Aende degree ipi kati ya hizi: Civil, Mechanical, Electrical, Mineral au Data Science? Matokeo yake ni GPA 1.6 (PCM)

Kama wenye D 2 wanaruhusiwa vyuo vya tiba, iweje mwenye Msingi wa Kemia asiruhusiwe, kwasababu ana basic ya biology?....atatakiwa asome Bios kama somo la ziada
Inawezekana, lakini anahitaji aongeze au ajifunze Biology ili akidhi vigezo vya udaktari.

Asithubutu, bongo sio nchi hii, kila regulator wa elimu ana mambo yake, mimi mwenyewe nishakuwa shamba darasa.
 
Kwahiyo kijana apoteze muda kusomea data. Asome engineering, data science asome kama short course.
 
Data Science asome kama short course.
 
Acha kumsomesha hizi traditional degree... Tafuta Degree ya Mechatronics ndio akasome. hii course nlikua naikubari sana lakini nikaenda electronics engineering udsm kwasababu

Acha kumsomesha hizi traditional degree... Tafuta Degree ya Mechatronics ndio akasome.
Hii course nlikua naikubari sanaa nkaenda electronics engineering udsm nkijua itakua hivi coz n electronics pure sio electronics and telecommunication kama dit au electronics and electrical kama must lakini nmekuta udsm nako imebase kwenye telecom zaidi najitahidi kutafuta chance nihamie kweny instrumentation and automation ili nirud kweny hii fani
 
1. Civil Engineering
2. Data Science
 
Ndio anaweza kuchukua Biomedical Scisnce ni nzuri sana kwa PCM.
Hii haihitaji biology ?

Hio kozi ya biomedical haina mabaraza ya watu wa kozi kama famasia, madaktari, meno nk ? Ambapo ili uje kufanya kazi lazima uwe na leseni zao ?, Inshu ni unakuta TCU qualifications zao wanakuruhusu kusoma afu ukimashamaliza degree yako baraza la kozi husika wanakunyima leseni ya kazi, kisa hukuwa na Biology ya form six.
 
Kwahiyo ajira haiendeshi maisha!!!???
Mantiki yangu ni kwamba kuajiriwa ni moja ya option ndogo kwenye kuendesha maisha.Ukilenga ajira tu unakuwa ni kama una-limit option zako. Chagua wigo mpana zaidi ili hata kama ajira ikiwa adimu unakuwa na option nyingine. Mfano unaweza kulenga shahada ambayo sasa hivi ajira nyingi lakini baada ya miaka kadhaa technology/mazingira yakafanya ajira kuwa ngumu.... kama ulikuwa umewekeza lengo kwenye ajira tu, unakwama. Mkuu, ajira ni jambo linalozidi kuwa gumu hasa kwa sababu ya ujio wa AI, hata Ulaya sasa hivi watu wanafanya shughuli tofauti na walizosomea.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…