Adv. Bashir Yakub: Tatizo siyo Law School

Mkimaliza kujadili matokeo ya Law school, Tujadili matokeo ya Cadre za Afya hasa hasa PST. Hayajatoka ila najua tu watakua wameharibu maana naona huko kwenye status updates zao ni vilio tu.
 
Na ndugu yangu anafundisha hapo anasema wanafunzi wengi vilaza hasa wanaotoka vyuo vyetu vya private.. Msingi wa mafunzo wao sio mzuri.. Sasa wanapokuja law school mambo yanakua magumu. Sasa sijui kamati itapia mitihani au itafanya mahojiano. Itafaa kama watapitia mitihani yao waone utopolo halisi na sio kutafuta mchawi
 
TATIZO SIO LAW SCHOOL.

Tatizo ni vyuo vya sheria. Tatizo linaanza na sifa za udahili wa wanafunzi wanaostahili kusomea sheria katika vyuo, na Pili mfumo wa ufundishaji vyuoni.

Kuna vyuo hadi mwenye D flat, D English, D kiswahili na D history anapata na nafasi ya kusoma sheria.

Sasa hivi karibia hamna chuo hakitoi degree ya sheria. Chuo hata kikiwa kipya moja ya kozi ambazo wanaanza nazo na ya sheria lazima iwemo.

Mchanganyiko huu hauwezi kuwa salama ukifika Law School ambapo maadili na taaluma ya sheria inasimamiwa kwa uthabiti.

Hatusemi vyuo vya sheria visiwe vingi ama watu wasidahiliwe kwa wingi, tunazungumzia ubora wa vyuo hivyo katika kutoa taaluma hiyo, na ubora wa wadahiliwa wenyewe.

Niwaambie kitu, asilimia 90 ya wanafunzi wanaomaliza sheria katika vyuo vyetu hawawezi hata kuandaa kiapo(affidavit). Kiapo tu.

Simsingizii mtu, mahakimu na mawakili mnaokaa na wanafunzi hao wakija field mnajua na mmekuwa mkikilalamika sana kuhusu hili.

Nazungumzia kiapo wala sizungumzii kuandaa mashitaka(Plaint au Charge) au utetezi( Wsd), kiapo tu hawajui.

Mtu kama huyu unataka Law School iseme amefaulu, ili akafanye nini mtaani. Akatoe huduma gani.

Kuna kitu jamii inapaswa kuelewa. Law School haizalishi tu Mawakili bali Mahakimu na Majaji. Tokea ilipoanzishwa hawi mtu Hakimu ama Jaji isipokuwa amefaulu Law School.

Unaonaje mtu kama Jaji ama hakimu mwenye mamlaka ya kuhukumu mtu kunyongwa hadi kufa, kuhukumu kifungo cha maisha jela, kifungo cha miaka 30, kuhukumu upoteze nyumba ama mali yako nk awe mtu aliyefaulu kiujanjaujanja tu ilimradi. Haiwezekani

Law School inahiaji watu "Pure" na wala haimuonei yeyote. Inahitaji watu ambao watabeba majukumu mazito kama hayo niliyoainisha hapo juu.

Hayo majukumu ni mazito sawa na ya udaktari. Ni majukumu ambayo mstari wake ni kati ya kifo na uhai.

Wanafunzi wenyewe wanajua na ndio maana wakifeli wanakimbilia kwenye media. Zipo taratibu za rufaa kwa waliofeli lakin hawataki kuzitumia sababu wanajua hawatatoka kutokana na ukweli. Wanajua kabisa wamefeli kwasababu hawajaiva inavyostahili.

Na suala la kuhakikisha Wakili anaiva vizuri kabla ya kuapishwa halijaanza na Law School. Lilikuwepo hata kipindi cha Bar Exam kabla Law School haijaanzishwa. Mwendo ulikuwa huu huu. Waulizeni waliopitia mfumo huu wa Bar Exam watakuelezeni. Mtu alikuwa akirudia mitihani hii hata mara 15 ili aweze kufaulu na kuapishwa kuwa Wakili.

