Afande Sele atashtakiwa kwa kosa gani baada ya kumtukana Mungu?

Afande Sele atashtakiwa kwa kosa gani baada ya kumtukana Mungu?

Asipokufa itadhihirisha kwamba dini zao Ni ushuzi tu na ntaanza kuabudu bange pamoja na Afande. Nahesabu siku kuanzia leo.
Asipokufa itadhihirisha kwamba Mola anaamua atakalo yeye na sio watakalo waja.

Qur an 81: 29 Allah anatuambia kwamba "And in no way can you decide except "when" Allah "so" decides, The Lord of the worlds".

Katika mapokeo mangine tunaambiwa, Laiti wangekusanyika wanaadam wa dunia nzima kutaka kumdhuru ambae Allah hajataka adhurike basi hawatoweza kumduru mja huyo, na ikiwa watakusanyika wanaadam wa dunia nzima kutaka kumnufaisha ambae Allah hajataka anufaike basi hawezi kunufaika mtu huyo.

Kwahiyo mkuu wewe hesabu siku na zikifika nenda kaabudu bange, wala hunikomoi mimi wala mhumkomoi Kishki.
 
Hii tafsiri yake ni pana, vyombo vya ulinzi vinapaswa wamshikilie Afande mapema, kifo kinachoombwa hapo kinaweza kuwa na maana nyingi..

Afande sele amekosea big time, ila hii pia sio sawa, sababu hapo hata plot ikitengenezwa Nani atakayejua? Kuthibitisha maombi yao.

Mungu aliyemtukana na kumkashifu afande ni Mungu wa wote, sina maana ya kumtetea, ila hii sina uhakika Kama iko sawa🙏🙏imani
Umesema sawa kabisa mkuu.
 
Usipotoshe mkuu!

Hawa watu kina nani?

Wala usizungumze for the sake of kuzungumza tu.
Sina haja ya kupotosha mkuu!
Nilimaanisha watu wa rangi hiyo (Arabs?) Huyu anafaa kuongozwa ili atoke kati mwenendo wake huo. Naamini kama angekua nchi za Uarabuni angeuawa
 
Hivi ikitokea afande sele ,akatubia na kuomba msamaha kwa mola wake ,na wakamalizana kimya kimya,itakuweje na hao mashekh?

kilichopaswa kwa hawa mashekh ,ni kumlingania na kumweleza makosa yeka ,

kuna mtu alikufuru kama firauni mpaka kujiita mungu,ila mbona hakuombewa kifo?

watu wasichojua mungu ni wetu sote ,wema na waovu ,mungu huyo huyo ,na pia hata huyo muovu anaweza akamrejea mungu wake mpaka hamtaamini ,ebu warudi kwenye Tarekh(historia) ya wema waliotangulia ,wote walitokea kwenye uwovu ,

mtume alipigwa mawe twaif ,lkn hakuwaombea dua mbaya ,bado alikuwa na matumaini huwenda katika hao walompiga mawe atazaliwa wema katika wao ,

Ni vyema mashekh wapunguze jazba na mhemko ,na wawe viongozi wa kuwaongoza watu wanapopotea kabla ya kuhukumu ,bora wangemwita ama kumnasihi na kama angekataa au kupinga labda hapo wangekuwa na pakuanzia ,

mtu hujamwita hujamwelimisha au kumweleza kosa lake ,maana huwenda yeye akawa anajiona yuko sawa kwa mujibu wa imani yake ,

TUSIPENDE KUADHIBU ,MTOTO HAFUNDISHWI KWA KUMCHAPA BILA KUMWAMBIA KOSA LAKE ,MWELEZE KOSA LAKE ,MPE NAFASI YA KUJISAHIHISHA KWANZA NA KAMA ATAREJEA MAKOSA HAPO SASA MNAPO PAKUANZIA
well said!
 
Apo mnachochea moto tu, Afande asipokufa kabla ya hio ramadhani huoni kuwa atapata nguvu zaidi ya kudharau dini?

Watu kama yule jamaa ni wa kuwaacha tu.
Fact na Mungu huwa mda mwingine hahangaiki na Mambo madogo Kama haya!
 
Sina haja ya kupotosha mkuu!
Nilimaanisha watu wa rangi hiyo (Arabs?) Huyu anafaa kuongozwa ili atoke kati mwenendo wake huo. Naamini kama angekua nchi za Uarabuni angeuawa
Kwahiyo ndugu now tunatambuana kwa rangi zetu?????

Sheikh Kishki ni Mtanzania wa kuzaliwa, kukulia, kusoma na kila kitu chake. Tusiwe na hulka hii.....

Anayo fanya Sheikh kishki kwa nchi yake (Tanzania) baadhi yetu wala hatujawahi kuyafanya na hatutaweza kuyafanya kamwe.

Kuhusu afande sele angekuwa nchi ya kiarabu angeshauwawa huo ni mjadala on it's own.
 
Kwahiyo ndugu now tunatambuana kwa rangi zetu?????

Sheikh Kishki ni Mtanzania wa kuzaliwa, kukulia, kusoma na kila kitu chake. Tusiwe na hulka hii.....

Anayo fanya Sheikh kishki kwa nchi yake (Tanzania) baadhi yetu wala hatujawahi kuyafanya na hatutaweza kuyafanya kamwe.

Kuhusu afande sele angekuwa nchi ya kiarabu angeshauwawa huo ni mjadala on it's own.
Aisee ndio leo namsikia huyu shekhe, BTw Naomba radhi post yangu kama itakua haina maadili.
 
Back
Top Bottom