Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Usinikumbushe P. Diddy yule faza ni katili wa MECHANICS sijapata ona
 
Atakua T.O Martin Chegere huyo. Ndio najua ali wai kupata mshike mshike chuo kati yake na lectures...
 
Huyo dogo hakufukuzwa chuo kwa dharau ila alidisco kwa kushindwa ku manage time...
 
Physics advance ni Nouma,Unahitaji mkono mwepesi kusolve bila kuremba,Pia Unahitaji kufall in love naturally katika hisabati,
 
Ugumu wa Physics unategemea na Mwl ,sisi tulipata bahati miaka hy kufundishwa na Wamarekani (volunteers) yaani wako very simple na wana tactics nyingi na simple huwezi amini National exam kwa PCB , Physics na Biology watu ndio walifaulu mostly ,nilichojifunza walimu wa kibongo wana complicate sana mambo .
 
P. Diddy sijui atakuwa wapi sasa hivi ,Kinunda ,Mzee Maganga ,Kirumbuyo nk
 
Physics itabaki kuwa Story kwa wengi but ma TO wengi hutokea kombi ya pcm kwani ni rahisi kutransfer knowledge ya physics kwenda hesabu na chemistry.
 
Nimesoma Advanced Physics hivyo nakumbuka vizuri mziki wake, tena enzi hizo ukifika unapewa UP kama reference book pia kulikuwa na Nelkon 6th edition.

Physics noma sana. Ukitaka ujue Physics sio mchezo tembelea kwenye vyuo vikuu ulizia waosoma Physics kwa level zote iwe BSc, MSc na PhD yaani wa kutafuta. Nakumbuka kuna rafiki yangu alikuwa kwenye darasa la BSc (Education) waliokuwa wanasoma Physics na Maths ni wawili tu. Hao jamaa walikuwa hawalali jinsi Physics ilivyokuwa inawasumbua.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…