Aende chuoni miaka 5 kisha apewe mtaji au aende kusaidia biashara ya familia miaka mitano kisha afunguliwe biashara?

Aende chuoni miaka 5 kisha apewe mtaji au aende kusaidia biashara ya familia miaka mitano kisha afunguliwe biashara?

Anaweza kwenda shule lakini pia mudavwa ziada woote anatumia kujifunza biashara pia akawa karibu na wafanyakazi na kuwauliza maswali ataua ndege wawili kwa wakati mmoja
Kumbuka sio kwenda chuo tu, kuna GPA ya kuipambania ambayo inabidi apige kitabu, kuchanganya mambo inaweza kumuathiri
 
AENDE CHUONI AKASOME WE LIVING IN THIRD WORLD COUNTRY AENDE CHUONI AKAPTE MAARIFA ZAIDI
 
Anataka kuchelewa tu huyo akimbie mbio nyingi Sana kwenye Biashara hiyo miaka mitano ya Experience atakuwa konki mno
 
Tazama Mo na watoto wa Bakhresa walifanya nini?

Nijuavyo wote walienda kusoma kwanza, walivyorudi wakazikuta biashara wakaendelea na biashara.
 
Kamaliza form 6,

Ni mtoto wa kwanza wa kwanza wa kiume, wa pili yupo form 5 wa kike, wa tatu wa kiume yupo form 1, wa nne wa kiume yupo darasa la saba

Wazazi wanajishughulisha na biashara, mambo ya usafirishaji na makazi.

option mbili


1. Apprenticeship
miaka mitano afunzwe kwa ukaribu biashara ya usafirishaji ili kujua changamoto za magari, kudeal na madereva, kuzijua kodi za kulipa, kuvijua vibali, kutafuta masoko, connections , n.k. kisha akifika 25 afunguliwe biashara ya usafirishaji.

2.University
Miaka mitano chuoni degree na masters ya business administration, akimaliza achague afanye biashara ya chaguo lake mtaji atapewa ama atafute ajira (akitaka) ila kwa sharti apate GPA ya 4.0 au zaidi kwenye degree na Masters.

vinginevyo akipata Gpa pungufu, kuishia degree, kusitisha masomo, n.k. itambidi apitie njia ya mwanzo upya kufunzwa biashara ya usafiri miaka mitano kisha afunguliwe biashara ya usafiri.
Elimu
 
Option 1 inafaa sana hiyo ya pili ni utapeli. Biashara haisomewi darasani
Mim naunga mkono kwenda kujifunza biashara as waasis wake bado wapo. Lkn hii ni kama anajielewa maana atashika hela akiwa mdogo so asipokua makini anaweza kupotea.
 
Back
Top Bottom