kuwa hiii kesi ilisimamiwa na wakili aliyefuzu Law school au Bar exams!

Hata leo tunawaona majaji wa UPE! wapo sana! Kiingereza utakimbai! wapo sana!

2. Ina maana hakuna chuo kinachopokea watoto wazuri ? Hakuna shule zenye watoto wazuri huko sekondari? Ina maana vyuo vyote tanzania nzima at that particular time ilikuwa na watoto wazuri 26 tu ie wote waliosoma sheria only 26 were good upstairs?
 
Nadhani mfumo wa ufundishaji vyuoni sio Sheria tu hata kada zingine walimu wanaegemea Sana nadharia kuliko vitendi.

Matokeo yake mhitimu anakuwa mzuri kwenye nadharia kuliko kufanya kwa vitendo.

Hili ni tatizo kwa Taifa.

Elimu yetu ni tatizo
 
Umenena vyena kabisa kijana anafauli kidato cha nne napata division four anakuwa na D zake nne kisa nyumbani pesa ipo anaanza kusoma sheria certificate miaka miwili, anamaliza anaunga diploma miaka miwili anamaliza anaanza degree miaka mitatu mpaka minne akimaliza anaenda Law school

MY TAKE
Kwenye sheria waache kusoma kwa kufunga unga wafanye kama degree ya elimu huna elimu ya form six weee sahau kuhusu dregree ya uwalimu hii inaweza rekebisha kidogo.

Ndio maana hata sasa hivi kwenye elimu hawa vijana wanaoenda special diploma ya elimu kutoka kidato cha nne wakowa uko uko vyuo vya uwalimu wanapigishwa paper ya form six lengo wafit na diploma ya elimu.
 
Wakili Bashir Yakub amejielekeza vibaya na anatakiwa kupuuzwa kwa sababu zifuatazo.

Mosi , Kumeibuka wimbi la baadhi ya watu waliofaulu law school (mawakili) kuponda kwamba tatizo lipo kwenye vyuo vinavyoandaa wanafunzi wa sheria na sio law school.

Kama tatizo lipo vyuoni pekee Swali yeye amewezaje kuwa wakili? Ikiwa na yeye uwakili wake ameupata baada ya kuwa ameanzia kwenye vyuo hivyo hivyo anavyovisema vina matatizo?

Pili, Wakili Yakub amegusia alama za udahili wa watu wanaodahiliwa kwenda kusoma sheria kwamba wanachukua mpaka watu wenye alama D kwenye masomo yao hivyo hii inachangia watu kufeli law schoo, Hoja hii haikutakiwa kutolewa na mtu kama yeye ambae amesema ni wakili.

Kwa sababu inaonekana hana uelewa na jambo hili. Watu wote wenye alama D katika masomo yao ya kidato cha nne huwalazimu kwenda kuanzia ngazi ya cheti kwa mwaka mmoja, baadae huenda ngazi ya Diploma kwa miaka miwili na baadae hupata sifa za kwenda ngazi ya degree baada ya kuwa wamepata GPA ya 3+ na rekodi zinaonyesha watu hawa wamekuwa wakifanya vizuri

Kwani Yakub hajui kama unaweza kutoka form six na one ya point 7 na ukafika chuo ufaulu ukawa sio mzuri? Je hao wanafunzi wote waliofeli law school wote wana alama D? Yakub amejielekeza vibaya na je hata hizo taaluma zingine hajawahi kusikia daktari amefeli wakati udahili wao ni wa juu?

Tatu, anasema saizi kila chuo kinatoa degree, kwa ufupi ni kwamba hakuna chuo kinachotoa degree vyuo vinatunuku degree huwezi kusema unaenda UDOM, UDSM au MZUMBE ukasema unaenda kupewa degree vyuo vinatunuku degree baada ya kuwa umepitia mafunzo waliyoyaweka ya kukupima. Hata yeye ndo njia hiyo hiyo aliitumia mpaka akawa wakili.

