Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Advance Physics ilivyokuwa inatugeuka ndani ya chumba cha mtihani

Mgote ndio mwalimu aliyefundisha vizur topic ya projectile...pamphlet lake lilikuwa na solving nondo hatari....ila mnyama adv PHYSICS syo wa mchezoo mchezo...nakumbuka kwny necta ya physics kuna jamaa katikat ya pepa alianza kuliaa ...invigilator anamuuliza vp..anasema pepa haliendii..kitu ilikuwa imekaza hatarii yaani balaah...ila yote hayo elimu ya kibongo ni ya kukariri sana na kufanyia mtihani baasi...tusitegemee kuzalisha wakina elon musk kamwe
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kuliaa kwenye kulia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] [emoji23] kuliaa kwenye kulia hapo

Sent using Jamii Forums mobile app
Physics somo rahis sana i always followed principle na kufanya maswal magum mpaka kichwa kifunguke. ..of coz hakuna somo rahis kwangu kama physics na biology ... I realy loved they are in my blood untill now

a e i o u
 
Hivi vitu sio vigumu. Ugumu uliletwa na tulikuwa tunakariri na kusomea mitihani pamoja na lugha. Hata vichwa wa enzi hizo wengi walikuwa tu na vipaji vya kukariri. Wachache walielewa logic ya hivi vitu.
Sasa hivi nikiangalia swali la advanced physics nacheka na kusema msuli wote ule mbona swali la kawaida sana
 
Hahaha Daaah physics ni balaa Kuna T.O mmoja hivi alimaliza 2006 alikuja Kutufundisha sisi tukiwa form 6 tukajiona Vilaza Wote.. vitabu vya Chand...Roger. vyote tuliona Tumemaliza na Hakuna Swali Gumu.. Jamaa Halafu alikuwa ana dharau balaa na Chuo alifukuzwa Kisa Dharau kwa Maprofesa kwahiyo akabak anapiga Tuition mtaani tu na Sifa Kibao na Kuwaona Watanzania wote hawana Akili ila Yeye peke yake

Ila Nakumbuka Siku ya Mtihani wa Physics Nilipiga msuli Usiku halafu kesho yake Pepa Asubuhi Na Nikasolve Maswali Kama matatu hivi ya Chand kwenye Pepa Yamekuja Vile vile Nikasema Nashukuru Mungu Ndalichako kaniona

Ila Yote tisa nitarudi Shule Zote ila Siyo Advance
Hahaha mkuu acha tu...mim mwenyewe Adv sirudi ayse...yaani nikikumbuka karibia asilimia 70 ya maisha yangu yakusoma Advanved nilitumia kusoma Physics....cha ajabu chemistry na Adv math sikuwa nasoma kihivyo na ndio masomo niliyofaulù kuliko huyu mdudu Physic

Sent from my SM-G532F using Tapatalk
 
Physics ni Nomaaaa Hakuna cha Biology wala Chemistry sijui....wala Economics dadadekiii
Basi tuuuu
Ndiyo maana hata walimu wa Physics wapo wachache mno lkn mwisho wa siku wanalipwa sawa na Mwalimu wa Ngwin,life is not fair
 
Tangu naingia f5 physics nilikua nikiona simple na sion watu wanafeli nini.. miez ya mwisho nikaacha kusoma kabisa.. alaf pepa one nahis nilipata yote, pepa two[emoji26][emoji26] niliona maswal mawili tu.
Mmmmmh
 
Hiyo Projectile motion ilinipa marks zote kwenye pure maths... alaf watu wa egm walikuwa wanaiogopa vibaya mi nikasema nakomaa nayo... kama mtoa mada nikawa nacalculate height, range, angle na kuderive formula tu na swali likaja humo humo!!