Lengo ni hilohilo kumuandaa mtu sahihi atakayebeba haya majukumu mazito ya kifo na uhai.

Kwa ufupi, kama kuna sehemu ya kushugulikia kuondokana na kadhia hii ni vyuo vya Sheria. Mifumo ibadilike kuanzia sifa za udahili hadi ufundishaji.

Sifa za udahili wa shetia zimeshushwa mno, Pili Wajitoe katika kufundisha Theory na wajikite katika Practical. Law is about practise 80% and theory 20%.

Tusitafute mchawi Law School. Na ukitaka kujua ukweli wa hili ni nadra mno tena mno mtu ambaye amemaliza chuo akapractise kwa muda aidha kwa mawakili au mahakamani then akaenda Law School, kumkuta amefeli.

Hao wachache mnaosikia wanafaulu wengi sio fresh from school. Ni watu ambao wametoka ofisi za mawakili au wamepractise mahakamani.

Hawa wa kutoka chuo moja kwa moja Law School hufeli karibia wote, itokee tu.

Kwahiyo ni muhimu kuangalia hayo mambo mawili, Kwanza sifa za udahili wa wanafunzi ambao wanatakiwa kusomea sheria, Pili mfumo wa vyuo ubadilike kutoka theory na kuwa practical zaidi.

Tuachane na Law School iandae watu Mahiri. Tunahitaji watu mahiri wabebe majukumu mazito ya kifo na uhai.
Hili tatizo sio kada ya sheria tu, hata afya kuna vyuo kibao vinatoa degree na diploma za mambo ya afya na bila shaka hakuna ubora.
Serikali imeamua watu wengi isemekane wamesoma haijalishi elimu iwe na ubira au la
 
Nimeteta na wakili mmoja juu ya hili sakata la kufeli kwa wanafunzi wengi pale School of law... Nimeambiwa wanafunzi wengi wanayapuuza masomo ambayo kwa sehemu kubwa yanatokana na masomo walioyoyasoma kinadharia huko vyuoni walikohitimu....hapa hawatilii mkazo kwa kujiamini kuwa hayo masomo waliyasoma na wakayafaulu hivyo kwao ni vigumu kuyafeli ila wakiletewa mitihani yake yenye mitego kidogo kwa masomo hayohayo wanajikuta Wana angukia pua.

ila kubwa zaidi nimeng'atwa sikio kuwa wengi wanafeli sana SoMo la hesabu ambalo ni changamoto kwa wanasheria wengi ambao wao msingi wa taaluma yao ni masomo ya sanaa.
 
Na ndugu yangu anafundisha hapo anasema wanafunzi wengi vilaza hasa wanaotoka vyuo vyetu vya private.. Msingi wa mafunzo wao sio mzuri.. Sasa wanapokuja law school mambo yanakua magumu. Sasa sijui kamati itapia mitihani au itafanya mahojiano. Itafaa kama watapitia mitihani yao waone utopolo halisi na sio kutafuta mchawi
Acha umbea, vyuo vya private kwani kuna sehemu wanajaza vyuo walivyosoma? Acheni kusingizia vitu vya ajabu
 
Wanasheria wanaosoma school of law - wanafeli kwasababu moja TU
hawajui kingereza hayo mambo mengine mnatafuta Mtu wa kumtoa kafara nothing else!
Mkuu sasa wewe hata kiswahili kinakupa shida.

Jufeli❌
Wanafeli❌
Kingereza❌
 
Kwamba hawaelewi maneno kama pro bono, alibi, in absentia, a fortiori, ab initio, ab ab intra, actio personalis moritur cum persona, ex turpi causa non oritur actio, Amicus omnibus, amicus nemini
Inflaglento delecto

Res gastae

Ratio decidendai

Obita dicta

Onus of proband

Locus standai
 
Hapa watu washaingiza siasa ngoja vilaza waongezeke kwa kasi siasa haijawahi kusaidia elimu.
 
TATIZO SIO LAW SCHOOL.

Bashir Yakub, WAKILI.
+255 714 047 241.

Tatizo ni vyuo vya sheria. Tatizo linaanza na sifa za udahili wa wanafunzi wanaostahili kusomea sheria katika vyuo, na Pili mfumo wa ufundishaji vyuoni.

