Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

physics_650x400_51489484821.jpg


5aeb30138efc5bd38c3a8aacd40cc677--projectile-motion-the-motion.jpg


Wakuu japo sijapost kwenye jukwaa hili kwa miezi kadhaa sasa hivyo naomba mnipokee tena mtaalamu Deadbody ,

Wakuu najua JF kuna watu wa kila aina ya masomo humu hivyo leo naomba niwakusanye watu wote waliosoma Advanced Physics tuje tukumbushie namna tulivyokuwa tunashangaa ndani ya chumba cha mtihani .

Ngoja nianze mimi aisee kuleta ushuhuda wangu wa kwanza kabisa:

Story inaanzia pale tu kijana Deadbody niliporipoti Advance school mara ya kwanza aisee ambapo nikapokewa kwa furaha sana na watu niliosoma nao Olevel na Primary.

Walinipokea kwa mbembwe sana maana balaa langu walikuwa wanalijua vizuri kuwa Physics na Maths niliumbiwa mimi(hahaha sipo serious hapa).

Nikapokelewa na kuonyeshwa Block nitakaloishi na maisha ya boarding ndio yakaanza rasmi .

TOPIC YA KWANZA KUFUNDISHWA KWA SOMO LA PHYSICS

Kama ilivyomazoea ya shule za advance kuwa walimu hukimbilia kuanza projectile motion,measurements and error hivyo ikawa hivyo hivyo kwa mwwalimu wetu ambaye alikimbilia kuanza na PROJECTILE MOTION.

ProjectileMotion.jpg


Dah aisee nilishangaa sana kuona topic hiyo ikifundishwa ndani ya siku moja na kuisha yote huku ikiwa na formula nyepesi mno kwa mwanafunzi kilaza kama Jesca kuelewa.

Formulas zilikuwa za Range ,height ambapo kila nikigusa swali kwenye kitabu cha CHAND linaenda natia tiki ,nikaanza kujiuliza kwanini watu wanasema hii topic ngumu mbona nimesolve maswali yote aiseeee..

Dah nikahitimisha tu kwa kujiona mimi ndio mwamba ,mwamba wa mathematics na sikwami kabisa swali la PROJECTILE MOTION .Wakati najitamba hivyo kumbe washikaji wananichora tu kuwa huyu dogo kaja kwa mbwembwe tumtazame kwanza ataishia wapi.

Projectile+motion.jpg


Mwendo ukawa ndio ule ule muhuni nikigusa tu maswali ya examples ya mwalimu napasua tena kwa muda mfupi tu.Na kwa jinsi nilivyokuwa na mbwembwe ilikuwa mtu akiniletea swali la projectile naliweka kwenye calculator lote then nikipiga alama ya sawa sawa kitu imooooo.Wenzangu wakawa wananiambia dogo fanya moja moja kupunguza brackets maana zitakuchanganya,ila kwakuwa nataka kuonyesha mimi ni kichwa sichanganywi nikawabishia na kuweka lote.

Aiseee nilikuwa mpenda sifa hatari enzi hizo kushinda hata BASHITE,nikasema likizo hii watanikoma mchikichini huko ndio nitakuwa nasolvia watu kwenye mabanda ya mihogo wakati wa kusubiri pindi .

Dah maisha yanaenda kasi sana na hatimaye nikapewa habari njema na mwanangu mmoja hivi kuwa kwa mgote jumamosi ni mtihani wa PROJECTILE MOTION hivyo nenda kawaonyeshe aisee kuwa wewe ni mwamba Dar nzima.Nikajawa na sifa kama kawaida yangu na kuwaza mda wote kuwa jumamosi inachelewa aisee nikafanye maajabu mchikichini huko.

SIKU YA MTIHANI WA PROJECTILE MOTION IKAFIKA

projectile_motion_prob_2.png


Kwa kujiamini kabisa nikakaa seat ya mbele kabisa maana nilikuwa sitaki mtu anichungulie tusije tukagongana marks tukawa wote wa kwanza wakati mimi nimetumia nguvu kubwa sana na nimekamia show.