Anasema hata chuo kikiwa kipya kinaanza na kozi ya sheria , hii inaonyesha Yakub hajui kabisa vigezo vya chuo kukubaliwa kuanza kufundisha kozi flani angekuwa anajua asingesema hivyo. Upya wa chuo sio kikwazo cha chuo kufundisha sheria. Akasome sheria zinazoanzisha vyuo ili ajue.

Nne, anasema asilimia 90 ya wanafunzi wanaomaliza chuo hawajui kuandaa kiapo hili hajasema amefanya utafiti gani, Tanzania tuna vyuo zaidi ya 10 vinavyofundisha sheria ametumia utafiti upi kubaini hili au ameandika tu?

Tano, wakili Yakub anasema mawakili na mahakimu wamekuwa wakilalamika sana juu ya ubovu wa wanafunzi je ni kwa nini baadhi ya mahakimu hao pia wamekuwa wakifeli law school? Na je hakuna mawakili wabovu? Yakub anataka kuaminisha watu kuwa kila mtu aliyepita law school ni mwamba kitu ambacho sio kweli

Sita, Anasema Law School haizalishi mawakili tu, bali inazalisha majaji na mahakimu hii nakubali lakini je ndo iwe sababu ya kuponda wanafunzi wote na kumnyima nafasi ya kufungua akili yake ili ajue kama upande wa pili pia kuna tatizo? Yeye ni wakili anajua kuwa tuna mahakim na majaji wengi ambao walishapita hapo law school lakini bado ukisoma judgement’s zao utakuta kuta shida ya kisheria? Je hajawahi kuona kitu kama hiki?

Anasema law school inahitaji watu pure je yeye ni pure ? Ni kweli ni jambo jema kupata watu pure je Toka ametoka law school anataka kusema anajua kila kitu kwenye sheria?

Wakili Yakub asifunge akili na kuanza kuona waliopo chini wote hawana uwezo bali wenye uwezo ni wale tu waliofaulu law school kitu ambacho sio kweli.

Unaweza kwenda law firm’s na mahakaman kufanya field na ukaenda law school ukafeli.

Ushauri wa Yakub umeegemea upande mmoja hajataka kabisa kuonyesha weaknesses za upande wa pili.
 
Kuna MDA mawakili tunaowaamini wanajizima data mpk unashindwa kuamini huko law school walienda kusomea Ujinga ama vipi?

Refer wale mawakili wa serikali kwenye ile kesi ya mbowe
 
Yule Jaji aliyemhukumu mtu kwa uchawi unamwambia nini? Ili hali sheria zetu haziamini uchawi? Mpaka mahakama kuu ikaitisha file haraka na kubadilisha hukumu?
Sheria zetu zinaamini uchawi.

Witch craft act ipo .

Ni story za mtaa tu kuwa serikali haiamini uwepo wa uchawi.

Na story zimesambaa nchi nzima kama uongo mwingine usambaavyo
 
HAYA NI MATOKEO YA WATU KUTUMIA SANA HIZI SIMU JANJA. WATU WANAPOTEZA UMAKINI. HIZ KITU ZINAELEKEA KUWA JANGA KUBWA SANA. HATA HUKO MAKAZINI KUNA WATU HAUWATOI KWENYE SIMU JANJA. WANAKESHA INSTA, TIKTOK NA MITANDAO MINGINE WAKIFATILIA UMBEA WA KUJUA LEO DAIMONDI SIJUI KATEMBEA NA NANI SIJUI KAJALA KAFANYA UPUUZI GANI YAANI NDOIVO.
 
Wanasheria wanaosoma school of law - wanafeli kwasababu moja TU
hawajui kingereza hayo mambo mengine mnatafuta Mtu wa kumtoa kafara nothing else!
Tuliza mshono wewe hujui unachoongea.

Wakati nipo hapo kuna mkufunzi mmoja alikuja kukokotoa swali alilokuwa ametoka kuwatungia Cohort ya mbele yetu likamshinda. Na hapo ameshakaa nalo mda mrefu.

Sasa jiulize mtu aliyekutana na swali hilo kwa mara ya kwanza na lilikuwa la lazima huku akikimbizana na mda.
 
Back
Top Bottom