Afande Faustine Mafwele ni Mzima wa afya. Hajatekwa, hajahojiwa wala kukemewa. Yupo Ofisini kajaa tele kama pishi la Mchele

Afande Faustine Mafwele ni Mzima wa afya. Hajatekwa, hajahojiwa wala kukemewa. Yupo Ofisini kajaa tele kama pishi la Mchele

Hili li Chadema;

Wekeni hizo video zenu tuzione
 
Faustine Mafwele ni afisa wa ngazi ya juu ndani ya Jeshi la Polisi la Tanzania, Assistant Commissioner of Police (ACP) pia ni Zonal Crimes Officer (ZCO) wa Kanda Maalum ya Polisi ya Dar es Salaam Special Zone. Ni kaimu wa Muliro (Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam. Kumbuka huyu ndo Mtuhumiwa namba moja alomteka Sativa.
View attachment 3547443
Kuna habari zimekuwa zikizagaa kwamba sijui Kakamatwana Jeshi, sijui Wamemteka, Wamemjeruhi, wamemuingilia kinyume na maombile, wengine wanasema katolewa jicho nk.

Yaani kwamba kutokana na mauaji yaliyotokea 29 Oktoba 2025, basi naye kwamba Mungu kamuadhibu..

Ukweli ni kwamba habari hizo ni uzushi uongo na uzandiki wa hali ya Juu.

Mimi nimemuona kwa macho yangu Jumapili 22 Februari 2025 akiwa Dar Es salaam. Wala hana shida yoyote na anaendelea na kazi zake kama kawaida. Wala hajabadilisha gari, hajabadilisha walinzi wala hajifichi. Kwa ufupi hakuna anayemtafuta wala kumkera kwa chochote. Mafwele wala hata hajali.. Anachekea shavuni akisoma anavyoandikwa mitandaoni eti kapigwa.

Hata sijui kwanini watu wameingizwa Mkenge wakakubali.

Ila nahisi ni moja ya kazi za TISS kuwashika masikio watanganyika kwani wanajua wanadanganyika.

Wanataka watu Verified wasupport uzushi na matango pori, baada ya hapo ajitokeze.

Wanajua wale wote waliokuwa wanaongelea hili swala watapoteza ushawishi kwa Jamii na hawataaminika tena. Ni moja ya mbinu zinatumika kuwavunja nguvu wanaharakati.

Wanawatumia kwa kuwapa taarifa za Uongo kisha Ukweli unajulikana kinyume na ilivyokuwa inasemwa.

Hii ya Mafwele isingekuwa imepangwa, basi angekuwa anaonekana anatoa matamko kumsaidia Muliro au Polisi wangekanusha.. Polisi wanakanusha habari za mitaani za TTF washindwe kukanusha habari za Boss wao?

Pamoja na yote, siungi Mkono kuhusika kwake katika mauaji ya Watoto wetu 29.10.2025 na siku zilizofuatia..

Nalaani kutekwa kwa Polepole na Rafiki yangu Mdude Nyagali.

Pia nalani wote waliotupa matumaini hewa kwamba Mafwele kafanyiziwa. Ndicho kitu natamani kuona na kusikia lakini kwa huzuni kubwa ni habari za Uongo. Mafwele hakuna hata alomfokea, kumkanya wala kumuangalia kwa jicho la ukali. Inasikitisha sana.

Na anayejiita Kaka wa Polepole naye simuelewi kwani atakuwa anavuta bangi. Anadai eti Afande Mliro alimkimbia ili asimkamate. Muliro akimbie aende wapi. Kwanza hana wasiwasi. Kila siku yupo mtaani wala hajifichi.

Kaka wa Polepole aache bangi.. Anaongea upuuzi tu.. Asitutoe kwenye reli... Sifa za kijinga.

Matamanio yetu ni kuona wote waliohusika kuua watoto wetu wanachukuliwa hatua kwa mjibu wa Sheria.

Tume ya Mzanzibari Samia inahoji wakulima na wafugaji wa Nangurukuru na Sitimbi, badala ya kumhoji Mafwele na Muliro waeleze walitumia mbinu gani kuua na wameua watu wangapi na miili wameizika wapi.

Mara ya kwanza hii tume ya Mzanzibari Samia nilijua tume ya Uchunguzi kumbe ni tume ya kukusanya maoni na mapendekezo ili wampelekee Samia huko Zanzibar.

Wizi mtupu. Ila siku yaja💪


Kwa nini sasa unatumia picha ya kitambo sana,?

Huyo ni Idd Amini anapashwa kutupwa mto wa mamba

Ajitokeze adharani tumone Live bila chenga, vinginevyo no more drama

Picha za zamani sana
Hata akijitokeza hadharani, utajuaje kama amevuliwa ubingwa?

Anyway, mimi binafsi hizo habari sikuziamini toka siku ya kwanza. Na nashangaa sana wanaharakati ambao wengine nawaheshimu wanadandia habari kama hizi.

Kwanza kama mtu unapenda haki kweli, usingependa mtu kama huyo apotezwe maana ni mmoja wa mashahidi muhimu kama siyo washitakiwa wa kwanza wa kwenda ICC.
 
Back
Top Bottom