Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Yeah kweli Mkuu ..
Ammendment kubwa zimefanyika baada ya yale matukio mawili ya moto 2016.
sa hivi kule nyuma ya Mess kuna fence na wanavaa shamba dress hamna ile kujiachia kama zamani
Mesi kama.kabisa hahahahaj


Kuchafuu moshi tuu ukatani .

Babu chaula mpishi yupo.?
 
Duuh noma.sana wamekuwa mifugo hivi wamekarabati Yale mabweini yote mabweni yamechoka balaa wiring yake imekaa kidanger danger tu daah ile shule enzi zetu ilikuwa hatari sana
Mkuu sa hivi ukienda Iyunga utaikataa. .
imekarabatiwa yote imekuwa mpya kabisa.
 
Mesi kama.kabisa hahahahaj


Kuchafuu moshi tuu ukatani .

Babu chaula mpishi yupo.?
Wale wapishi nilikuwa siwajui hata majina .
Si unajua advnce tulikuwa busy na shule mambo ya jikoni tulikuwa sio sana
 
Nakumbuka siku ya pepa la Physics,,sikuweza swali hata moja,,,sasa kituko siku ya practical,,yaan nilishindwa hata kuunganisha betri. Hatimae nika deferentiate constant kwenye hilo somo. Ingawa Mathematics na GEOGRAPHY nilipata D D. Kiukweli Physics ya Advance inahitaji Uvumilivu.
 
physics_650x400_51489484821.jpg


5aeb30138efc5bd38c3a8aacd40cc677--projectile-motion-the-motion.jpg


Wakuu japo sijapost kwenye jukwaa hili kwa miezi kadhaa sasa hivyo naomba mnipokee tena mtaalamu Deadbody ,

Wakuu najua JF kuna watu wa kila aina ya masomo humu hivyo leo naomba niwakusanye watu wote waliosoma Advanced Physics tuje tukumbushie namna tulivyokuwa tunashangaa ndani ya chumba cha mtihani .

Ngoja nianze mimi aisee kuleta ushuhuda wangu wa kwanza kabisa:

Story inaanzia pale tu kijana Deadbody niliporipoti Advance school mara ya kwanza aisee ambapo nikapokewa kwa furaha sana na watu niliosoma nao Olevel na Primary.

Walinipokea kwa mbembwe sana maana balaa langu walikuwa wanalijua vizuri kuwa Physics na Maths niliumbiwa mimi(hahaha sipo serious hapa).

Nikapokelewa na kuonyeshwa Block nitakaloishi na maisha ya boarding ndio yakaanza rasmi .

TOPIC YA KWANZA KUFUNDISHWA KWA SOMO LA PHYSICS

Kama ilivyomazoea ya shule za advance kuwa walimu hukimbilia kuanza projectile motion,measurements and error hivyo ikawa hivyo hivyo kwa mwwalimu wetu ambaye alikimbilia kuanza na PROJECTILE MOTION.

ProjectileMotion.jpg


Dah aisee nilishangaa sana kuona topic hiyo ikifundishwa ndani ya siku moja na kuisha yote huku ikiwa na formula nyepesi mno kwa mwanafunzi kilaza kama Jesca kuelewa.

Formulas zilikuwa za Range ,height ambapo kila nikigusa swali kwenye kitabu cha CHAND linaenda natia tiki ,nikaanza kujiuliza kwanini watu wanasema hii topic ngumu mbona nimesolve maswali yote aiseeee..

Dah nikahitimisha tu kwa kujiona mimi ndio mwamba ,mwamba wa mathematics na sikwami kabisa swali la PROJECTILE MOTION .Wakati najitamba hivyo kumbe washikaji wananichora tu kuwa huyu dogo kaja kwa mbwembwe tumtazame kwanza ataishia wapi.

