Deadbody umenichekesha sana na uandishi wako hasa ukizingatia nilikuwa nakumbuka matukio ya advance. Kwa kweli ile level ya elimu kwa masomo ya sayansi ni ngumu kupita hata masomo ya digrii ya kwanza (sijui kuhusu ya pili).
Old moshi hiyo,tulikuwa tunafundishwa na mwalimu (aka Pdiddy) ana sauti ndogo halafu ana aibu sana hivyo anaishia kusema na ubao tu. Mifano yake ubaoni mnaelewa vizuri tu sema sasa akiacha maswali unaona kama haukuwamo darasani vile.
Prep ya physics nikifanikiwa swali moja tu kutoka kwenye UP,siku imeisha maana nakuwa nimetumia si chini ya masaa 3-4 kupata ufumbuzi ukijumlisha na baridi la moshi ndio hamu ya kulalal inakuja haraka.
Nakumbuka tulikuwa na mshikaji wangu tukakubaliana kuuza godoro moja (tuwe tunatumia moja kwa zamu) ili kupunguza muda wa kulala ili fiziksi isitushinde lakini mwisho wa hakuna cha maana tulichopata.
Nadhani sitamshauri mwana familia wangu yeyote kusoma advance, ni kupoteza muda tu.