Afande Kagame: Wanajeshi huwa hawalalamiki?

Afande Kagame: Wanajeshi huwa hawalalamiki?

Afande Kagame siku nyingine najua unapitia pitia mitandao ya kijamii ya Watanzania iliyoandikwa kwa lugha za Kiswahili ama Kingereza kama Jamii Forums na kadhalika.

Afande najua hupendi kuulizwa maswali ila mimi ngoja nikuulize swali, mbona unakuwa muoga wa kurudi frontline kupambana na haya makundi FDLR, RLA, PRA, RUF,PDR na mengine mengi ambayo sijayataja hapa wakati wewe ndio uliwafukuza madarakani tokea 1994?

Unadhani watakaa Congo DRC, Tanzania, Kenya, South Sudan, Burundi, Uganda, USA, Canada na Australia mpaka lini kwenye hali ngumu kimaisha na kiukimbizi wakati Rwanda ni nchi yao pia?

Wengi wa wanajeshi uliowapindua wameshakufa vimebaki vizazi vipya ambavyo dhumuni lao kubwa ni kurudi Rwanda iwe kwa nguvu au kwa demokrasia. Wewe mwenyewe ulikaa Uganda na Tanzania miaka mingapi kama mkimbizi mpaka mjomba Museveni alipokupa mipango ya kurudi Rwanda au umesahau?

Usiogope kupambana afande Kagame, sababu anayeua kwa upanga lazima atauawa kwa upanga. Au umesahau kuwa dunia nayo ilikuwa inaona jinsi RPF ilivyokuwa inaua Wahutu na Wakongomani ndani ya Rwanda na ndani ya Congo DRC majimbo ya Kivu Kaskazini na Kivu Kusini kulipiza kisasi cha genocide ya Watusi ya mwaka 1994 iliyofanywa na serikali ya Habriymana?

Sawa ipo wazi kuwa Habyrimana alikua mbaguzi, katili, mkabila na asiyependa demokrasia hilo linajulikana, ila na wewe toka uchukue madaraka kutoka kwenye kivuli cha Bizimungu umekua kama yeye, hakuna tofauti!

Sasa usiogope kurudi frontline kupambana na ukumbuke kuwa Rwanda hakuna uchaguzi huru toka Mbeligiji aondoke, bali mtutu wa bunduki ndio unaamua mtawala.

Mchawi wala sio Wakongomani au Watanzania au Warundi au Waganda bali mchawi ni wewe mwenyewe uliyevuruga mambo kwa kuukumbatia ukabila na ulevi wa madaraka kama role model wako mjomba Museveni.

Sasa Afande Kagame acha kulalamika kama sio mwanajeshi mbobezi, bali usiogope kurudi uwanja wa mapambano kushika bunduki na kuongoza vikosi na ipo siku usiyotegemea watu watasogea Kigali.

Yaliyomkuta Kanali Doe pale Monrovia na wewe yanaweza kukukuta siku watu wakisogea Kigali na wewe ukiwa haujaondoka ikulu. Au umesahau Mobotu alivyoponea uchupu chupu kule Gabolite alipogoma kuondoka Zaire ya zamani mwaka 1997?

Acha uoga afande, wewe uliingia madarakani kwa mtutu wa bunduki, basi na watu wakitaka kukutoa madarakani kwa mtutu wa bunduki "Usilalamike".
Afande Kagame ni mkombozi na mlinzi wa jamii ya kitusi hapa maziwa makuu
 
Afande Kagame ni mkombozi na mlinzi wa jamii ya kitusi hapa maziwa makuu
Hakuna tofauti kati ya jamii za kitusi na jamii nyingine hapa maziwa makuu.Afande ni mbinafsi,mpenda madaraka na askari muoga anayeogopa kurudi frontline.Tatizo jamii za watusi hapa maziwa makuu ni wabinafsi,wapenda madaraka na wabaguzi,na afande Kagame ana hulka hizo hizo kupendelea watu wa jamii zake.
 
Hakuna tofauti kati ya jamii za kitusi na jamii nyingine hapa maziwa makuu.Afande ni mbinafsi,mpenda madaraka na askari muoga anayeogopa kurudi frontline.Tatizo jamii za watusi hapa maziwa makuu ni wabinafsi,wapenda madaraka na wabaguzi,na afande Kagame ana hulka hizo hizo kupendelea watu wa jamii zake.
Afande Kagame aliwaokoa watusi wa Rwanda na maafa mwaka 1994 na baadae Wanyamulenge wa huko Drc dhidi ya dhulma za Mobutu......hii jamii imeonewa Sana hapa maziwa makuu.
 
Afande Kagame aliwaokoa watusi wa Rwanda na maafa mwaka 1994 na baadae Wanyamulenge wa huko Drc dhidi ya dhulma za Mobutu......hii jamii imeonewa Sana hapa maziwa makuu.
Unazielewa siasa za rwanda Mkuu,since independence
 
We Mrundi unashida kweli kweli, haya kamata huo mtutu basi ukamtoe maana nanona General Kagame is living rent free in your head.
Mkuu umecatch feelings mimi kutoa maoni yangu up here??????Mtutu waga haukamatwi bali unashikwa mkuu,warundi wanaweza kukusaidia katika hili.Na kuna tofauti ya ujenerali wa kujipachika na ujenerali halisia.
 
Nipo ingawaje sina cha kuchangia
JamiiForums790734876.jpg
 
Back
Top Bottom