Sitasahau hii siku hasa pale nilipoufungua mtihani wa PROJECTILE MOTION na kukutana na Concepts mpya ambazo sijawahi hata kuhisi kama nazo ni projectile aisee.

Kusoma swali hata halina terminologies ngumu kuelewa ila isipokuwa sina cha kuandika baada ya kulielewa lile swali.Hahahah formulas zangu za RANGE na Maximum height zote hazitumiki na ndio nazitegemea sasa hapo.

Ule mtihani na mimi tulikuwa level tofauti kabisa ambapo ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejifunza hesabu za kujumlisha namba zenye tarakimu moja then umtolee hesabu za magazijuto.

Ule mtihani haukuwa standard yangu japo majirani zangu wanaagiza karatasi za kujibia tu baada ya kujaza za mwanzo.Muhuni natamani nisikusanye niondoke hivyo hivyo ila sasa Mgote anayesimamia mtihani ndio kakaa mbele yangu kiasi kwamba hata nikigeuza jicho tu ananiona ,hhahah noma.

Nikakutana na concepts za kitu kina kuwa projected kutoka kwenye gari linaloenda kwa speed fulani na kitu chenyewe kina speed yake aiseee.Wakati huo air unaambia inaspeed yake then natakiwa kutafuta umbali kitakapotua kutokea umbali ambao gari lilikuwepo wakati wa kurushwa.

material-YTA5u3DP.png


Kila nikiangalia naona nashindwa hata kuchora mstari wa range maana kitu kilirushwa kikiwa kwenye height fulani above the ground.

Kiukweli hilo ndio baadae nikaja kugundua lilikuwa swali rahisi kuliko mengine.Hayo mengine ilikuwa balaaa tupu maana hadi ndege wa angani waliokuwa wanatembea walipishana na hiko kitu walichokiproject tena kwa speed tofauti.

Mfano swali lingine lilikuwa linaanzia mbali kinouma kuwa ,ball imeenza kuserereka kwenye umbo lina shape ya U na kuibuka juu na kuendelea na projectile motion na mara gafla ukagongana na body nyingine huko juu hivyo nitafute velocity waliyogongana nayo halafu unapasuka then kipande kimoja kinaondoka kwa speed yake na kingine kwa speed yake (data zingine ziliwekwa)

Hapo ndio Deadbody nikanza kushtuka kuwa hata ndege na hewa zinaweza kutumika kwenye projectile motion kumbe.

curv_proj_ep2.png


Aisee nilijiona mweupe sana kichwani na hakukuwa na uwezekano wa mimi kupata 1/100 ule mtihani.

Nikasema isiwe shida,maana kukusanya pepa nyeupe ni aibu acha nijitoe ufahamu nitafute range na maximum height ambazo hazijaulizwa nitapate pa kuondokea nyumbani.

Utaratibu ulikuwa simple sana ,yani ukifanya mtihani week hii,majibu yanatoka week ijayo na sikurudi tena huko mpka dk hii napoandika mada hii sijui ule nilipata A au B na sitaki kujua.

NIKAANZA MAISHA MAPYA



Kama principle ilivyokuwa ,ukiona umeshindwa kushinda nao basi ungana nao.Nikaanza kusoma Physics upya mchikichini na nikagundua nilikuwa sijui chochote aisee maana hata circular motion ingeniumbua.
Dah ngoja niishie hapa aisee maana mzuka ukipanda nitaanza kutoa matusi humu kuhusu Newton Rings (Wave 2 ) na madude ya mule..

NAJUA WATU KAMA MIMI WAPO WENGI HUMU,NAOMBA LEO TUJARIBU KUKUMBUSHIA HUYU MNYAMA 'PHYSICS'

KARIBUNI

cart.gif
Mi nilipigaga pindi la mechanics kwa Mody physics nkajiona tayar nimeshaiva. Tumereport shuleni nkakuta watu wana mavitini makubwa kama schand,nikajaribu kudadis dadis nikaambiwa huyo ndo Mgote. Ikabid siku moja niazime kitini nione utofauti wa notes zake na za Mody, Mmmmh maswali niliyokutana nayo ni balaa tupu mana yale maswali ambayo kwa Moody tuliyaona ni magumu,yeye Mgote ndo aliyasolve kama examples then huko mbele maswali yanazid tu kuwa magumu. Mgote ni hatari, alinifanya niione advance ngumu mno kiasi cha kutaka kubadili combie [emoji1] [emoji1] [emoji1]
 