Projectile+motion.jpg


Mwendo ukawa ndio ule ule muhuni nikigusa tu maswali ya examples ya mwalimu napasua tena kwa muda mfupi tu.Na kwa jinsi nilivyokuwa na mbwembwe ilikuwa mtu akiniletea swali la projectile naliweka kwenye calculator lote then nikipiga alama ya sawa sawa kitu imooooo.Wenzangu wakawa wananiambia dogo fanya moja moja kupunguza brackets maana zitakuchanganya,ila kwakuwa nataka kuonyesha mimi ni kichwa sichanganywi nikawabishia na kuweka lote.

Aiseee nilikuwa mpenda sifa hatari enzi hizo kushinda hata BASHITE,nikasema likizo hii watanikoma mchikichini huko ndio nitakuwa nasolvia watu kwenye mabanda ya mihogo wakati wa kusubiri pindi .

Dah maisha yanaenda kasi sana na hatimaye nikapewa habari njema na mwanangu mmoja hivi kuwa kwa mgote jumamosi ni mtihani wa PROJECTILE MOTION hivyo nenda kawaonyeshe aisee kuwa wewe ni mwamba Dar nzima.Nikajawa na sifa kama kawaida yangu na kuwaza mda wote kuwa jumamosi inachelewa aisee nikafanye maajabu mchikichini huko.

SIKU YA MTIHANI WA PROJECTILE MOTION IKAFIKA

projectile_motion_prob_2.png


Kwa kujiamini kabisa nikakaa seat ya mbele kabisa maana nilikuwa sitaki mtu anichungulie tusije tukagongana marks tukawa wote wa kwanza wakati mimi nimetumia nguvu kubwa sana na nimekamia show.

Sitasahau hii siku hasa pale nilipoufungua mtihani wa PROJECTILE MOTION na kukutana na Concepts mpya ambazo sijawahi hata kuhisi kama nazo ni projectile aisee.

Kusoma swali hata halina terminologies ngumu kuelewa ila isipokuwa sina cha kuandika baada ya kulielewa lile swali.Hahahah formulas zangu za RANGE na Maximum height zote hazitumiki na ndio nazitegemea sasa hapo.

Ule mtihani na mimi tulikuwa level tofauti kabisa ambapo ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejifunza hesabu za kujumlisha namba zenye tarakimu moja then umtolee hesabu za magazijuto.

Ule mtihani haukuwa standard yangu japo majirani zangu wanaagiza karatasi za kujibia tu baada ya kujaza za mwanzo.Muhuni natamani nisikusanye niondoke hivyo hivyo ila sasa Mgote anayesimamia mtihani ndio kakaa mbele yangu kiasi kwamba hata nikigeuza jicho tu ananiona ,hhahah noma.

Nikakutana na concepts za kitu kina kuwa projected kutoka kwenye gari linaloenda kwa speed fulani na kitu chenyewe kina speed yake aiseee.Wakati huo air unaambia inaspeed yake then natakiwa kutafuta umbali kitakapotua kutokea umbali ambao gari lilikuwepo wakati wa kurushwa.

material-YTA5u3DP.png


Kila nikiangalia naona nashindwa hata kuchora mstari wa range maana kitu kilirushwa kikiwa kwenye height fulani above the ground.

Kiukweli hilo ndio baadae nikaja kugundua lilikuwa swali rahisi kuliko mengine.Hayo mengine ilikuwa balaaa tupu maana hadi ndege wa angani waliokuwa wanatembea walipishana na hiko kitu walichokiproject tena kwa speed tofauti.

Mfano swali lingine lilikuwa linaanzia mbali kinouma kuwa ,ball imeenza kuserereka kwenye umbo lina shape ya U na kuibuka juu na kuendelea na projectile motion na mara gafla ukagongana na body nyingine huko juu hivyo nitafute velocity waliyogongana nayo halafu unapasuka then kipande kimoja kinaondoka kwa speed yake na kingine kwa speed yake (data zingine ziliwekwa)

Hapo ndio Deadbody nikanza kushtuka kuwa hata ndege na hewa zinaweza kutumika kwenye projectile motion kumbe.

curv_proj_ep2.png


Aisee nilijiona mweupe sana kichwani na hakukuwa na uwezekano wa mimi kupata 1/100 ule mtihani.

