Aende degree ipi kati ya hizi: Civil, Mechanical, Electrical, Mineral au Data Science? Matokeo yake ni GPA 1.6 (PCM)

Kwahiyo kijana apoteze muda kusomea data. Asome engineering, data science asome kama short course.
Huwezi kusoma data science kama "short course". Hii ni fani kubwa sana inayoegemea hesabu ngumu kama linear algebra, probability, statistics na calculus.

Degree zote za D.S hapa bongo ni za miaka 4.

Ni kweli kwamba serikali na makampuni binafsi, hasa wale big 4 wa tz(Yas, Voda, CRDB na NMB) wanaipa kipaumbele, na ninaona kweli wanaajiri sana kwenye sekta hii, ila ajira hizo ni chache.

Fani hii ina milango ya kujiajiri pia kwa wale wanaopenda kujiongeza.

Ungeshauri asome computer science ambayo ndo fani mama ya hizi tanzu kama data science na cybersecurity ili awe na uwanda mpana.

Binafsi naona ni bora mtu asome anachopenda tu.
 
Hivi unaijua Data Science?
Pia naona unachanganya Sana kazi za technician na engineer.
Hapo karibu vyote umevuta picha engineer anaenda kufanya kazi za level ya technician. Mhandindisi vs Fundi mchundo.

Hili tatizo watanzania wengi tunalo.
Mechanical Engineer siyo motor vehicle technician.
Civil engineer siyo bricklayer au mason.

Kuna kazi za mhandisi (engineer) fundi uhashi wa kawaida hawezi kamwe.

Mechanical engineering iko broad Sana hadi hydraulics siyo magari pekee.

USHAURI WANGU akasome civil engineering akikosa asome Data Science.

SABABU: Civil engineering ajira bado zipo kuajiriwa na kujiajiri. Serikali na sekta binafsi bado wanatenga bajei kubwa kwenye hii sekta.

Pili hii ni kati ya fani chache ambazo hazita athiriwa directly miaka ya karibuni na AI au na robotics.

Data Science inaendana na kasi ya maendeleo ya teknolojia ya kisasa. Ina complement AI kwa 100%.

Sasa hivi karibu kila sekta data muhimu sana. AI bila data sawa sawa na kumiliki mswaki bila meno. Au jembe la ng'ombe bila kuwa na ng'ombe wa kulimia.

Biashara zote na maamuzi yote ya serikali au kampuni kubwa yanategemea data science.
Telecom industry, Mining, Health, Economics, Business kiujumla, Manufacturing, Energy, e.t.c vinategemea data science kwa sana.
 
Kabla hujamaliza Form six unatakiwa ujue nini unataka kusoma chuo kikuu.

Toa mineral na Data science, akafanye engineering, Data science ni part ya hizo zote

Huyu mtu wako kwenye hivyo vitu ulizotaja ni kama anabet future yake, akianza kusoma atakuwa hana Idea nzuri ya maisha baada ya chuo
 
Mkuu ngoja nikurekebishe kidogo,wapo mainjinia engine wamepitia mtiririko wa ufundi.
Mfano kaanzia labda(Moshi techn,mtwara techn,ifunda,Tanga,au iyunga).Hiyo ni O level,anachaguliwa kwenda MUST,DIT,ATC,(diploma/FTC/NTA levelfour).Halafu anakwenda kuchukua degree yake.
Injinia wa hivi anakuwa yuko vizuri kuliko hao wa mitaani.
Lakini kingine ufundi ni mtu mwenyewe(kipaji)
 
Mwambie akasome petroleum engineering, huko akabobee kwenye gas. Wengi watasema mafuta yanataka kupitwa na wakati. Kuna kitu LPG inakuja Tanzania, kuna mradi mkubwa sana wa kuchakata gas, mpaka mradi unaanza dogo atakuwa ameshamaliza. Akikosa ajira Tz, fursa nje sasa!
 
Shukrani sana kwa uchambuzi
 
Asijaribu kugusa hio Petroleum Engineering atajuta
 
Linear algebra, probability, statistics na calculus hizi zote zipo kwa mtu anayesoma kozi zifuatazo:
1. Bachelor of Mathematics
2. Bachelor of Physics
3. Bachelor of Computer Science
4. Bachelor of Engineering

Kwa hiyo Datance inapaswa kuwa course ndani ya kozi hizo.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…