Ila wanafunzi wa Advanced Physics kuwen wakweli, ambacho huwa kinawafelisha hasa ni kipi?
Physics Unasoma Leo kesho umesahau,concepts zipo kiimagination zaidi Sasa kuzileta kwenye reality ni shiiida
 
Basi haki yangu kupata E. Shule niliyoenda advance sisi ndo tulikua PCM wa kwanza. Hamna walimu hamna lab hamna chochote. Walimu walikua ni wa O level. Bila kukomaa na tuition na umakini wa nisicheze na hela ya mama ningezungusha zero kubwa tu. Ila PCM sisomi hata iweje. Niko radhi nikasome PhD ila PCM sirudi. Kwanza hata kupata E ilikua miujiza tu.
Hongera mkuu wenzio walimu walikwepo lkn tuliambulia S
 
physics_650x400_51489484821.jpg


5aeb30138efc5bd38c3a8aacd40cc677--projectile-motion-the-motion.jpg


Wakuu japo sijapost kwenye jukwaa hili kwa miezi kadhaa sasa hivyo naomba mnipokee tena mtaalamu Deadbody ,

Wakuu najua JF kuna watu wa kila aina ya masomo humu hivyo leo naomba niwakusanye watu wote waliosoma Advanced Physics tuje tukumbushie namna tulivyokuwa tunashangaa ndani ya chumba cha mtihani .

Ngoja nianze mimi aisee kuleta ushuhuda wangu wa kwanza kabisa:

Story inaanzia pale tu kijana Deadbody niliporipoti Advance school mara ya kwanza aisee ambapo nikapokewa kwa furaha sana na watu niliosoma nao Olevel na Primary.

Walinipokea kwa mbembwe sana maana balaa langu walikuwa wanalijua vizuri kuwa Physics na Maths niliumbiwa mimi(hahaha sipo serious hapa).

Nikapokelewa na kuonyeshwa Block nitakaloishi na maisha ya boarding ndio yakaanza rasmi .

TOPIC YA KWANZA KUFUNDISHWA KWA SOMO LA PHYSICS

Kama ilivyomazoea ya shule za advance kuwa walimu hukimbilia kuanza projectile motion,measurements and error hivyo ikawa hivyo hivyo kwa mwwalimu wetu ambaye alikimbilia kuanza na PROJECTILE MOTION.

ProjectileMotion.jpg


Dah aisee nilishangaa sana kuona topic hiyo ikifundishwa ndani ya siku moja na kuisha yote huku ikiwa na formula nyepesi mno kwa mwanafunzi kilaza kama Jesca kuelewa.

Formulas zilikuwa za Range ,height ambapo kila nikigusa swali kwenye kitabu cha CHAND linaenda natia tiki ,nikaanza kujiuliza kwanini watu wanasema hii topic ngumu mbona nimesolve maswali yote aiseeee..

Dah nikahitimisha tu kwa kujiona mimi ndio mwamba ,mwamba wa mathematics na sikwami kabisa swali la PROJECTILE MOTION .Wakati najitamba hivyo kumbe washikaji wananichora tu kuwa huyu dogo kaja kwa mbwembwe tumtazame kwanza ataishia wapi.

Projectile+motion.jpg


Mwendo ukawa ndio ule ule muhuni nikigusa tu maswali ya examples ya mwalimu napasua tena kwa muda mfupi tu.Na kwa jinsi nilivyokuwa na mbwembwe ilikuwa mtu akiniletea swali la projectile naliweka kwenye calculator lote then nikipiga alama ya sawa sawa kitu imooooo.Wenzangu wakawa wananiambia dogo fanya moja moja kupunguza brackets maana zitakuchanganya,ila kwakuwa nataka kuonyesha mimi ni kichwa sichanganywi nikawabishia na kuweka lote.

Aiseee nilikuwa mpenda sifa hatari enzi hizo kushinda hata BASHITE,nikasema likizo hii watanikoma mchikichini huko ndio nitakuwa nasolvia watu kwenye mabanda ya mihogo wakati wa kusubiri pindi .

Dah maisha yanaenda kasi sana na hatimaye nikapewa habari njema na mwanangu mmoja hivi kuwa kwa mgote jumamosi ni mtihani wa PROJECTILE MOTION hivyo nenda kawaonyeshe aisee kuwa wewe ni mwamba Dar nzima.Nikajawa na sifa kama kawaida yangu na kuwaza mda wote kuwa jumamosi inachelewa aisee nikafanye maajabu mchikichini huko.