Nikikumbuka physics nakumbuka advance iyunga, RIP mr doppler, maana mbaba siku ya doppler effect anatiririka mpka unasema dah aya bwana, kwakweli adv physics ilinifanya mbaya iyungani sinaga hamu nayo mazee inakufanya ukose muda wa kupambana na mikate ya bios na chems, ukirudi chem wakutana na mr sudi azingua balaa n prac zake dah
Duuh Doppler alishakufa [emoji15]

Jamaa walimpa jina LA Doppler kwa kuishuka hiyo mada kibabe pale iyunga

Daaah so sad
 
Mkuu na mimi nilipita pale .
By the time tumefika pale tulipata story za Mr.doppler ila Mke wake bado yupo anapika vitumbua kule lumbira, wenywe tulikuwa tunamuita Mama doppler.
Soud nahisi ashastaafu naw .
hahahah Soud mzee mbabe sana nasikia kuna mwaka alitia mkojo kwenye practical ya chemistry.
Mwasile alitusaidia sana mwaka wetu tulifaulu vizuri ofcourse.
Hao wote iyunga niliwaacha Sudi mbabe sana. Namjua Doppler nae nampata na huyu mwasile a very polite teacher hanaga mbwembwe za kijinga .

Na kuna yule madam wa kemia na kuna jamaa mmoja mfupi hi ana umbo dogo hivi daah

Iyunga kitambo sana lumbira ,kalobe,nzovwe,tazara mitaa ya kupunga upepo[emoji2]
 
Sie tumepita nafikir tulikuwa intake ta 3 toka advance ianze, mambo yalikuwa ovyo sana pale, adriano jamaa wa bios bado yupo?
Wewe utakuwa ilikuwa nyuma ya akina japhet HP enzi zile ilikuwa ovyo sana kwakwelj advance iyunga zero za kumwaga angalau saivi wanajitahidi mi nilipita pale o level
 
Hao wote iyunga niliwaacha Sudi mbabe sana. Namjua Doppler nae nampata na huyu mwasile a very polite teacher hanaga mbwembwe za kijinga .

Na kuna yule madam wa kemia na kuna jamaa mmoja mfupi hi ana umbo dogo hivi daah

Iyunga kitambo sana lumbira ,kalobe,nzovwe,tazara mitaa ya kupunga upepo[emoji2]
Yule madam daah afu jina nimesahau tena ila alihamaga iyunga alienda shule ya day uyole hko .
huyo jmaaa mfupi nae nilikuwa nakutana nae mabibo hostel last year alikuwa anamalizia Masters ya physics pale mlimani.
 
Yeah Mkuu sa hivi wanabanwa sana kama watto wa loleza.
Me bado application za physics nqzitumia huku school of engineering.
Engineering is the best though.
Hshahahah pole sana kwa madogo infact inawasaidia pia badala ya kwenye kuzurura mitaani usiku
 
Mi nilipigaga pindi la mechanics kwa Mody physics nkajiona tayar nimeshaiva. Tumereport shuleni nkakuta watu wana mavitini makubwa kama schand,nikajaribu kudadis dadis nikaambiwa huyo ndo Mgote. Ikabid siku moja niazime kitini nione utofauti wa notes zake na za Mody, Mmmmh maswali niliyokutana nayo ni balaa tupu mana yale maswali ambayo kwa Moody tuliyaona ni magumu,yeye Mgote ndo aliyasolve kama examples then huko mbele maswali yanazid tu kuwa magumu. Mgote ni hatari, alinifanya niione advance ngumu mno kiasi cha kutaka kubadili combie [emoji1] [emoji1] [emoji1]
Huyu mgote kutini chake wala sikukigusa ilikuwa shida tupu
 