Kuna vyuo hadi mwenye D flat, D English, D kiswahili na D history anapata na nafasi ya kusoma sheria.

Sasa hivi karibia hamna chuo hakitoi degree ya sheria. Chuo hata kikiwa kipya moja ya kozi ambazo wanaanza nazo na ya sheria lazima iwemo.

Mchanganyiko huu hauwezi kuwa salama ukifika Law School ambapo maadili na taaluma ya sheria inasimamiwa kwa uthabiti.

Hatusemi vyuo vya sheria visiwe vingi ama watu wasidahiliwe kwa wingi, tunazungumzia ubora wa vyuo hivyo katika kutoa taaluma hiyo, na ubora wa wadahiliwa wenyewe.

Niwaambie kitu, asilimia 90 ya wanafunzi wanaomaliza sheria katika vyuo vyetu hawawezi hata kuandaa kiapo(affidavit). Kiapo tu.

Simsingizii mtu, mahakimu na mawakili mnaokaa na wanafunzi hao wakija field mnajua na mmekuwa mkikilalamika sana kuhusu hili.

Nazungumzia kiapo wala sizungumzii kuandaa mashitaka(Plaint au Charge) au utetezi(Wsd), kiapo tu hawajui.

Mtu kama huyu unataka Law School iseme amefaulu, ili akafanye nini mtaani? Akatoe huduma gani?

Kuna kitu jamii inapaswa kuelewa. Law School haizalishi tu Mawakili bali Mahakimu na Majaji. Tokea ilipoanzishwa hawi mtu Hakimu ama Jaji isipokuwa amefaulu Law School.

Unaonaje mtu kama Jaji ama hakimu mwenye mamlaka ya kuhukumu mtu kunyongwa hadi kufa, kuhukumu kifungo cha maisha jela, kifungo cha miaka 30, kuhukumu upoteze nyumba ama mali yako nk awe mtu aliyefaulu kiujanjaujanja tu ilimradi. Haiwezekani.

Law School inahiaji watu "Pure" na wala haimuonei yeyote. Inahitaji watu ambao watabeba majukumu mazito kama hayo niliyoainisha hapo juu.

Hayo majukumu ni mazito sawa na ya udaktari. Ni majukumu ambayo mstari wake ni kati ya kifo na uhai.

Wanafunzi wenyewe wanajua na ndio maana wakifeli wanakimbilia kwenye media. Zipo taratibu za rufaa kwa waliofeli lakini hawataki kuzitumia sababu wanajua hawatatoka kutokana na ukweli. Wanajua kabisa wamefeli kwasababu hawajaiva inavyostahili.

Na suala la kuhakikisha Wakili anaiva vizuri kabla ya kuapishwa halijaanza na Law School. Lilikuwepo hata kipindi cha Bar Exam kabla Law School haijaanzishwa. Mwendo ulikuwa huu huu. Waulizeni waliopitia mfumo huu wa Bar Exam watakuelezeni. Mtu alikuwa akirudia mitihani hii hata mara 15 ili aweze kufaulu na kuapishwa kuwa Wakili.

Lengo ni hilohilo kumuandaa mtu sahihi atakayebeba haya majukumu mazito ya kifo na uhai.

Kwa ufupi, kama kuna sehemu ya kushugulikia kuondokana na kadhia hii ni vyuo vya Sheria. Mifumo ibadilike kuanzia sifa za udahili hadi ufundishaji.

Sifa za udahili wa shetia zimeshushwa mno, Pili Wajitoe katika kufundisha Theory na wajikite katika Practical. Law is about practise 80% and theory 20%.

Tusitafute mchawi Law School. Na ukitaka kujua ukweli wa hili ni nadra mno tena mno mtu ambaye amemaliza chuo akapractise kwa muda aidha kwa mawakili au mahakamani then akaenda Law School, kumkuta amefeli.

Hao wachache mnaosikia wanafaulu wengi sio fresh from school. Ni watu ambao wametoka ofisi za mawakili au wame-practise mahakamani.

Back
Top Bottom