Nikasema isiwe shida,maana kukusanya pepa nyeupe ni aibu acha nijitoe ufahamu nitafute range na maximum height ambazo hazijaulizwa nitapate pa kuondokea nyumbani.

Utaratibu ulikuwa simple sana ,yani ukifanya mtihani week hii,majibu yanatoka week ijayo na sikurudi tena huko mpka dk hii napoandika mada hii sijui ule nilipata A au B na sitaki kujua.

NIKAANZA MAISHA MAPYA



Kama principle ilivyokuwa ,ukiona umeshindwa kushinda nao basi ungana nao.Nikaanza kusoma Physics upya mchikichini na nikagundua nilikuwa sijui chochote aisee maana hata circular motion ingeniumbua.
Dah ngoja niishie hapa aisee maana mzuka ukipanda nitaanza kutoa matusi humu kuhusu Newton Rings (Wave 2 ) na madude ya mule..

NAJUA WATU KAMA MIMI WAPO WENGI HUMU,NAOMBA LEO TUJARIBU KUKUMBUSHIA HUYU MNYAMA 'PHYSICS'

KARIBUNI

cart.gif
Mtaalamu natafuta walimu wazuri wa physics na chemistry nina mdogo angu nataka nimpeleke tuition
 
Yeah kweli Mkuu ..
Ammendment kubwa zimefanyika baada ya yale matukio mawili ya moto 2016.
sa hivi kule nyuma ya Mess kuna fence na wanavaa shamba dress hamna ile kujiachia kama zamani
Shamba dress [emoji3][emoji3][emoji3][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Huyo jamaa alitoka Tosamaganga,haa haa dah ndie aliniachia darasa akawa anakuja kutupiga pindi,paper ya physics mwaka wake alijibu maswali yote na yote alipata zote wakati mimi hapo niko PCB kila kitu naona hewa tu nikakomaa zangu na C and B [emoji28][emoji28][emoji28]
Haya mzee naona ushakuwa dr wa maua...horticulture
 
Wale wapishi nilikuwa siwajui hata majina .
Si unajua advnce tulikuwa busy na shule mambo ya jikoni tulikuwa sio sana
Naikumbuka luthuli a makazi yangu ya kudumu,vp mng'ong'o alipata yale madini alikuwa anatafuta kule jumba la dhahabu?
 
On namkumbuka mr doppler alikuwa anapiga pindi zake mkizidiwa na materials basi vijembe vinaanza mtakuwa dr wa waua sua huko hahaha

Haaa haaa zamani kama kilimo hakijawa dili ulikua upuuzi kusoma ila sasa hivi hakuna kozi inalipa kama za kilimo na ukaotea mradi mzuri au kampuni
 
Toka nianze Kusoma mpaka leo nipo Pharmacy mwaka wa Tatu SIJAWAHII ONAA SOMO JEURI KAMA PHYSICS...[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji119][emoji119]HAPANA AISEE.... Kilee kidumee sioo
 
kwakweli hata mimi nitarudi shule zote lkn sio advance ya PCB!
Biology na Chemistry zinatembea lkn Advanced physics hapana aiseee! Topic kama Magnetism, Adiabatic Expansion! Kwakweli A.physics ni nomaaaa.
Nakumbuka nilotoka jasho kwenye Practical baada ya kukuta pendulum la ajaab, unafunga uzi kwenye rula halafu bob inaning'inia kwa kutengeza umbo la pembe tatu! I wont forget
2b2d2de6dda6ca2dc8227dea3e98ca59.jpg
Hivi hii sio tishu kweli umechorea mchoro baa?
 
Hahaha UP ilikuwa hatari na zile units zake za inch, yard, ile UP ya njano ile page zake ziko kama unga wa dona hahahaha, kuna kitu inaitwa ROTATIONAL DYNAMICS ilinitesa sana hii kitu asee
Rotational dynamics sijawah kuelewa na ctailewa ni hatariii
 
Back
Top Bottom