SIKU YA MTIHANI WA PROJECTILE MOTION IKAFIKA

projectile_motion_prob_2.png


Kwa kujiamini kabisa nikakaa seat ya mbele kabisa maana nilikuwa sitaki mtu anichungulie tusije tukagongana marks tukawa wote wa kwanza wakati mimi nimetumia nguvu kubwa sana na nimekamia show.

Sitasahau hii siku hasa pale nilipoufungua mtihani wa PROJECTILE MOTION na kukutana na Concepts mpya ambazo sijawahi hata kuhisi kama nazo ni projectile aisee.

Kusoma swali hata halina terminologies ngumu kuelewa ila isipokuwa sina cha kuandika baada ya kulielewa lile swali.Hahahah formulas zangu za RANGE na Maximum height zote hazitumiki na ndio nazitegemea sasa hapo.

Ule mtihani na mimi tulikuwa level tofauti kabisa ambapo ni sawa na mwanafunzi wa darasa la kwanza aliyejifunza hesabu za kujumlisha namba zenye tarakimu moja then umtolee hesabu za magazijuto.

Ule mtihani haukuwa standard yangu japo majirani zangu wanaagiza karatasi za kujibia tu baada ya kujaza za mwanzo.Muhuni natamani nisikusanye niondoke hivyo hivyo ila sasa Mgote anayesimamia mtihani ndio kakaa mbele yangu kiasi kwamba hata nikigeuza jicho tu ananiona ,hhahah noma.

Nikakutana na concepts za kitu kina kuwa projected kutoka kwenye gari linaloenda kwa speed fulani na kitu chenyewe kina speed yake aiseee.Wakati huo air unaambia inaspeed yake then natakiwa kutafuta umbali kitakapotua kutokea umbali ambao gari lilikuwepo wakati wa kurushwa.

material-YTA5u3DP.png


Kila nikiangalia naona nashindwa hata kuchora mstari wa range maana kitu kilirushwa kikiwa kwenye height fulani above the ground.

Kiukweli hilo ndio baadae nikaja kugundua lilikuwa swali rahisi kuliko mengine.Hayo mengine ilikuwa balaaa tupu maana hadi ndege wa angani waliokuwa wanatembea walipishana na hiko kitu walichokiproject tena kwa speed tofauti.

Mfano swali lingine lilikuwa linaanzia mbali kinouma kuwa ,ball imeenza kuserereka kwenye umbo lina shape ya U na kuibuka juu na kuendelea na projectile motion na mara gafla ukagongana na body nyingine huko juu hivyo nitafute velocity waliyogongana nayo halafu unapasuka then kipande kimoja kinaondoka kwa speed yake na kingine kwa speed yake (data zingine ziliwekwa)

Hapo ndio Deadbody nikanza kushtuka kuwa hata ndege na hewa zinaweza kutumika kwenye projectile motion kumbe.

curv_proj_ep2.png


Aisee nilijiona mweupe sana kichwani na hakukuwa na uwezekano wa mimi kupata 1/100 ule mtihani.

Nikasema isiwe shida,maana kukusanya pepa nyeupe ni aibu acha nijitoe ufahamu nitafute range na maximum height ambazo hazijaulizwa nitapate pa kuondokea nyumbani.

Utaratibu ulikuwa simple sana ,yani ukifanya mtihani week hii,majibu yanatoka week ijayo na sikurudi tena huko mpka dk hii napoandika mada hii sijui ule nilipata A au B na sitaki kujua.

NIKAANZA MAISHA MAPYA



Kama principle ilivyokuwa ,ukiona umeshindwa kushinda nao basi ungana nao.Nikaanza kusoma Physics upya mchikichini na nikagundua nilikuwa sijui chochote aisee maana hata circular motion ingeniumbua.
Dah ngoja niishie hapa aisee maana mzuka ukipanda nitaanza kutoa matusi humu kuhusu Newton Rings (Wave 2 ) na madude ya mule..

NAJUA WATU KAMA MIMI WAPO WENGI HUMU,NAOMBA LEO TUJARIBU KUKUMBUSHIA HUYU MNYAMA 'PHYSICS'

KARIBUNI

cart.gif
Nimecheka sana maan nimehis kama unaniongelea mimi Daah advanced physics bana iachen tu maan hata wanaoipata A si kwamba wanaijua bt mtihan unawalenga.
 
Back
Top Bottom