Umenikumbusha mwalimu Otto pale Forest hill secondary enzi izo
 
Hshahahah pole sana kwa madogo infact inawasaidia pia badala ya kwenye kuzurura mitaani usiku
Yeah kweli Mkuu ..
Ammendment kubwa zimefanyika baada ya yale matukio mawili ya moto 2016.
sa hivi kule nyuma ya Mess kuna fence na wanavaa shamba dress hamna ile kujiachia kama zamani
 
Kweli kabisa mkuu. Kabla ya miaka ya 2000 ilikuwa ukiripoti unapewa dude hilo huku units zikiwa katika inch, yard, feet

Ukipiga swali la kwanza hadi la tano mwisho. Chini hakuendeki [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23]
Unapewa kitabu cha Urusi..University Physics, na kabla 2000 ilikuwa mtu anapewa na sliding ruler inatumika kama calculator
 
Lengo LA kusoma PCB ni kuwa MD a.k.a medical doctor, sasa application ya topic ngumu za pys siion
 
Mock iyo.. lilitoka swali limepikwa balaa la fluid dynamics na nikashindwa kulitembeza.. ile tumetoka kwenye mtihani jamaa wanasimuliana jinsi swali husika lilivyokuwa maji.. kumbe lilitolewa kwenye pam la Mgote, na mimi siyapendi kinoma.. actually mapamphlet ya kibongo na vitabu vya wahindi (chand) nilikuwa sivigusi.. asa kuja kujihakikishia kwenye ilo pam..[emoji55][emoji55] solution ilikua mistari miwili, wakati swali nusu page ya A4.. ni shida!
 
Hahaha Daaah physics ni balaa Kuna T.O mmoja hivi alimaliza 2006 alikuja Kutufundisha sisi tukiwa form 6 tukajiona Vilaza Wote.. vitabu vya Chand...Roger. vyote tuliona Tumemaliza na Hakuna Swali Gumu.. Jamaa Halafu alikuwa ana dharau balaa na Chuo alifukuzwa Kisa Dharau kwa Maprofesa kwahiyo akabak anapiga Tuition mtaani tu na Sifa Kibao na Kuwaona Watanzania wote hawana Akili ila Yeye peke yake

Ila Nakumbuka Siku ya Mtihani wa Physics Nilipiga msuli Usiku halafu kesho yake Pepa Asubuhi Na Nikasolve Maswali Kama matatu hivi ya Chand kwenye Pepa Yamekuja Vile vile Nikasema Nashukuru Mungu Ndalichako kaniona

Ila Yote tisa nitarudi Shule Zote ila Siyo Advance

Huyo jamaa alitoka Tosamaganga,haa haa dah ndie aliniachia darasa akawa anakuja kutupiga pindi,paper ya physics mwaka wake alijibu maswali yote na yote alipata zote wakati mimi hapo niko PCB kila kitu naona hewa tu nikakomaa zangu na C and B [emoji28][emoji28][emoji28]
 
kwakweli hata mimi nitarudi shule zote lkn sio advance ya PCB!
Biology na Chemistry zinatembea lkn Advanced physics hapana aiseee! Topic kama Magnetism, Adiabatic Expansion! Kwakweli A.physics ni nomaaaa.
Nakumbuka nilotoka jasho kwenye Practical baada ya kukuta pendulum la ajaab, unafunga uzi kwenye rula halafu bob inaning'inia kwa kutengeza umbo la pembe tatu! I wont forget
2b2d2de6dda6ca2dc8227dea3e98ca59.jpg

Daah…nimecheka sana na hii comment…yaani pendulum zilikuwa zinabadilisha uelekeo kabisa. Kuna private candidate alipangiwa shuleni kwetu…ndani ya nusu saa akwa anaomba kuhamia swali lingine, sio kuwa kamaliza bali anataka akajaribu swali lingine….
 
Yeah kweli Mkuu ..
Ammendment kubwa zimefanyika baada ya yale matukio mawili ya moto 2016.
sa hivi kule nyuma ya Mess kuna fence na wanavaa shamba dress hamna ile kujiachia kama zamani
Duuh noma.sana wamekuwa mifugo hivi wamekarabati Yale mabweini yote mabweni yamechoka balaa wiring yake imekaa kidanger danger tu daah ile shule enzi zetu ilikuwa hatari sana
 
Back
Top Bottom